31 July 2013

KESI YA ASKOFU KAKOBE YASHINDWA KUNGURUMA



Na Rachel Balama
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeahirisha kesi ya ubadhirifu inayomkabili Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBC), Zakaria Kakobe hadi Septemba 26, mwaka huu kutokana na Jaji anayesikiliza kesi hiyo kuumwa.

Kesi hiyo iliahirishwa jana na Msajili wa Mahakama Kuu kutokana na Jaji Iman Abood anayesikiliza kesi hiyo kuumwa na kutofika mahakamani.Upande wa walalamikaji unawakilishwa na Wakili Barnabas Luguwa, upande wa utetezi unawakilishwa na  Wakili Miriam Majamba.
Kesi hiyo namba 79/2011 ilifunguliwa Mei 26, mwaka jana na wachungaji watatu wa kanisa hilo; Deuzidelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma.Hata hivyo, baadaye Mc h u n g a j i K a d u m a alilazimika kujitoa kutokana na ushauri wa ndugu na daktari, baada ya kupata ajali na kulazimika kufanyiwa u p a s u a j i mk u bwa wa kichwa.
Baadaye, msimamizi wa kanisa hilo wilayani Liwale, mkoani Lindi, Mchungaji Ignas Innocent aliwasilisha maombi kutaka kujiunga katika kesi hiyo huku akidai ameamua kupigania haki na kwamba, kuna mambo ambayo anataka kuyaweka wazi. 
Wa c h u n g a j i h a o wanamtuhumu Askofu Kakobe licha ya mambo mengine, kwa ubadhirifu wa mali na fedha zaidi ya sh.bilioni 14 na ukiukwaji wa katiba ya kanisa hilo.Awali, Askofu Kakobe kupitia kwa wakili wake, Miriam Majamba aliwawekea p i n g ami z i l a a w a l i walalamikaji hao akidai hawana haki ya kumfungulia kesi, lakini juhudi zake ziligonga mwamba baada ya mahakama kulitupilia mbali.
Katika pingamizi lake hilo, licha ya kudai walalamikaji hawana haki ya kisheria kumfungulia kesi, kwamba si wachungaji wa kanisa hilo kwani walishafukuzwa tangu mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment