Na Darlin Said
SEKTA ya elimu ni miongoni mwa sekta
muhimu katika kuhakikisha Serikali inafikia malengo yake ya milenia ya kukuza
uchumi na kuleta maendeleo hapa nchini.Kuthibitisha hilo, kuna msemo unaosema kuwa elimu ndio
ufunguo wa maisha, msemo huo ukiwa na maana ya kuwa bila ya elimu hakuna
maendelo.
Elimu ikipewa kipaumbele itasaidia
kuwepo kwa wataalamu katika sekta mbalimbali hali itakayosaidia kupiga hatua
kimaendeleo na kuondoa umaskini katika jamii
.Kwa kulitambua hilo Mamlaka ya
Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) mbali na majukumu yake,
imekuwa mstari wa mbale kuhakikisha walimu wanajiunga na hifadhi ya jamii ili
kufikia malengo yao pamoja na kuwa salama katika sehemu zao za kazi ili waweze
kutoa elimu iliyo bora.Hivi karibuni SSRA ilifanya kongamano
liliowahusisha Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ambalo lilifanyika mkoani
Morogoro.
Katika kongamano hilo Afisa Mwandamizi wa SSRA, Bw.Frank
Kilimba anasema chama hicho cha walimu CWT kina jukumu la kuwakilisha maslahi
ya wanachama wake katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.Pia Bw.Kilimba anasema CWT lazima
ihakikishe inatoa elimu na uhamasishaji kuhusu Hifadhi ya Jamii miongoni mwa
wanachama wake ambao ni walimu.
“CWT kwa kufanya hivyo itawasaidia
walimu walio wengi hasa waliopo vijijini kujiunga na mifuko hiyo ili waweze
kujikomboa hasa baada ya kustaafu,”anasema Bw.Kilimba.Mbali na walimu Bw. Kilimba anatumia
nafasi hiyo kuelezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo katika
uhamasishaji wa shughuli mbalimbali kwa lengo la kuongeza wigo wa hifadhi ya
jamii kwa watu wote.
“Hivi sasa kila Mtanzania aliye katika
ajira binafsi au anayejiajiri anaweza kuamua kujiunga na kuchangia Mfuko wa
Msingi wa Hifadhi ya Jamii anaoupenda.
Anasema kwa mujibu wa takwimu za SSRA
mwaka 2011 takribani watu milioni 1.5 ndio waliokuwa katika huduma za hifadhi
ya jamii na hadi kufikia mwaka 2012 pamekua na watu milioni 1.7 ambayo ni sawa
na ongezeko la asilimia 13.Hivyo SSRA inafanya kazi bega kwa bega
na vyama hivyo vyenye kusimamia maslahi ya wafanyakazi hasa katika masuala ya
hifadhi ya jamii ili kumsaidia mfanyakazi pamoja na kuleta maendeleo hapa
nchini.
A l i o n g e z e a k w a kusema waajiriwa
au wanaojiajiri wanayo haki ya kujiunga na mifuko ya hiari wanayoipenda ili
waweze kujiwekea akiba itakayowasaidia pale watakapohitaji hasa baada ya
kustaafu.
Mbali na hilo anasema mfuko unatakiwa kutoa namba
maalumu na kadi ya uanachama kwa kila mwanachama wa mfuko husika.
Wakati huo huo, Bw.Kilimba anasema kuwa
kwa hivi sasa ni haruhusiwi mwajiri yeyote kumchagulia mwajiri wake mfuko wa
hifadhi ya jamii tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.Bw.Kilimba anaongezea kwa kusema
vilevile mfuko mmoja haupaswi kumwandikisha kwa mara ya pili mwanachama ambaye
tayari ameandikishwa na mfuko mwingine wa msingi.
“Muongozo huu auhusu Mfuko wa Bima ya
Taifa (NHIF) na Mifuko ya Hiari (Supplementary Scheme),” Bw. Kilimba aliongezea
kwa kusema.Mbali na hilo anatoa wito kwa waajiri
kujitahidi kutoa fursa sawa kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii kuweza kutoa
elimu ya mipango ya mafao kwa wanachama, kwa namna yoyote mwajiri asitoe tamko
wala mwelekeo wa kumtaka mwajiriwa kuwa mwanachama wa mfuko fulani.
Anasema kufanya hivyo ni kumnyima
mfanyakazi haki ya uhuru wa uchaguzi wa mfuko anaoupenda mwajiriwa.Aidha nasema mifuko ya hifadhi ya jamii
ina wajibu wa kutoa elimu kuhusu haki, wajibu, taratibu za kujiunga na kupata
mafao.
Awali Bw. Kilimba anasema mfuko wa
hifadhi ya jamii kwa hivi sasa hauruhusu mwanachama yeyote kuhama kutoka mfuko
mmoja kwenda mwingine.Anasema mwanachama mtarajiwa anaweza
kuchagua mfuko wa kujiunga, pia na yule anayekaribia kustaafu anaweza
kuunganisha vipindi vyake vya uchangiaji kutokana na mabadiliko ya ajira yake
alijikuta amechangia mfuko zaidi ya mmoja.
SSRA inaendelea kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Hifadhi ya Jamii ili kuleta ustawi
na maendeleo kwa wananchi.
Anasema jitihada hizo ni pamoja na
mamlaka kurejea kanuni na sheria mbalimbali, tathmini za mifuko ya hifadhi ya
jamii, kurejea vikokoto vya mafao, mifuko kufanya mikutano ya mwaka kwa
kuwahusisha wadau mbalimbali pamoja na jitihada nyinginezo nyingi zinazoendelea
kuboresha sekta hii.
Pia anasema SSRA ipo katika mchakato wa kufanya
mabadiliko ambayo yatamuezesha
No comments:
Post a Comment