05 July 2013

KOMBANI ABARIKI MOROGORO KUWA JIJI

 Na Ramadhan Libenanga, Morogoro
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, C e l i n a K o m b a n i amesema sasa umefika wakati mwafaka kwa Manispaa ya Morogoro kuwa jiji baada ya kukidhi vigezo muhimu ikiwemo masuala ya usafi na miundombinu ya barabara kuwa katika kiwango cha lami.
Kombani alisema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Serikali za Mitaa yanayoadhimishwa kitaifa katika Manispaa ya Morogoro ambapo alisema akiwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa aliwahi kukataa maombi ya Manispaa hiyo kuwa jiji kutokana na kushindwa kukidhi vigezo mbalimbali ikiwemo usafi.


Kwa sasa niko tayari kuwa mpiga debe ili kuhakikisha Manispaa hiyo inakuwa jiji, kwanza ina sifa stahili, mwaka huu imeshika nafasi ya tatu kitaifa kwenye suala la usafi, barabara za lami zimeongezeka," alisema Waziri Kombani
Alisema kuwa Manispaa ya Morogoro isitafute mchawi kwa wakati ule kutoruhusiwa kuwa jiji kwani vigezo vingi havikuwa vimetimia lakini kwa sasa kila kitu kinaonekana wazi, hoteli nzuri, kwa wakati wake manispaa ilishika nafasi ya 13 kiusafi.
Alisema pia Manispaa ya Morogoro iko katikati ya kuelekea mikoa mbalimbali na nchi za jirani, hivyo kuwa na hadhi ya jiji kutasaidia kuboresha zaidi utoaji wa huduma mbalimbali. 
K o m b a n i a l i y e k u w a akimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, alisema siku ya Serikali za Mitaa ni muhimu kwa mamlaka za Serikali za Mitaa kama watekelezaji wakuu wa mipango ya maendeleo ya taifa na hutumia siku hiyo kujipima kwa kuangalia walikotoka, walipo na wanakokwenda katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
A l i t u m i a n a f a s i h i y o kuwakumbusha watendaji wa Serikali za Mitaa, kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao, ili wananchi waweze kutambua kuwa Serikali inatambua na kuthamini juhudi zao na kutoa hamasa kwao katika kusimamia vyema miradi hiyo.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni Amani, Uadilifu na uwajibikaji ni nyenzo muhimu kwa mchakato wa katiba mpya.No comments:

Post a Comment