29 July 2013

RAIS KIKWETE AZINDUA WILAYA YA KYERWA



 Na Mwandishi Maalum, Karagwe
RAIS Jakaya Kikwete, amezindua rasmi Wilaya Mpya ya Kyerwa katika Mkoa wa Kagera.Hafla za uzinduzi wa wilaya hiyo iliyofanyika juzi katika eneo la Nkwenda na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Kyerwa. Rais Kikwete alisema wilaya hiyo imeanzishwa miaka mwili kutokana ahadi yake mwenyewe Juni, mwaka 2010.

Wilaya hiyo iliyokuwa sehemu ya Wilaya ya Karagwe ina tarafa nne, kata 18 na vijiji 84 na watu 321,026 . Wilaya ya Kyerwa inatarajiwa kuwa na madiwani 23 ikiwa ni pamoja na madiwani 18 wa kuchaguliwa kutoka katika kata zote 18 za Wilaya hiyo.Rais Kikwete aliiagiza Wizara ya Ujenzi kuanza maandalizi ya kuijenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Bugene, Karagwe kupitia Wilaya ya Kyerwa hadi Mulongo kwenye mpaka wa Tanzania na Rwanda.
Wa k a t i h u o h u o , Ra i s Kikwete, Kikwete jana alizindua rasmi Kivuko cha Mv Ruvuvu kitakachofanya kazi kwenye Mto Ruvuvu katika eneo la Rusumo, Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera.Rais Kikwete amezindua Mradi Mkubwa wa Kusambaza Umeme katika vijiji 12 vya Wilaya ya Karagwe katika sherehe iliyofanyika katika Kijiji cha Nyakayanja, Nyaishozi wakati akiwa njiani kutoka Wilaya ya Ngara kwenda Wilaya mpya ya Kyerwa.
Rais Kikwete amezindua miradi hiyo miwili ya kivuko kipya na mradi wa umeme ikiwa ni moja ya shughuli zake za kukagua miradi ya maendeleo katika ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Kagera. Miradi hiyo yote imegharamiwa na Serikali ya Tanzania.Kivuko cha Mv Ruvuvu kinachukua nafasi ya kivuko cha zamani ambacho kimezeeka na kilikuwa kimeanza kuonekana hatari kwa wasafiri waliokuwa wanatumia kivuko hicho.
Kivuko hicho kilichonunuliwa kwa thamani ya sh bilioni 2.9 kilijengwa nchini Uholanzi, kina uwezo wa kubeba abiria 50 waliokaa, abiria 30 waliosimama na magari matano madogo.Ak i z u n g umz a k a b l a y a kumwalika Rais Kikwete kuzindua kivuko hicho, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, alisema kuwa kuzinduliwa kwa kivuko hicho ni mwanzo wa uzinduzi wa vivuko 25 ambavyo tayari ujenzi wake umekamilika ama unakamilika ama karibu kuanza na ambavyo gharama zake zote zinalipwa na Serikali ya Tanzania.
Baadhi ya vivuko hivyo ni Mv Ujenzi (Ukerewe), Mv Musoma (eneo la Kinesi Mkoani Mara), Mv Karambo, Mv Msanga Mkuu, Mv Ilagara, Mv Kaunda na kivuko kikubwa kitakachofanya safari zake kati ya Dar Es Salaam na Bagamoyo kwa nia ya kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam.
Kivuko hicho cha Dar es Salaam- Bagamoyo kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 kwa wakati mmoja na kitajengwa kwa gharama ya sh bilioni tisa.Dkt. Magufuli pia amewaambia wananchi kuwa wanafunzi wenye sare za shule watatumia kivuko hicho cha Mv Ruvuvu bila malipo yoyote kama ilivyo sera ya Serikali kwa vivuko vyote nchini kwa wanafunzi.
.

No comments:

Post a Comment