Na Rehema Mohamed
RAIS Jakaya Kikwete, ameiagiza Mamlaka ya Uwekezaji nchini (EPZA),
kuhakikisha wananchi wanaohamishwa katika maeneo ya uwekezaji, kuwatafutia
viwanja na kuwajengea nyumba ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea kati ya
wananchi na wawekezaji.
Alisema tatizo
la wananchi kuvunjiwa maeneo yao na kulipwa fidia ya fedha inachangia mgogoro
mkubwa kwa wananchi, hivyo mamlaka husika iwajengee nyumba na kuwawekea maeneo
ambayo yatawasaidia kujiendeleza kiuchumi.
Rais Kikwete
aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipotembelea Banda la EPZA lililopo kwenye
Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)
.
Awali,
Mkurugenzi wa EPZA, Dkt. Adelhelm Meru, alimhakikishia Rais Kikwete kuwa miradi
ya ujenzi wa viwanda na bandari umeshasainiwa, bado utekelezaji wake.
"Kumekuwa
na utaratibu wa wananchi kuvunjiwa nyumba zao na kulipwa fidia ya fedha; hivyo
kushindwa kujikwamua kiuchumi, utaratibu huu siutaki uendelee kutumika ni vyema
kila mwananchi ajengewe nyumba inayolingana na aliyovunjiwa.
"EAPZ
haina budi kuhakikisha wananchi wanapohamishwa wanapewa viwanja, kujengewa
nyumba na kuangalia kama maeneo wanayopelekwa yana fursa za kibiashara,"
alisema Rais Kikwete.
Aliwashukuru viongozi wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara nchini (TANTRADE); na kuwataka waimarishe ulinzi katika
viwanja hivyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza wakati wowote.
Alisema katika viwanja hayo, kunapaswa
kufungwa kamera za uchunguzi ili kuepusha wi z i u n a o e n d e l e a amb a o
unahatarisha usalama wa bidhaa za wafanyabiashara na wananchi wanaofika kupata
mahitaji.
Pia Rais Kikwete alitembelea Banda la
Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA); na kuitaka mamlaka hiyo ishirikiane na viwanda
ili kuongeza ujuzi wa teknolojia za kisasa ambazo kwenye baadhi ya viwanda
hakuna.
Aliongeza kuwa ni vyema teknolojia
zinazotumiwa na VETA, zikasambazwa kwenye kampuni nyingine ili iweze kuharakisha
maendeleo na kukuza uchumi.
Akizungumzia ujenzi wa nyumba za
kibiashara na viwanda katika eneo la Kurasini, Dkt. Meru alisema kuwa mradi huo
ni wa ubia kati ya Serikali ya China na Tanzania.
Alisema China itatoa fedha sh. bilioni 600
kwa ajili ya ujenzi wakati Tanzania itagharamia ardhi na sh. bilioni 90 kwa
ajili ya ulipaji wa fidia na tayari sh. bilioni 25 zimetengwa kwa ajili ya
fidia awamu ya kwanza.
Aliongeza kuwa, mradi huo ukikamilika
utatoa ajira kwa watu 25,000 ambapo Watanzania hawatatumia fedha nyingi kwenda
kununua bidhaa zao nje ya nchi bali bidhaa zote zitapatikana nchini.
Dkt. Meru alisema eneo la uwekezaji la
Bagamoyo, mradi umetengewa sh. bilioni 50.2 na utaanza wakati wowote.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Zebadiah
Moshi, alisema kwa sasa wamegundua mashine mpya zinazotumia kelele na miale ili
kuzalisha umeme kwa matumizi ya nyumbani ambao hauna gharama kwa watumiaji.
Alisema
kuwa sasa wanaendelea kuwafundisha wanafunzi teknolojia mpya ienee kila sehemu
ili kuondokana na adha ya umeme.
No comments:
Post a Comment