31 May 2013




Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) Dar es Salaam jana, wakati akitangaza matokeo mapya ya mtihani wa Kidato cha Nne (CSSEE) uliofanyika Oktoba mwaka jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Profesa Rwekaza Mkandara. (Picha na Prona Mumwi)

2 comments:

  1. Mheshimiwa,DOKTORI,Shukuru ,sasa IWEJE ?Wale mliowaambia kama walifeli na kuwanyima haki zao za msingi kama Raia wa nchi hii ya Udanganyifu na Ulaghai pamoja na WIZI wa Haki za Binadamu mnataka warudi shuleni au mnazidi kuwakebehi tuuuu?
    Mimi naona waambie hao waliofanya njama hizi kwa makusudi basi wabakie kuwa hivyo sisi haturudi tena darasani waachie watoto wao wasome haki itapatikana siku ya HAKIIIIII.

    ReplyDelete
  2. tatizo kubwa katika nchi yetu hii ni udini na ukabila umekithiri katika kila sekta , watoto hupasishwa kutokana na dini zao na kabila lao , hata kama ni vifuu , na haya mambo huanzia pale mtihani wa darasa la saba , ndipo mchujo mkubwa hufanyika kuwaondoa wanafunzi wengi waisilamu , na ikifia kidato cha sita hivyo hivyo , ili kuhakikisha hawaingii vyuoni. Labda mtu anaweza kusema uwezo wao mdogo ndio maana hawapasi, sawa basi hata hizi kazi zisizohitaji akili nyingi shuleni kama za polisi, jeshi, uchumi, sheria, uandishi wa habari bado utaona sehemu ndogo sana waisilamu , jee hamuoni hili ndilo tatizo la matatizo yetu hapa nchini? turekebishe hili kwanza, kuwepo uwiano wa kidini kikabila na rangi na jinsia.

    ReplyDelete