05 July 2013

KUKUA NA KUSHUKA KWA NCHI YA MISRI

Na Salim Nyomolelo
NCHI ya Misri ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye historia kubwa licha ya kukumbwa na migogoro ya kisiasa ya mara kwa mara ambapo juzi tumeshuhudia kutolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Bw. Mohamed Morsi ambaye amedumu madarakani kwa mwaka mmoja kutokana na kuendesha nchi kwa kuweka mikakati mikali ya dini ya kiislamu na kusababisha wananchi kumpinga.
Bw. Morsi alichukua nchi hiyo kutokana na uchaguzi uliofanyika kupitia chama chake cha Muslim Brotherhood baada ya kutoka kinguvu kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo mwaka mmoja uliopita, Bw. Hosni Mubarak ambaye alidumu madarakani kwa miaka mingi na kushindwa kukuza uchumi wa nchi hiyo.
Historia ya Misri
Mizizi ya utaifa wa Misri ilianza kipindi cha karne ya 18 ambacho kinaangaliwa kama maabara ambapo Misri ilitungwa. Maelemeo matatu katika karne hiyo yaliashiria mielekeo mitatu, kwanza ni mageuzi ya watu kama Bw. Ali Bey al-Kabir yaliyojaribu kupunguza idadi ya miundo ya kikabaila iliyodhibitiwa na mamluki katika delta ya nchi hiyo, kuwepo kwa vuguvugu la uhuishaji katika Uislamu lililoongozwa na Sheikh Hassan al-Attar pamoja na kuibuka katika majiji ya Cairo na Alexandria kwa kikundi cha watu mashuhuri, wasomi na wafanyabiashara, waliotajirika hasa kutokana na ardhi ambao waliokuwa tayari kutoa rasilimali zao kuendeleza juhudi ya kitaifa.

Hayo yote yaliungana na mambo mengine na kuzaa vuguvugu la kitaifa la Misri lililokuwa na athari kubwa iliyoenea kote. Uhamishwaji wa jeshi la wavamizi wa Kifaransa mwaka 1801 ulitoa nafasi kwa vuguvugu la kitaifa la nchi hiyo kujiimarisha na kujitawala ndani ya himaya ya Kituruki ambapo hadi kufikia mwaka 1805 ilikuwa ya jimbo la himaya ya Kituruki.
Wazo la kujenga Misri huru halikutoka kwa Bw. Pasha kwa jeshi la Makhufu la jumuiya ya Jenerali Yakub lilikuwa tayari limetangazwa ambapo vuguvugu lao lilivunjika kutokana na kumalizika kwa msafara wa Wafaransa na kuondolewa kwa kiongozi wao. Wafaransa walihimiza wazo la Misri huru kupinga utamalaki wa Waingereza ambapo fikra za Bw. Pasha kuhusu uhuru wa Misri zilitofautiana na fikra za Waingereza na Wafaransa.
Baada ya kushika madaraka huko Misri, Bw.Ali alijizatiti kuimarisha nafasi yake na kulijenga taifa ambapo katika harakati hizo mwaka 1807 aliwashinda Waingereza ambao walikuwa wakifanya hujuma dhidi ya mamlaka yake.
Hata hivyo Bw. Ali alikomesha athari za mamluki katika Misri ya Juu, hasa kwa walioshirikiana na Waingereza. Mnamo mwaka 1811, aliwafuta viongozi wa upinzani wa mamluki ambao walikwamisha juhudi za kupata mamlaka ya kisiasa katika Misri ya Chini na baada ya kuwaondoa Mamluki, Bw. Ali alishughulikia ujenzi wa himaya na jukumu la kujenga taifa.
Ibrahim Pasha ambaye ni mtoto wa Bw. Muhammad Ali Pasha ambaye alikuwa jenerali mkuu aliyashtua mataifa ya Ulaya kutokana na ushindi wa awali alioupata kutoka kwenye vita kati ya Uturuki na Misri. Mataifa ya Ulaya yaliamua kumuokoa Sultani wa Uturuki kwa sababu walijua kuwa Bw.Pasha angeachiwa kuiangamiza himaya ya Kituruki na kuanzisha mamlaka yake ya upanuzi wa ukoloni wao ungepingwa na majimbo mengine ya himaya ya Kituruki yangehuishwa na kuimarishwa chini ya uongozi wake.
Katika kipindi cha mwaka 1863 hadi mwaka 1879 aliyerithi baada ya tawala fupi za Bw. Al-Abbas na Bw. Said aliona kuwa tatizo la kitaifa lilihusu uhuru na kujitawala kitaifa. Alibuni mkakati wa kupunguza utegemezi wa Misri kwa Uturuki kwa njia ya mazungumzo ambapo baadaye angeifanya Misri iwe nchi huru na kisha angeanzisha asasi za serikali ya ndani.
Ili kuimarisha nafasi yake, alianzisha mfumo wa kurithishana ufalme wa Misri na akapata cheo cha Khedive. Pia alijitwalia haki ya kutangaza sheria za kiutawala na ya kujadiliana juu ya mipango ya kiuchumi na nchi za kigeni bila kulazimika kuidhinishwa kwanza na Sultani ambapo mwaka 1873 aliifasili Misri kama Taifa ama Dola.
Hata hivyo, madaraka waliyokuwa nayo watu wa Wamultazim juu ya ardhi yalionekana kwamba yangekwamisha maendeleo ya Misri kama taifa unganifu la kisasa. Ili kutatua tatizo hilo, Bw. Pasha alibuni sera ya mgawanyo wa ardhi ambapo ardhi yote inayofaa kwa kilimo nchini iligawanywa katika makundi sita ambazo ziligawiwa kwa matabaka ya familia ya Bw. Pasha na maofisa wa kijeshi, Mamluki, Maulama, watawala wa kigeni nchini Misri, wakulima wadogo wadogo pamoja na Mabedui.
Sera hiyo ya mgawanyo wa ardhi haikupokewa vizuri na watu hususan wale waliopokonywa ardhi yao na dola ambapo sera ya ardhi ya Bw. Ali ilichukuliwa kama hatua ya mpito kati ya ukabaila na ubepari na ilikuwa ni hatua ya lazima endapo Misri ilitaka kujitoa kutoka taifa lenye utegemezi mkubwa wa ardhi na kuwa taifa linalotegemea nguvu za mitaji na masoko.
Bw. Ali aliugeuza uchumi wa kilimo wa Misri kutoka ngazi ya kijungujiko na kuwa uchumi wa mazao ya biashara kwa kuhimiza ulimaji wa pamba sambamba na kilimo cha nafaka. Zaidi ya mifereji 30 ilichimbwa kwa ajili ya kumwagilia mashamba ya taifa.
Kipindi cha mwaka 1840 hadi mwaka 1879 ndicho kilikuwa cha mpito kwa Misri kutoka ukabaila kwenda kwenye hatua za mwanzo za uchumi wa kibepari ambao kwa kiwango kikubwa ulikuwa wa kilimo. Sera ya serikali kumiliki ardhi ilikuwa ni matayarisho ya umilikaji ardhi wa binafsi na mwaka 1858 sheria ilipitishwa ambayo ilianzisha haki ya umilikaji binafsi wa ardhi na ilipofika mwaka 1880 watu kadhaa walikuwa wameshajitwalia maeneo makubwa ya ardhi.
Maendeleo ya kitamaduni
Baadhi ya watu walifikiri kwamba usasishaji wa uchumi, viwanda na siasa lazima uambatane na uigaji wa maadili ya nchi za Magharibi na wengine waliamini katika uanzishwaji wa falsafa halisi ya utamaduni wa kitaifa.
Asasi za elimu zilizoendelea za wakati wa Bw. Ali zilipanuliwa na kupatiwa nguvu za kisheria na sera ya elimu ya taifa ya Bw. Ismail wa mfumo wa elimu wa Misri ulichanganya sifa za kimapokeo na za kisasa, ulikuwa na chuo kikuu cha kimapokeo chenye kiwango cha juu kabisa cha taaluma, asasi nyingi za kisayansi zenye mtaala uliojikita katika mawazo ya kisasa ya kisayansi na kielimu ya jamii na kusababisha kutokea jumuiya ya wasomi nchini Misri ambayo, kwa upande wake, iliwezesha ustawi wa vyombo vya habari na vuguvugu la uchapishaji. Hata hivyo Misri ilikuwa kimbilio la wasomi na waandishi kutoka sehemu mbalimbali za himaya ya Kituruki waliokimbia mateso kutoka utawala wa kifalme.
Mapinduzi ya Urabi mwaka
1881 hadi mwaka 1882
Wakati mabwenyenye wa Misri walipata umashuhuri baada ya mwaka 1840 na watu kama vile Tahtawi na Bw. Mubarak wakaanzisha utamaduni halisi wa kitaifa ambapo jeshi la Misri lilikuwa ndio lenye nguvu zaidi katika Afrika. Jeshi hilo lilikuwa na dhima kubwa katika jitihada za kuleta mapinduzi nchini Misri. Kuibuka kwa kikundi chenye nguvu kiitwacho maarufu kama Kikundi cha Hilwan kilichoongozwa na Urabi kilikuwa ndio mwanzo wa mapinduzi nchini Misri. Kikundi kilishinikiza matakwa yake kwa taifa na kikafanikiwa kuwa chama cha kitaifa mwaka 1879 ambacho kilishirikiana kwa karibu na vikundi vyenye wafuasi wengi nchini na kufungamana na jeshi.
Kutokana na kung’atuliwa kwa nguvu kwa Bw. Ismail mwaka 1879, Chama cha kitaifa kikiungwa mkono na jeshi kilimdhibiti kwa werevu mtawala mpya Bw. Khedive Tawfik na kumfanya kibaraka. Kutokana na hali hiyo, mataifa ya Ulaya yaliamua kulishughulikia suala la Misri kwa uvamizi wa kijeshi na mwaka 1882 kikosi cha manowari cha Waingereza kiliishambulia kwa mabomu Alexandria ambapo uvamizi huo uliangamiza jeshi la Misri na Urabi.
I n g awa ma p i n d u z i y a Mi s r i hayakutekeleza malengo yake ya muda mfupi, yalikuwepo mafanikio kadha wa kadha yaliyotokana na kipindi hicho ikiwa ni pamoja na uhuishaji wa fikra za Kiislamu ambalo lilitumiwa kuhamasisha uungaji mkono wa mapinduzi. Chimbuko la uozo wa kitaifa uliochochea ari ya mapinduzi lilionekana kama ni upotoshaji wa Uislamu.
Hata hivyo mageuzi yoyote ya maana nchini ilibidi yafungamane na misingi ya dini ya Kiislamu wa siasa kali na kuwa na nafasi muhimu sio tu katika uhuishaji wa kisiasa uliopelekea kwenye mapinduzi yaliyoshindwa bali katika masuala ya kijamii ya ufufuaji wa taifa.
Tukio lingine muhimu la kipindi hicho cha historia ya Misri ni kuibuka kwa Bw. Abdallah al-Nadim mwaka 1843 hadi mwaka 1896 aliyefundisha umma misingi na mawazo ya utaifa. Aliweza kuamsha maoni ya umma kupitia magazeti na maandishi yake na alichochea itikadi ya kitaifa ambayo wakati huo ilizidi kuwa kali na kuwa chachu muhimu kwa ufufuaji wa taifa na alikuwa msemaji mkuu wa umma wa wafallahin ambao baadaye aliwatangaza kuwa wadhibiti wa mapinduzi.
Taathira ya Misri
Ufufuaji wa Misri ulikuwa na athari iliyofika mbali, baadhi ya maeneo barani Afrika kama pamoja na Sudan, Ethiopia, Pembe ya Afrika (eneo la Kaskazini Mashariki mwa Afrika) na eneo la Maziwa Makuu katika Afrika ya Kati yalipambana kwa mara ya kwanza na ubepari wa Misri uliobuniwa wakati wa kipindi cha mvuvumko. Mzinduko wa Misri pia ulitishia mpango wa dunia pamoja na mataifa yenye makoloni yaliona suluhisho la tishio hilo ni upunguzaji wa silaha kwa Afrika.
Vita vya mapinduzi ya kisiasa vilianza mwaka 1803 hadi mwaka 1805 ambapo vilimuweka madarakani Bw. Muhammed Ali kuwa kiongozi mkuu wa Misri ambapo pia mwaka 1807 kulitokea vita vya kumuondoa madarakani Bw. Ali vilivyopiganwa kati ya Waingereza na Misri. Waingereza waliivamia Misri kwa vikosi 5,000 vya majeshi katika mji wa Alexandria ambapo Bw. Ali alichukua uamuzi wa kumuua kiongozi wa Mameluke ili kuimarisha ngome yake.
Mwaka 1811 hadi mwaka 1818 baada ya utambuzi wa Ottoman katika nchi ya Misri ambapo kiongozi alikuwa Bw. Ali ilisababisha maelewano makubwa kati ya Misri na Uturuki ambapo walishirikiana kupigana vita na zehebu la Kiislamu la Wahabi ambapo Misri ilishindwa na kuchukua eneo hilo kuwa chini ya dola ya Ottoman.
Mnamo mwaka 1820 hadi mwaka 1839 Bw. Hussein ambaye ni mtoto wa Bw. Ali aliivamia na kuchukua baadhi ya maeneo ya nchi ya Sudani ambayo ni pwani ya bahari ya Sham pamoja na eneo lote la Kusini mwa mto Nile.
Vita vya kwanza vya Dunia
mwaka 1914 hadi mwaka 1918
Ushiriki wa Misri katika vita vya kwanza vya dunia mwaka 1914 hadi mwaka 1918 dola ya Ottoman ilishindwa vita dhidi ya Waingereza na kuwa chini ya utawala wa Waingereza licha ya kuwa ilikuwa huru.
Katika vita kuu vya pili vya dunia vilivyopiganwa mwaka 1939 hadi mwaka 1945 Misri haikushiriki kutokana ilikuwa chini ya utawala wa Waingereza ambao ndio walishiriki kwenye vita hivyo.
Hata hivyo, kufikia mwaka 1948 hadi 1949 kulikuwa na vita kati ya Waarabu na Waisrael ambapo Misri ilichukua eneo la Gaza na ilipofika mwaka 1951 hadi mwaka 1952 nchi ya Misri ilianzisha kampeni ya kuwaondoa Waingereza katika maeneo ya mfereji wa Suez ambapo Januari 25, mwaka 1952 Waingereza walishambulia majeshi ya Misri na kuua watu 50 na kujeruhi watu 100 jambo ambalo lilisababisha kuondoa majeshi yake na badala yake ilipofika mwaka 1956 Jeshi la Waingereza lilishirikiana na Jeshi la Ufaransa pamoja na Jeshi la Israel kushambulia Misri.
Mwaka 1962 hadi mwaka 1970 Misri ilipeleka vikosi vya majeshi kuisaidia nchi ya Yemeni dhidi ya wafuasi wao Saudi Arabia na mwaka 1990 hadi mwaka 1991 Misri ilipeleka vikosi vya kijeshi kujiunga na jeshi la UN-backed ambapo ilisaidia kuikomboa nchi ya Kuwait dhidi ya Irak.
Hadi kufikia mwaka 1990 hadi sasa kiliundwa chama cha Kiislamu maarufu kama Muslim Brotherhood Rebellion ambacho kilikuwa kikifanya kampeni ili kushika utawala nchini hapo.
Kuanzia mwaka 2011 Misri kulikuwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa kuhusiana na kukaa madarakani kwa muda mrefu takriban miaka 30 kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bw. Hosni Mubarak na kufikia mwaka 2012 Bw. Mubarak alitolewa madarakani kwa nguvu ya umma na baadaye alichaguliwa Bw. Mohamed Moris kupitia chama chake cha Islamic Brotherhood ambapo pia jeshi la nchi hiyo limemuondoa madarakani kwa nguvu.
*Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa vyombo vya habari



No comments:

Post a Comment