17 July 2013

MSAFARA WA PINDA WAPATA AJALI


 Mwandishi Wetu, Namtumbo
MSAFARA wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, umepata ajali iliyohusisha magari manne na kusababisha Katibu wa Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma (RPC) Moses Konala na Ofisa Kilimo wa mkoa huo, Andrew Tarimo, kupata majeraha madogo usoni na kichwani.
Ajali hiyo ilitokea juzi mchana wakati msafara huo ukitoka wilayani Tunduru kwenda Namtumbo. Waziri Pinda yuko mkoani hapa kwa ziara kikazi.

Mi o n g o n i mwa ma g a r i yaliyohusika katika ajali hiyo ni la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii chini ya Mpango wa Chanjo wa Taifa ambalo liliharibika vibaya.
Gari hilo ndilo walilopanda waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma waliomo kwenye ziara hiyo.
Mmoja wa mashuhuda alisema wakiwa njiani kwenda Namtumbo msafara huo ulisimama ghafla katika Kijiji cha Namijigwela wilayani Namtumbo na kutokana na vumbi kubwa madereva wa magari mengine walishindwa kuona mbele na kusababisha magari hayo kugongana.
Magari yaliyopata ajali ni DFP 6627 lililokuwa likiendeshwa, Jordan Nchimbi, gari la polisi PT 1437 ambalo lilikuwa na askari na lingine lenye namba STK 7919.
Gari lingine lilikuwa na namba DFP 8709 lililokuwa likiendeshwa na Faraja Ngonyani. Kamanda wa polisi hakupatikana kuzungumzia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment