Na Said
Hauni, Lindi
MKUU wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amewataka
wananchi wa Kanda ya Kusini kutunza mazingira ikiwemo kuacha tabia ya uchomaji
moto na ukataji wa miti ili kuepusha nchi kugeuka jangwa.
Mwananzila alitoa rai hiyo
jana wakati akifungua warsha kwa wadau wa hifadhi ya misitu (Mjumita na
Mkuhumi) iliyofanyika mjini Lindi.
Akifungua warsha hiyo
iliyojumuisha washiriki wa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma alisema misitu ina
mchango mkubwa ikiwemo kujitengenezea chakula chake na kunyonya hewa ukaa kwa
kutoa hewa safi na kuhifadhi hewa chafu katika udongo mara mbili zaidi ya
kiwango chake katika dunia.
Mkuu huyo wa mkoa alisema
tabia ya ukataji miti ovyo mara nyingi imekuwa ikichangia uharibifu wa
mazingira na hivyo kuongezeka kwa hali ya joto kali inayosababisha madhara kwa
nchi kutokana na kukosekana kwa mvua ya uhakika.
Mwananzila alisema iwapo
mazingira hayatalindwa upo uwe z e k a n o mk u bwa wa kuongezeka kwa joto,
majangwa, vimbunga, mafuriko, bahari kuendelea kujaa maji kutokana na kuyeyuka
kwa barafu.
Alisema Serikali kwa upande
wake imeipa kazi Mjumita katika kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya mpango
wa Mkuhumi katika ngazi za vijiji na Taifa kwa lengo la kujenga uelewa na
kupata maoni ya wananchi juu ya upashanaji habari pale utaratibu wa biashara ya
hewa ukaa utakapokuwa tayari katika ngazi za kimataifa.
Pia aliyaagiza mashirika ya
Mjumita, Mkuhumi, taasisi nyingine na jamii yaliyopo ukanda wa Kusini yafanye
kazi kwa ushirikiano wa pamoja ili kuleta mafanikio kwa kanda nzima ya Kusini
na Taifa kwa ujumla.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi
alisema hewa ukaa huzalishwa zaidi ma nchi za mataifa makubwa yaliyoendelea
kutokana na viwanda vyao huku nchi za Afrika zikizalisha Oksijeni ya kwenye
miti yao ya mali asili.
Kwa upande wake Mshauri wa
masuala ya misitu mkoani humo, Mwinjuma Mkungu alisema lengo la mafunzo hayo ni
kuwapa elimu wadau, watendaji wa Serikali ngazi za halmashauri na vijiji ili
kulinda mazingira ikiwemo misitu.
Aidha,
alisema semina kama hiyo ilishafanyika katika Kanda ya Nyanda za Juu (Mbeya)
Kanda ya Kati (Dodoma) na Kaskazini (Arusha) na kujumuisha washiriki 243 na
kuongeza hadi mwisho wa semina hiyo itakuwa imehusisha washiriki 343 na
kuongeza kuwa semina nyingine itafanyika katika Kanda ya Mashariki (Dar es
Salaam
No comments:
Post a Comment