30 November 2010

Siri ya kuachwa Chiligati yatajwa.

*Makamba upepo si mzuri ndani ya CCM.
*Kamati kuu kukutana D'Salaam kesho.
*Msekwa naye atoboa, ajenda ni moja.
 


Na John Daniel.

HATIMAYE siri ya kuachwa kwa aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Baraza jipya la
Mawaziri, Bw. John Chiligati, imefichuka.

Siri hiyo imetajwa kuwa ni kuandaliwa kwa Bw. Chiligati kurithi mikoba wa Katibu Mkuu wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Yusuf Makamba, anayetakiwa kupangiwa kazi maalum au kupumzika kabisa siasa.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya CCM vimeeleza kuwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kupitia vikao husika vya chama hicho ana mpango kumpa nafasi hiyo, Bw. Chiligati kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni uwezo wa kuhimili kuweka sawa makundi yote na ushirikiano mzuri ndani ya chama.

Sababu nyingine iliyotajwa ni uzoefu wake ndani ya chama hicho pamoja na kushughulikia nyufa zilizotokana na Uchaguzi Mkuu ambapo ushindi wa CCM ulipungua ikilinganishwa na mwaka 2005.

"Mmekuwa mkiandika sana kuondolewa kwa Mhe. Makamba katika nafasi yake lakini safari hii habari hizo ni za kweli, chama kinahitaji mabadiliko ya Katibu Mkuu kama mtendaji mkuu.

Anayeandaliwa kuchukua nafasi yake muda wowote kuanzia sasa ni Mhe. Chiligati, anaonekana kuwa ni mzuri na mtu mwenye msimamo wa kati, anayemudu makundi yote, mwenye uhusiano mzuri na waandishi wa habari, anaweza kukisaidia chama kundoa nyufa za Uchaguzi Mkuu,"kilisema chanzo chetu.

Ilielezwa kwamba tayari Rais Kikwete amejiandaa kuwasilisha hoja hiyo katika kikao maalum cha Kamati Kuu (CC) kinachotarajiwa kufanyika kesho mjini Dar es Salaam kama ajenda ya mengineyo kutoka kwa Mwenyekiti.

Vyanzo vyetu vilieleza kuwa Rais Kikwete ameamua kubaki na ajenda hiyo mkononi mwake na kuhusisha wazee wachache ndani ya chama hicho bila kutaja sababu za kufanya hivyo.

Hata hivyo duru za kisiasa zimeeleza kuwa huenda uamuzi huo unatokana na kutaka kukwepa makundi na mgongano wa kimaslahi kuhusu suala hilo.

Majira ilipomtafuta Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bw. Pius Msekwa ili kupata ufafanuzi wa suala hilo hakuwa tayari kuzungumzia taarifa hizo kwa kile alichoeleza kuwa hawezi kuzungumza kitu ambacho hakijaamuliwa na vikao rasmi vya chama hicho.

Alisema CCM si mali ya mtu mmoja hivyo maamuzi ya kumwondoa Katibu Mkuu na masuala yote yanayohusu chama hicho huamuliwa na kikao na si mtu mmoja huku akimtaka mwandishi wa habari hizi kumweleza kwanza alikopata taarifa hizo za kuenguliwa kwa Bw. Makamba.

Hata hivyo alipoulizwa kama ana taarifa za kikao cha CC cha kesho na ajenda zake, alikiri kwamba ana taarifa na kikao hicho huku akieleza kuwa kinatarajiwa kuwa na ajenda moja tu ya kupitisha majina ya wagombea umeya katika manispaa na majiji.

"Usipende kuandika habari za kufikirika, hayo ni maneno ya mitaani, hayana ukweli wowote wala hao waliokwambia hawawezi kuthibitisha, siwezi kuzungumzia jambo ambalo halijatoka kwenye kikao, maadili ya CCM ni kwamba taarifa inayotolewa ni ile iliyoamuliwa na kikao.

"Ni kweli kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu tarehe moja Desemba hapa Dar es Saalam, tayari tumepewa ajenda ya Kamati Kuu,  ni moja tu ya kupitisha majina ya wagombea umeya, kama ipo nyingine mimi sijui na si kweli, ni maneno ya uwongo tu,"alisisitiza Bw. Msekwa.

Alisema Katibu Mkuu mwenyewe, Bw. Makamba ndiye aliyewapa ajenda hiyo moja ya CC na kusisitiza kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu hakuna kikao kilichoketi kujadili suala lolote kuhusu mabadiliko ya uongozi wa chama hicho.

Licha ya tetesi za kuenguliwa Bw. Makamba duru za kisiasa zilieleza kuwa Idara ya Usalama na Maadili pamoja na Kitengo cha Propaganda cha chama hicho, pia vinatarajiwa kukumbwa na mabadiliko makubwa kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mbali ya Bw. Chiligati kutajwa kurithi mikoba ya Bw. Makamba pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana Dkt. Emmanuel Nchimbi, anatajwatajwa katika nafasi hiyo.

Juhudi za kumpata Bw. Makamba ili kuzungumzia tetesi hizo  zilishindikana kutokana kile kilichoelezwa kuwa amefiwa na yuko mkoani Tanga. Hata simu zake zote za mkononi hazikuweza kupatikana hadi tunakwenda mitamboni.

Kuondolewa kwa Bw. Makamba katika nafasi hiyo imekuwa gumzo la muda mrefu sasa, kwa mara ya mwisho ilidaiwa kuwa Katibu huyo alimsihi Rais Kikwete kumwacha ili akamilishe awamu ya kwanza ya  ya miaka mitano kwa sababu mbalimbali.

25 comments:

  1. Itakuwa bora akiondolewa! kazidi jeuri na majibu ya ujuba! wapo tele wenye busara ndani ya CCM, awekwe mwengine mwenye kuimudu hiyo nafasi!

    ReplyDelete
  2. MWACHE MZEE KAJIZEEKEA ! HAWEZI KWENDA NA KASI YA DUNIA YA SASA ! WAZEE WENGI WAPO KWA AJIRA TU WAMECHOKA AKILI TUWASAMEHE BURE

    ReplyDelete
  3. MZEE MAKAMBA NI MUDA WAKE WA KUSTAAFU NI BORA AKAPUMZIKE, NA RAISI ASIJE KUMPA JUKUMU KUBWA TENA MAANA ATAWEZA KUHARIBIKIWA ZAIDI,MAKAMBA ALIKUWA NA UAMUZI WA HARAKA NA USIO NA UPENUZI KUNA BAADHI YA MAAMUZI YAKE NI FITINA!! NA PIA ALIWEKA MATABAKA NDANI YA CCM ALIZIDISHA MPASUKO NA KUWEKA MAKUNDI KILA LA KHERI MGOSINGWA

    ReplyDelete
  4. BORA MAKAMBA AONDOKE AMEFANYA CCM MALI YAKE!YEYE NDIYO AMESABABISHA CCM KUPOTEZA MAJIMBO NA WALA SIO SPIKA MTAAFU SAMUEL SITA,AMEWAFANYIA GHILIBA WASHINDI WA KURA ZA MAONI AKAWAWEKA WALIOSHINDWA NA MATOKEO NDIYO HAYO! KATIBU MKUU WA CCM NI LAZIMA UWE MVUMILIVU,MWENYE STAHA,HEKIMA,BUSARA....MAKAMBA AMEKOSA VYOTE HIVYO!

