25 July 2013

GARI LAUA DAR



. Na Theophan Ng'itu
MTU mmoja amefariki dunia papo hapo mara baada ya kugongwa na gari katika Barabara ya Nyerere eneo la Panasonic Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert 

Kiondo alisema kuwa mtu huyo mwanaume ambaye jina lake halikufahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45-50 aligongwa na gari lenye namba T 288 AZB aina ya Nisani Civilian Min-Bus.
Kiondo alisema kuwa, gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Abraham Said (39) mkazi wa Tandika mji mpya, ambapo alimgonga mtu huyo aliyekuwa akivuka barabara na maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na dereva anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment