27 May 2013

Viongozi CCM Tabora wazomewa mkutanoni

Na Mwandishi Wetu, Tabora


 BAADHI ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kukumbwa na izomeazomea kutoka kwa wananchi wakati wa mkutano wa hadhara.
Tukio hilo lilitokea kwenye mkutano huo ambao ulifanyika kwenye viwanja vya stendi ya mabasi ya zamani ambapo CCM ilikuwa ikifanya mkutano wake.
Mkutano huo wa hadhara ulifanyika baada ya viongozi wa CHADEMA wakiongozwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, kufanya mkutano eneo hilo na kusema wabunge wa CCM Tabora hawawatendei haki wapiga kura wao.
Alisema viongozi wa CHADEMA watapiga kambi mkoani Tabora kuwatetea wananchi kuhusiana na haki zao.
Hatua hiyo iliwafanya CCM nao kujibu mapigo kwa baadhi ya viongozi wake akiwemo Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Aden Rage, kujibu mapigo.
Dalili za zomeazomea zilianza mapema kwani baadhi ya wananchi walianza
vicheko na kejeli kwa viongozi wa CCM, huku wengine wakisikika wakisema hawataki majigambo, matusi bali wanataka barabara za lami
Tabora-Nzega, Tabora-Urambo na ile ya Itigi-Tabora, huku wengine wakisema Peoples Power’.
Wakati katibu wa CCM Mkoa wa Tabora Idd Ame,akimwaga sera zake,wananchi wachache waliokusanyika kwenye mkutano huo walianza kuzomea kila katibu huyo alipokuwa akitoa kauli kuhusu CHADEMA.
"Ndugu zangu wananchi hebu angalieni mnavyodanganywa, hivi hawa CHADEMA wanajigamba kujenga barabara wakati wao sio watoaji wa fedha na fedha zinatolewa na Serikali ya CCM sio hao CHADEMA, wanafiki waongo," alisema.
Alisema Zitto anaacha jimbo lake Kigoma kwenda Tabora kuwafundisha siasa.
Baada ya katibu huyo kutamka maneno hayo, ndipo wananchi walipoanza kuzomea kwa nguvu na kudai wanataka sera na si matusi, huku wengine wakisema CCM waongo siku zote walikuwa wapi kuja kufanya mikutano hadi CHADEMA waende.
Zomeazomea ilizidi ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora,alipoendelea kutamka kuwa endeleeni na huo ujinga wenu hapa tutaumizana hapa, alizidisha hasira za wananchi huku nao wakijibu mapigo kuwa; “Sawa tu tuumizane tumechoka na ahadi zenu za uongo.”
"Hapa tuko kamili endeleeni kuzomea tu, tutaumizana kweli kweli hapa msifikiri hatuwezi na tutawashtaki viongozi wa CHADEMA Tabora kwa kutufanyia fujo kwenye mkutano wetu,” alisema kada huyo wa CCM.
Wakati katibu huyo akitamka hayo,mjumbe wa NEC, John Mchele, alitoka jukwaani na kwenda kumnong`oneza katibu huyo.

15 comments:

  1. Nyie chadema kwanini muwanyime haki wenzenu kuendesha mkutano wao! Hao sio wananchi ila ni chadema, chama cha zomeazomea. Muandishi wa habari hii kawapamba tu.

    ReplyDelete
  2. Wananchi hao wamechoka kudanganywa, kwani lazima waambiwe na CHADEMA ? yaani mnawafanya watu wajinga hawawezi kutofautisha mchele na pumba. Zile siku za zidumu fikra za sijui nani zimepita !!!!!!!!! hivi hamjaamka usingizi wa chama kimoja ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na zama za chadema M4c za kuuza mbuzi kwenye gunia?

      Delete
  3. Mtazungumza lugha zote mwaka huu na mwakani. M4C imewashika pabaya. Aluta continua. Wananchi Tabora amkeni kutoka usingizi huo wa chama kimoja. Miaka 50 bado tunaahidiana barabara zisizoisha!.

    ReplyDelete
  4. mimi mzanzibibari si riziki mpaka ni-ione ccm imeshindwa vibaya sana katika mikoa yote ya tanganyika na zanzibar....

    ccm hawana ila jazba, chuki, ufisadi, mausi na uharibifu wa mali za umma... wameona hawana njia yakushinda uchaguzi wa 2015øøøsasa wanapita wakidanganya watu, kwakutumia pesa za mfuko wa hifadhi za taifa... mabanda hawana wala hoja hawazijui...

    ReplyDelete
  5. Watanzania ni wavivu wa kufikiria kwakweli,hivi kweli mtu anakuaminisha kana kwamba yeye ni mtakatifu, nasi bila kufikiria kitakacho
    tokea tunashangilia tu!!

    ReplyDelete
  6. hakuna mkweli kwny kusaka ulaji watanzania 2metawaliwa na siasa mbov hao viongoz wanawateka 2 muwape kura wajenge makwao hakuna mzalendo wa nchi kutoka chama chochote walaghai 2ukweli ni kuwa uchumi 2nao lakini 2meukalia hzo sera makelele 2 kwa vyama vyote

    ReplyDelete
    Replies
    1. "Heee et viongozi wanatudanganya ili tuwape kura wajenge makwao"Mbona unaongea kama mwenda wazimu?wewe huoni mahali nchi ilipofikia wala huoni nchi yetu inaelekea wapi, nchi imejaa dhuluma kila kona watu wanajitoa mhanga kutetea halafu we unabeza? Ok fyne onyesha wewe uzalendo wako ili wote tutoke hapa tulipo. Kama umekata tamaa ya maisha ni wewe sio sisi. Jamani tuwapuuuze watzu wa aina hii inawezekana hata familia ao wamezitelekeza kwani hawana uelewa wa kufikiria na kutatua matatizo wanategemea kupewa kanga zenye picha a watu fulani, tshirts n.k

      Delete
  7. Hapana bwana chadema itawapa kazi, itawajengea barabara za lami mpaka mlangoni, itawasomesha bureeeee, itawaruhusu wachimbe madini yao wenyewe wauzeee wapate fedha!. Nchi nzu ina rasilimal za kutosha. pipozi pawaaaa!

    ReplyDelete
  8. sisiem kuweni na busara za kuwasoma wananchi, sio kila jambo waonekane wametumwa na chadema. tutuashindwa kujijenga wenyewe nw kuwapa shavu wapinzani. mfano kuna haja gani ya kutosikiliza hoja za mbatia? mwigulu kuwa makini maana kile ukiingia singida lazima kuwe na fujo kila siku kampeni za kata ya iseke zinafanyika na hakuna fujo lakini jana ulipoingia ukashauri ccm wabebe mapanga na virungu.

    ReplyDelete
  9. Kumbe Mwigulu ana fujo. Kumbe kila mtu anachukia fujo. Kama unachukia fujo nanwewe usifanye fujo!

    ReplyDelete
  10. Hawa ccm wako kama vidama vya kondoo,Hawawezi kufikiri nini kilicho na ukweli na ni nini ni uongo . Hivi miaka hamsini ya ccm bado mnadanganyika tu ?hamuwezi kujua kama hawa ni wezi wahuni na matapeli no1, nchini ni wao. Eti pesa ziko Serikalini iko wapi hiyo Serikali ?Wakija tena waambieni siku zao ZINAHESABIKAA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ziikisha za hayo yataingia majizi mengine. Kama wewe utabahatika itakua vyema. Ningependa nikufahamu nipendekeze upewe utakatifu!!!!!!! Serikali lazima iwepo hata kama ukilia itakuawapo. Hakuna dola nzuri yoyote duniani. Bora yetu

      Delete
    2. NYANI WANAFUKUZA NGEDERE ILI WAO NDO WATUNZE SHAMBA LA MAHINDI

      Delete
  11. Jamani watanzania tuepuke hao wahuni wa chadema kama ukoma. Ni wadanganyifu wa kutupwa! Hawasemi huko nyuma hali ilikuaje. Hakuna hata kijiji kilichokua na huduma ya umeme. Mikoa mingi ili remote, haifikiki. Watu walikua hawawezi kununua hata dawa ya meno. Sasa hivi angalau kuna kamiddle class kanakoingilika kirahisi. Shida zetu ni kubwa sana na umasikini unatisha. Lakini turuhusu hawa wahuni waharibu na kunyang'anya hat hiki kidogo? Ndivyo wanavyotamba mitaani!Hata kama umejinyima ukajenga kibanda chako ukapaka rangi vizuri eti wanakuita fisadi

    ReplyDelete