    ReplyDelete
  5. ufa mwingi ndani ya ccm umesababishwa na makamba, majibu mengi na kata zilizopotea kwenda Chadema ni matokeo ya matabaka , na uchomoaji wa washindi halali na kuwaea wakushindwa aliofanya makamba. heri apumzike asiiharibu serikali ya kikwete, maana akitoka huyo hata muafaka wa mazungumzo mazuri kati ya Chadema na ccm kikwete anaweza kuufanikisha lakini angekuwepo Nomaaa, maana hajui wapi pa kufanya nini, na nini kifanyike wapi.
    dhana yake kubwa ni kudhani nchi hii ni ya vyama vya mpira ambapo unaweza kununua mchezaji toka simba akachezea miaka mitatu na mwaka mwingine anapigwa na chini na kwenda timu nyingine. viongozi na wanachama kwake ni wazuri pale tu akifanya jambo la kumsikiliza anachotaka; ukibisha tuu mwakani hugombei wala hupendekezwi ataweka mtu mwingine hata kama hajiwezi.
    nenda zako makamba kapumzike uwachanganye wazee wenzio, utuachie vijana. umetuvuruga kiasi cha kutosha sasa tunataka mabadiliko.

    ReplyDelete
  6. Jamani mnamuonea mzee wetu bure. Katika vikao vyote vya chama, maamzi hufanywa kwa pamoja. Hayafanywi na mtu mmoja kama mnavyojaribu kuonesha.

    Kama kuna wa kulaumiwa basi ni wote na hasa mwenyekiti kama alishindwa kueleza njia salama. Mzee asifanywe kafara.

    ReplyDelete
  7. Inshaalah akapumzike CCM ilikuwa mali yake.

    ReplyDelete
  8. Kwani katika CCM ni Makamba tu mwenye matatizo? Hata JK mwenyewe ana matatizo ya kuwakumbatia mafisadi na kuzikalia tuhuma za ufisadi kwa miaka mitano iliyopita. Kwa hiyo hata akiondoka Makamba ni sawa na nyoka kujivua gamba la zamani lakini anabaki kuwa nyoka!

    ReplyDelete
  9. Makamba kashikilia nafasi hiyo kwa udini tu wala sio ufanisi na JK analijua hilo ...JK maji yamekufika shingoni udini unakuponza....amka watanzania tunataka utekeleze ahadi zako na mkeo na mwanao wakati wa uchaguzi..acha bla..bla...!

    ReplyDelete
  10. LAKINI KAMA KWELI KUWA ANACHUKUA MIKOBA YA MAKAMBA BASI NI KAMA KUMUONDOA NGURUWE NA KUMWEKA NGIRI MAANA CHILIGATI HANA JIPYA WALA NINI.CCM MMEKOSA WA KUWEKA HAPO? KWA NINI MSIMPE MTU ALIYEIMUDU KAZI HIYO? NAYE SI MWINGINE BALI NI HON. MANGULA KAMA KWELI CCM MMEZIKA MAKUNDI NDANI YA CHAMA.MKAPA INGILIA KATI SWALA HILI ILI KUNUSURU CHAMA CHETU KWANI KWA CHILLIGATI IS AS GOOD AS MAKAMBA WHICH IS VERY HOPELESS INDEED AT THIS AGE OF GLOBALISATION.YOURS GOOD SAMARITAN NGOHE M.S.N

    ReplyDelete
  11. Bado JK unazidi kumkumbatia Hosea?Mwache Makamba siasa ni porojo tunataka tuone ahadi zako na familia yako zinatekelezwa.....achana na chama wewe rais wa watanzania wote....siasa waachie akina Msekwa na Makamba hatujakupeleka Ikulu ukauze sura ungana na mawaziri wako MH.Magufuli na Mwakyembe mchape kazi achana na FITINA NA SIASA ZA KISASI....Unatupeleka wapi?...Swahiba wako Marsha kaanza ujambazi...TUTAFIKA?HATA MWEZI BADO MZEE,DU...HIYO YA MWAKA

    ReplyDelete
  12. Zama hizi hatutegemei mtu kuongelea nafasi za upendeleo kwa udini bila Mashiko. Huo ni unafiki uliojaa chembechembe za Ubaguzi wa kidini. Tujaribu kumchambua Makamba kwa madhaifu yake na sio kwa dini yake. Hivi kuna mtu anaweza kuthibitisha uteuzi wowote uliofanywa kwa sababu ya udini? Hivi leo EL na Chenge wangekuwa Waislam tungesemaje? Mdau acha udini, kwa staili hiyo wewe ukipewa nafasi utakandamiza sana watu wa dini fulani. hufai kuigwa na ujirekebishe.

