Na Ester Maongezi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo
inatarajia kusikiliza kesi inayomkabili mwanamuziki nguli nchini Judith Wambura
'Lady Jaydee' dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group.Kesi hiyo
ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya
Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo
. Kwa mujibu wa
mdai huyo ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni
Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia Blogu yake.Kesi hiyo
ambayo ilitakiwa kuanza kusikilizwa Mei 27, mwaka huu na Hakimu Mkazi wa
Mahakama hiyo Athumani Nyamlani i l i s h i n d w a k u s i k i l i z w a k u t
o k a n a n a u p a n d e w a mdai kushindwa k u f i k a M a h a k a m a n i
hapo.
Hivyo ikapangwa Juni 13, ambapo pia kesi ilishindwa kusikilizwa kutokana na mdai kutokufika kwa mara ya pili na kupangwa kusikilizwa tena leo.Kwa mujibu wa Wakili wa Lady Jaydee, Mabere Marando aliyekuwepo Juni 13, alisema endapo mdai atashindwa kufika tena mahakamani hapo kwa mara ya tatu basi mteja wake anaweza akamfungulia kesi ya madai ya usumbufu kwa kumpotezea muda mteja wake..
No comments:
Post a Comment