24 May 2013

Wananchi kutoa milioni 156/- kujenga nyumba za walimu


Na Mwandishi Wetu,
Tabora


 WANANCHI wa Kijiji cha Making Kata ya Ichemba Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora wamekubaliana kuchanga shilingi milioni 156 ili ziweze kutumika katika ujenzi wa nyumba 13 za walimu.
Wananchi hao walifikia makubaliano hayo katika mk u t a n o wa h a d h a r a uliofanyika kijijini hapo juzi ambapo pamoja na mambo mengine waliafikiana kuchanga shilingi laki moja kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi, lengo likiwa ni kuondoa kero ya uhaba wa nyumba za walimu katika
shule ya msingi Making.
A k i z u n g u m z a n a waandishi wa habari kijijini hapo, Diwani wa Kata ya Ichemba, John Kadutu alisema kuwa mbali ya ujenzi huo nyumba za walimu, pia wamekubaliana kufanyia ukarabati wa vyumba vya madarasa, vyoo na kukarabati nyumba 5 za walimu.
Alisema kwamba tayari b a a d h i y a wa n a n c h i wameanza kutoa michango yao ambapo kwa upande wake tayari ametoa shilingi laki sita taslimu.
Awali mwalimu mkuu wa shule ya msingi Making, Nelson Mdiu aliwaambia waandishi wa habari kwamba shule yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba mkubwa wa nyumba za kulala walimu.
Alibainisha kuwa shule ya msingi Making ina upungufu wa nyumba 13 za walimu hali inayosababisha walimu wengi waliopangwa kufundisha katika shule hiyo, kukwepa kuripoti kwa wakati.
Mdiu alieleza kwamba shule hiyo yenye wanafunzi wapatao 660, pia inakabiliwa na upungufu mkubwa madawati, madarasa na matundu ya vyoo kwa walimu na wanafunzi.
Mwalimu huyo alisema kuwa mahitaji halisi ya nyumba za walimu ni 18 lakini zilizopo 7 na madawati mahitaji ni 220 yaliyopo ni 126 pekee.

No comments:

Post a Comment