Gladness Theonest na
Ester Maongezi
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Philip Mulugo amesema kuwa Serikali ina jukumu la kuhakikisha inatoa
elimu bora kwa wananchi wake na katika hali ambayo kila mtu anaweza kugharamia.Kauli hiyo
ameitoa jana jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza udhamini wa maonyesho ya
kwanza ya elimu kwa mwaka huu yatakayojulikana kama Vodacom Elimu Expo 2013.
Maonyesho
yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni na kupewa maudhui ya ‘Elimu Bora ndio
Tegemeo la watoto wetu, Tuijenge kwa Pamoja’.Mulugo alisema
kuwa, wananchi walio wengi wanaangalia ubora wa elimu na si kiwango cha ada na
ndio maana katika kipindi cha nyuma wengi wao walikuwa wakipeleka watoto wao
kupata elimu nje ya nchi.
Alisema kuwa, serikali na wadau mbalimbali
wa elimu nchini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujenga shule na kuweka huduma
zote, hivyo kuna haja ya kugharamia huduma hizo ili huduma bora ya elimu iweze
kupatikana nchini.“Kwa kuliangalia hilo serikali
inatafuta jinsi ya kutoa ada elekezo kwani elimu si biashara bali ni huduma kwa
kuweka kiwango fulani ambacho kitafanya kila mwananchi aweze kukimudu kwa
kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa wananchi wote na kwa gharama nafuu,”
alisema Mulugo.
Naye Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa
Vodacom, Kelvin Twissa alisema kuwa matumaini ya Vodacom Elimu Expo yatasaidia
kusuluhisha changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya elimu nchini.Twissa alizitaja moja ya changamoto
hizo kuwa ni pamoja na kulipa ada ya shule kwa kupanga foleni jambo ambalo linaonyesha
kupoteza muda mwingi katika mistari mirefu ya benki.
“Ni jambo la kusikitisha kabisa
kuchelewa kulipa ada ya shule kwa sababu ya foleni zilizopo katika benki zetu,
Kampuni ya Vodacom imekuja na njia ya kitatua changamoto hii na sasa kuna
uwezekano wa kulipa ada ya shule kupitia M-Pesa , hivyo tunawasihi wadau wa
elimu wanaomiliki shule kuanza kutumia huduma hii,” alisema Twissa.
Naye Mkurugenzi wa Elimu Expo Solution
Tanzania Limited, Joel Njama aliwataka wadau wa elimu nchini kujitokeza kwa
wingi katika maonyesho hayo na kusaidia elimu katika nyanja tofauti kutokana na
elimu kuwa ndio ufunguo wa maendeleo katika Taifa hili kubwa la Tanzania.
Maonyesho hayo ya siku tatu yanatarajia
kufanyika kuanzia Agosti 30, mwaka huu na yamedhaminiwa na makampuni ya Vodacom
Tanzania na Elimu Solutions Tanzania Limited.Aidha, yamelenga kuwahusisha wadau wa
elimu katika kuangalia mi a n y a i l i y o p o , k u g u n d u a changamoto na
kutafuta suluhisho la kupeleka elimu bora kwa Watanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment