02 December 2010

Mrema wa TANROADS ang'olewa rasmi

*Ni uamuzi wa Waziri Dkt. John Magufuli
*Akabidhiwa barua na Katibu Mkuu Chambo


Na John Daniel

HATIMAYE kasi na viwango katika utendaji kazi wa Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli umeanza kuonekana wazi baada ya kumwondoa rasmi aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Bw. Ephraem Mrema.Bw. Mrema ambaye
amekuwa akipigiwa kelele kwa kukumbwa na tuhuma mbalimbali za kiutendaji ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 300 huku akikataa kuonana na waandishi wa habari, aliondolewa rasmi Ofisini kwake jana.

Vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya serikali vililieleza Majira kuwa Bw. Mrema aliondolewa ofisini kwake saa 9.30 mchana na timu ya maofisa watano kutoka Wizara ya Ujenzi.

"Nakuhakikishia leo (jana) saa 9.30 ulikuwa mwisho wa Mrema Ofisini, walikwenda maofisa watano kutoka Wizarani wakiongozwa na Katibu Mkuu Chambo (Omar) na kumkabidhi barua yake ya kuondoka.

Walimtaka akabidhi Ofisi kwa Mkurugenzi wa Barabara Vijini, Bw. Patric Mfugale, ila nadhani taarifa rasmi itatolewa kesho (leo)," kilisema chanzo chetu.

Vyanzo vyetu ndani ya serikli vieleza kuwa tangu siku ya Jumapili wiki hii, Bw. Mrema alikuwa akihitaji kukutana kufanya mazungumzo na Dkt. Magufuli lakini waziri huyo hakuwa tayari kufanya hivyo.

Waziri Magufuli alikataa kuonana na Bw. Mrema kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuhitaji kuangalia nyaraka mbalimbali zinazohusu utendaji na majibu yake.

Juzi (Jumanne) Waziri Magufuli alidaiwa kutoa maamuzi yake kuhusu Bw. Mrema na kuwasilisha rasmi mapendekezo yake kwa Rais Kikwete jana kabla ya kuondolewa kwa mtendaji huyo.

Katika mapendekezo yake, Dkt. Magufuli alirejea tuhuma mbalimbali za Bw. Mrema na hali halisi ndani ya TANROADS pamoja na matarajio yake ya kiutendaji ndani ya wizara hiyo.

Ilielezwa kwamba baada ya muda wa Bw. Mrema kumalizika Novemba 27, mwaka huu kulikuwa na jitihada kubwa kuhakikisha anaendelea na nafasi hiyo, lakini kuteuliwa kwa Dkt. Magufuli kunatajwa kuwa ni kikwazo kwa juhudi hizo.

"Magufuli ni kiboko, hana cha tajiri wala maskini, akiona uovu anashughulikia, huyu mkubwa alikuwa tishio lakini kuondoka kwake ni hatua kubwa ya utekelezaji wa ahadi za Kikwete kuhusu barabara," kilisema chanzo chetu.Baadhi ya tuhuma za Bw. Mrema ni pamoja na kusababisha mgongano kati ya Bodi ya Tanroads, na wakala hiyo pamoja na wizara yenyewe.

Pia Bw. Mrema alidaiwa kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji wa TANROADS waliokuwa hawako na nia moja na kuitisha kikao cha wafanyakazi Oktoba 30, mwaka huu kutangaza maamuzi hayo.

Waliokumbwa na sakata hilo walikuwa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara, Bw. Thomas Mosso, Mkurugenzi wa Mipango, Bw. Jason Rwiza, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dodoma, Bw. Gerson Lwenge.

Wengine ni aliyekuwa Meneja Mkoa wa Morogoro, Bw. Charles Madinda, Meneja Mkoa wa Ruvuma, Bw. Abraham Kissimbo na Mhandisi Makao Makuu TANROADS, Bw. William Shilla.

Uchunguzi wa Majira ulibaini kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliwahi kuchunguza mradi wa barabara ya Bagamoyo-Msata ambayo TANROADS ilidaiwa kusaini mkataba kiaina na kampuni moja ya Korea.
Katika sakata hilo serikali ilisitisha na kupata hasara ya mabilioni ya fedha huku zabuni mpya ikitangazwa kwa mizengwe kupotosha ukweli.

Bw. Mrema amekuwa akiandamwa na mivutano mikubwa kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu. Mwaka 2008 alidaiwa kushtakiwa na PPRA ikitaka wizara kumchukulia hatua  kwa kukiuka sheria, taratibu na kauni za manunuzi, jambo ambalo halikufanyika. Hata hivyo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake hivyo kuzua hofu kuwa alikuwa akilindwa na vigogo.
Tuhuma nyingine iliyodaiwa dhidi ya Mrema ni uongozi wake kuukosesha serikali sh. bilioni 12 kutoka Benki ya Dunia (WB) zilizotolewa kujenga jengo la TANROADS.

Katika tuhuma hiyo ilidaiwa kuwa Bw. Mrema alikataa kujenga Ofisi za TANROADS eneo la Mabibo kwa madai kuwa anataka katikati ya Jiji la Dar es Salaam, hivyo kusababisha WB kuondoa fedha zao huku serikali ikiwa imelipa mshauri mwelekezi sh. bilioni tatu za kodi za Watanzania.

Juhudi za Majira kuwasiliana na Bw. Mrema ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila muda mrefu bila kupokewa.

34 comments:

  1. TUNAKUTAKIA KILLA LA KHERI DR, MAGUFULI UZIDI KUWA NA UFANISI NA WEPESI WA KAZI ZAKO, UMEFANYA BUSARA SANA KUTOKUTANA NAE MAANA UNGEKUTANA NAE TUU INGEKUWA KOSA!!MAANA HUYO JAMAA ANA KIZIZI UNGEISHIA KUMUONYA TU,HONGERA
    SANA BIG UP,TUNATARAJIA UOZO MWINGI NA UZEMBE UTAUONDOA,NA KAZI IFANYIKE USITUMIE MUDA MWINGI OFISINI MAANA KUNA BARABARA YA KILWA NI HASARA KUBWA KWA SERIKALI,NJIA NYINGI MIKOANI HAZIKAMILIKI NA HATA ZILIZOKAMILIKA KIWANGO NI HALI CHINI KABISA

    ReplyDelete
  2. Hongera Dr.Magufuli

    Unadhihirisha kuwa unaweza pale unapopewa mamlaka ya kufanya kazi

    ReplyDelete
  3. Ni baada ya uteuzi wako Dkt. Maugufuli nilipoijiwa na imani kuwa sasa watanzania tutarajie mambo mazuri toka kwako, huo ni mwanzo Dkt. mengi yapo mbele yako, kila la kheri na watanzania wote tuko pamoja na wewe.

    ReplyDelete
  4. Asante sana Rais jk kwa kurudisha Dr magufuli kwenye wizara yake sasa hata sisi watu mwanza vijini tutapata barabara safi hata kama si kiwango cha lami maana.Na huyo bwana Mrema ni fisadi mkubwa tena afikishwe kwenye vyombo vya sheria.Asante sana Dr Mugufuli.moses

    ReplyDelete
  5. viva Dakta,ww ni pombe kali na umedhihirisha hilo

    ReplyDelete
  6. SIJUI KIKWETE KWA NINI ALIKUTOA WIZARA HIYO NYETI, MAMBO YA KI-CCM WAYAWEKE KANDO NCHI KWANZA VINGINEVYO CCM TUTAZIDI KUPOTEZA MAJIMBO 2015. CHAPA KAZI MAGUFULI.

    ReplyDelete
  7. Naona kati watendaji wazuri waliobakia ccm yupo huyo pombe Magufuli , ila asifanye kama gia tu ya kuanzia aanzie kila kitengo na awabadilishe wote na kuwaweka watu wenye sifa za mambo ya Ujenzi na uzoefu wa miundo mbinu,na pia hii isiwe kwa wizara ya Ujenzi tu, iwe ni kila Wizara maana kuna Uozo uliopitiliza serikalini kuanzaia wakurugenzi hadi watawala wa ngazi ya chini kwani serikalini wamefanya sehemu ya nyumba zao na hata kazi wanatoa kindugu hata kama mtu hana sifa hiyo anapewa na akishaingia utakuta semina inaendeshwa nyingi ktk wizara ambayo inawalipa night na marupurupu mengi inayopelekea serikali hasara kubwa, ninaiomba Serikali ya kikwete kama kweli wameazimia kuleta maendeleo, lazima wakubali kuondoa uozo huo wote, na kulijenga tena Taifa lenye Heshima na lililo barikiwa, kwa kutoa na kugawa bajeti ya wizara husika na kuhakikisha kuwa kila hela au senti inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa maana nilikuwa napeleleza kwanini serikali watumishi wake wanalipwa hela si kwa wakati na huku serikali inawajua kuwa ni waajiriwa na ndio chanzo cha madai ya watumishi wa chini kama waalimu, manesi na madokta yanakuwa mengi, nilipata kujua kwa kufuatlila kuwa kwa watumishi hao wakubwa kama wakuregenzi, masekretary, huwa wanapanga bajeti lakini kuna watu wasio waminifu hasa wa Hazina wanachelewesha na hata mida nyingine wanapoteza mafali ya watu kisa na mkasa hakuna anayefuatilia kisa hujilikani au hujaonga mtu wa kukufuatilia madai yako, Je kwa style hii mtu unafanya kazi hulipwi na watu wengine wanajilipa ma over night, on transit payment,pdm ,kwanini hivyo nilipouliza pia kama wizara inadaiwa kama wizara ya elimu na waalimu kwanini basi wasiahangaike kuwallipa watu haki zao kuliko kuwatesa huku wakiendesha semina ya mabilioni kwa watu wakubwa kama masekretari na wakurugenzi na wa maofisa wa elimu huku wakilipa maover night na kulipiwa trip ya mabilioni na kula na kulala mahoteli makubwa ya malaki kwa siku? ni huzuni sana na kweli naomba serikali iwajibike kwa hilo kila wizara.

    ReplyDelete
  8. Kuna vitu Vingi vya aibu yanayoendela katika wizara mabalimbali, ila hii iwe changamoto kwa mawaziri na manaibu waziri na serikali ya jk kwa Ujumla, Pia kilio hiki naelekeza kwa wawkilishi wetu tuliowachagua Wabunge wa chama tawala na wale wa vyama vilivyochaguliwa kuwa na wabunge walishinikize serikali nakupitia Mawaziri waweze kuleta mabadiliko halisi na ya kweli na kuleta ukaribu Serikali na wananchi kwa kuwa ,mfano hata raia wa kawaida ukiwa na mahitaji unataka usaidiwe na serikali au wizara ni shida kwani hata kumuona katibu au mkubwa wa kitengo husika inakuwa shida kwani hao masekretari wa Ofisi watakusumbua na kukukatisha tamaa, mara leo bosi yuko bise busy mara yuko kwneye kikao mara kasafiri, wengine mpaka uwahonge ndio upewe kuonana nao, na hii ni serikali inawatumikia wananchi au? wananchi ndio wanatumikia kwa kuwanunua ili wasaidiwe, hii ni shida ya kila wizara,kuanzia wizara ya mambo ya ndani, immagration, Elimu, Afya, mpaka wizara nyingine zote hata kwenye mabo ya sheria. Tanzania tubadilike kila mtu awe na uchungu na nchi yake na uzalendo na lengo la kuindeleza nchi hii, pia nilipata kusoma habari katika gazeti fulani kuhusu wabunge wa ccm walioshindwa mwanza alivyoifanya ofisi aliyokuwa anaitumia kuondoka na vitasa na dhamani alizodai ameweka mwenyewe kwa hela yake, Haa!!!! ni aibu na ni ajabu kwanza mtu kama huyo hana Upendo na watu , Hana Utu , Hana uzalendo na nchi kwani ofisi ile si ya chama ni ya serikali,na kama raia alipaswa kuiendeleza nchi ikiwemo na kubadilisha baadhi ya vitu hata kama ni ya jumuia aua public,iwe ni sehemu ya mchango wake wa kukaalia kiti hicho cha ubunge kwa miaka yote, Je kwa mtu kama huyo aliyekuwa waziri anaonyesha hivyo na hao wengine watafanya nini? na je ttutalijenga Taifa kwa njia hiyo, ndio uozo niliongelea kwenye wizara,maana serikalini wamefanya sehemu ya kujichumia chao na kuondoka. mmmmmm Jk naomba uanaglie Taifa kwa jicho la Tofauti

    ReplyDelete
  9. Ng'oa baba, ng'oa visiki vyote, tupo nyuma yako

    ReplyDelete
  10. KUTOKANA na utafiti wa kisayansi kuonesha kuwa kutofanya tohara kwa wanaume ni moja ya sababu zinazochangia maambukizi ya Ukimwi, wanaume katika mikoa saba nchini wanatarajiwa kufanyiwa tohara kuanzia mwakani kwa sababu inayo idadi kubwa ya wanaume wasiotahiriwa.
    Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itaanza operesheni maalumu kwa kushirikiana na wadau wengine yakiwemo mashirika ya misaada kutoka Marekani, kufanya tohara kwa wanaume hao katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Kagera, Tabora, Shinyanga na Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

    SASA HII MIDUME YENYE GOVI MTAIKAMATA VIPI ILI KUWATAHIRI? AU MNASEMA TU?

    ReplyDelete
  11. Hii habari ya ukimwi na magovi imekujaje tena hapa

    ReplyDelete
  12. HATIMAYE!!!!!!!!!
    Hongera sana Dr Magufuli kwa kumundoa huyo fisadi, Dicteta Mrema. Endelea hivyo na Mungu mwenyewe atakulipa.Mrema ametia sana taifa hasara, amechezea kodi zetu walala hoi, APELEKWE MAHAKAMANI TAFADHALI.ASANTENI SANA VYOMBO VYA HABARI KWA KUTUELIMISHA KUHUSU HUYU MTU, TUNGEJUAJE YOTE HAYA? MUNGU AWABARIKI KWA KAZI NZURI MNAYOIFANYA MEDIA.

    ReplyDelete
  13. SAFI MNOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!11111

    ReplyDelete
  14. Dawa ya ufisadi ndiyo hii tu, kutengana nao ili wakauendeshe katika miradi yao binafsi kuliko kuendelea kuvutana nao eti kutafuta vielezo. watolewa tu ili nchi isonge mbele. tunahitaji watendaji wa serikali na si wakuzaji wa miradi yao. Hongera Dr.

    ReplyDelete
  15. Mh Dr Makofuli na Dr Mwakiembe mlisahau kuandika barua nyingine ya kumpa huyu HOSEA nae anatusumbua sana hapa. Yeye ndio kawa jengea mila na desturi za ufisadi. Au kwa vile ni mchaga. Mmeshaanza na huyo sasa tunataka kuona majana yanapuputika kwa watu wote wanaolalamikiwa na wananchi isijeikawa ni nguvu za soda. Hayo ndio maamuzi magumu.

    ReplyDelete
  16. Dr Magufuli, Wewe ni Mwanamume bwn, Umewezaji kumuondoa huyoooooo!Wengine walimfugafuga sana, sijui walikuwa wanakula nae au vipi, Wangemuondoa mapema taifa lisingeingia hasara kubwa kiasi hicho, Amezorotesha sana utendaji wa wakala, ameshusha sana ari ya wafanyakazi wa wakala,Amewagawa sana wafanyakazi kwamba kuna na makundi, wanaopendwa nae na Wasiopendwa, HALI YA WAKALA ILIKUWA MBAYA SANA, HONGERA MAGUFULI KWA KUINUSURU HALI HII.

    ReplyDelete
  17. Shina la ufisadi Tanroads limeng'olewa Hongera Mheshimiwa Magufuli

    ReplyDelete
  18. NI NANI ASIYE FISADI KWA NAFASI YAKE, NA AWE WA KWANZA KUMNYOSHEA KIDOLE MREMA WA TANROADS!MUNGU AKIULIZA ALIYEMSAFI NI YUPI ATAKAYESALIMIKA?

    ReplyDelete
  19. Hakika Mh. MAGUFULI ni mkombozi wetu hasa sisi tulio watu wa kipato cha chini;kwani hasa huku mijini watu wenye pesa huchukua sehemu zenye zlizotengwa maalumu kwa ajili ya jamii:pia kwa mfano hapa Moshi sehemu ya uwanja mdogo wa ndege wa mjini hapa uliuzwaga sasa tunaomba sana sehemu ile irudishwe kama ramani inavyosoma.Kwani waliochora ramani hiyo hawakuwa wajinga na hao waliojigawia ni werevu.Tumia haki kwa hilo na Mungu atakusaidia.Kazi njema.

    ReplyDelete
  20. Natumaini kwa uhakika kabisa wabunge mmeapa kwa kushika Vitabu Vitakatifu-Biblia na Msaafu.Sasa kama kweli mliapa tendeni haki kwa wote bila upendeleo maana yake mlimweka Mungu kuwa Kinga yenu,mwogopeni Mungu na mtende kazi kama Mh. MAGUFULI na Mawaziri wote wawe hivyo bila kumwangalia mjomba,shanagazi ama binamu.Hongera Magufuli kwa kazi saaaaaaafi.
    CHARLES KIJUU

    ReplyDelete
  21. Safi sana Dr. Pombe. Hata sisi wa Kigoma tuna imani kuwa ndani ya muda mfupi tutakuwana uhakika wa kutoka dar mpaka kigoma kwa tax kama ulivyo ahidi wakazi wa mwanza na yalitimia.

    ReplyDelete
  22. Dr.P. ukimaliza kusafisha hiyo wizara,Tungeomba Mh.Raisi akuhamishie wizara ya Mambo ya ndani huko kuna hitaji mtu kama wewe.

    ReplyDelete
  23. Wewe ni mwanaume ambaye kiwango chake hakipimiki. Akili, busara na hekima unayo,
    woga wa kijinga na wasi wasi kwenye kazi huna. Fisadi kun'golewa na mzizi wake??? Kweli Dr. wewe ni kiboko ya uchafu. Wapatikane basi wengine kama wanne hivi huko kwenye mawizara. Anyway, tunamsubiri Anna Tiba, naye anaonekana haogopi kofi la mtu.... Hongera Dr.

    ReplyDelete
  24. hongera sana mzee wa kazi(DR Magufuli) umembakiza KAKOKO RM wa arusha. maana nae ni fisadi wa kutupwa

    ReplyDelete
  25. Masumbuko Shaban MakulaDecember 2, 2010 at 7:27 PM

    Maisha bora kwa kila mtanzania yanakuja kwa kazi nzuri ya kiongozi mwaadilifu, mzalendo na mtenda haki.Dr. John Pombe Magufuli ni kielelezo cha kiongozi mzuri kwa kujali maslahi ya taifa zima.Viongozi wengine waige mfano wa Dr. Magufuli. Kigogo Mr. Mrema alikuwa ameshindikana ndani ya TANROAD, leo hii kang`ooka kwa Maslahi ya taifa

    ReplyDelete
  26. Mnanikumbusha ile enzi ya 'Mikingamo sautiiii ya wasemakweli daima, ntasema tu...nitasema kweli daima fitina kwangu mwikooooo!! Raha sana. Mwingine nani AFUATE?? HOSEA!!

    ReplyDelete
  27. Poa tu mbele kwa mbele Pombe Magufuli uma kote kote mpaka kieleweke na safari nyeupe kwako 2015

    ReplyDelete
  28. Salute kuu kwako Mh. Dkt Pombe na Dkt Harrison mambo yenu ni moto wa kuotea mbali. Mh. rais hakukosea kuwapa hii nafasi nasi tunataka barabara ya Tabora, Sikonge mpaka Mbeya ipitike nyakati zote kukuza uchumi wa mkoa wetu uliosahaulika tangu Uhuru, kama alivyoahidi mkuu wa kaya, nakupongeza pia JK kwa kuibua vifaa adhimu kwa mustakabali wa taifa letu.
    Bhelum

    ReplyDelete
  29. AIBU TUPU KWA SERIKALI YA KIKWETE..KWANI SIKU ZOTE HAKUJUA KWAMBA E.MREMA HAFAI NA AMEINGIZIA SERIKALI HASARA KUBWA? KIKWETE ALIJUA ILA NA ULIKUWA MPANGO MAHUSUSI WA KUPORA PESA ZA KAMPENI,NDIO MAANA KIKWETE ALISHINDWA KUMWONDOA.NI AIBU SANA,RAIS ANASHINDWA KUMWONDOA EXVANGANT PERSON LIKE MREMA HADI ANAKUJA KUONDOLEWA NA MAGUFURI ALIYEINGIA JANA..THAT'S SHAME.

    ReplyDelete
  30. Rais wetu hakomi kutiwa aibu kama huyo mama sophia simba wanasiri gani na kikwete.Ni mama asiye kuwa adabu hata bado tena anpewa uwaziri sasa Jk unataka tena akuabishe?msukuma

    ReplyDelete
  31. MUNGU akulinde Dr. Magufuli; kazi unayofanya ni njema sana kwa taifa letu. Laiti kama viongozi wetu wote wangekuwa na msimamo wako thabiti wa kiutendaji, nchi yetu ingekuwa imeendelea sana, na maisha ya watanzania yangekuwa bora mara dufu. Lakini viongozi wetu wengi wametawaliwa na ubinafsi, wengine si wabinafsi lakini waoga wa kufanya maamuzi magumu. Ni kweli mwanadamu si mkamilifu, lakini wapo waaminifu, naamini Dr. Magufuli ni mmoja wao, na anapokengeuka hujirekebisha mara moja, hang'ang'anii upotovu.

    ReplyDelete
  32. hongera sana, najua mara baada ya jina lako kutangazwa kushika wizara hiyo bw mrema alijua fika hatima yake imefika. mhe waziri tunakuuomba uiangalie upya barbara ya kilwa ikibidi uende mbaali zaidi kuwaadabisha waliohusika na ujenzi huo kwa maana ya wale walioko chini yako.

    ReplyDelete
  33. Tuhuma zinazomkabili huyo Dicteta Mrema zisinyamaziwe. Hizo Bilions za walipakodi maskini zichunguzwe na ijulikane ni akina nani waliokuwa wakimpa huyo Mrema kiburi cha kuiongoza TANROAD kama mali yake. Hii ni aibu kubwa sana kwa taifa. Kila siku tunasikia flani mwizi flani mwizi inakuwa kama nchi haina wenyewe. Ningeomba iundwe tume ya kuchunguza hizo tuhuma za mrema naamini kuna mengi yatagundulika na kuwekwa bayana.
    Ni hayo kwa leo.
    Joseph kisyoky
    4545 Conneticut Ave
    Apt 918 Washington DC,USA

    ReplyDelete
  34. broo mapadlock ni noma tunakusubiri mizani kibaha

    ReplyDelete