    ReplyDelete
  13. Mzee wetu Mkamba apumzike, awaachie watu wengine nafasi hiyo

    ReplyDelete
  14. Nimefurahi sana kusikia Makamba anatimuliwa.Amefanya makosa mengi nadani ya CCM pamoja kumdhulumu Bashe wa Nzega kutangaza yeye si raia wa Tanzania.Pia alimkufuru Mungu alipokwenda Pemba [Zanzibar] na kusema 'Mungu oyeee".Adhabu ya Mwenyezi Mungu inamuanza,bado mutasikia mengi.

    ReplyDelete
  15. Ndugu yangu Ngohe mchangiaji mwenzangu hapo juu,Kikwete hawezi kumchukua Mh Mangula hata kama anafaa kwani yeye alikuwa akimpigia "CHAPUO" Ndugu Salim Ahmed Salim wakati wa mchakato wa ugombea urais 2005,kwa ufupi Mangula si MWANAMTANDAO,na hata kama ni kiongozi mzuri vipi kama si mwanamtandao hupati hata ukatibu kata,hakuna ubishi VIATU VYA MANGULA ,MAKAMBA HAVIWEZI KUMTOSHA ,angalia ccm ya katibu Mangula na ccm katibu Makamba je huoni tofauti?,HII NI SERIKALI YA KIUSHIKAJI BWANA ,SIYO MAADILI KAMA NDUGU YANGU UNAVYOFIKIRI!

    ReplyDelete
  16. Ahmad
    Ni bora Makamba apumzike namkumbuka akiwa Tanga Mkuu wa wilaya mimi nikiwa na miaka 20 sasa nakimbilia 60 yeye bado yupo,atakuwa amechoka,ni bora mzee wetu apumzike na tuache kumsakama kalifanyia kazi kubwa taifa hili,tuwe na adabu na heshima kwa mzee wetu huyu tuache kuropoka maneno ya hovyo

    ReplyDelete
  17. chiligati nenda na ukakiboromoe kabisa ccm ifie mbali na jk wake hicho si chama ni genge la wahuni na mafisaidi

    ReplyDelete
  18. Aah mnaliacha genge la wahuni wa mjini city centre, wachezeshaji wa disco na wauza pombe na kuisakama CCM eti genge la wahuni. Wewe tazama tu fujo zao utajua kuwa hawa ni wahuni tu maana hata huko vijijini wameanza kuwaiga, kama vile majuzi tu wamempiga mtoza ushuru kwenye kituo. Na kukataa matokeo halali na kushindwa kutoa ushahidi wa kuthibitisha kuwa mmeibiwa ni nini kama si uhuni uliokubuhu?

    na kwanza nyie chama si chenu yanayojiri ndani yake yanawauma nini? Kwenu kunatokota bado kuungua mnakimbilia kwenye vyungu vya wenzenu. Ruzuku hiyoo inawatafuna sasa hivi! Waacheni CCM na mambo yao na nyie hangaikeni na ya kwenu.

    Yenu yanawashinda ya wenzenu myavyalia vibwaya!

    ReplyDelete
  19. Kuboronga kwa Makamba lawama zangu zote kwa Kikwete kwani Philip Mangula alikuwa mzuri katika nafasi ya katibu mkuu, kwanini alimleta Makamba?Huyu ameleta matatizo makubwa sana kwa kushindwa kukemea wanachama watovu wa nidham matokeo yake wale wote waliosimamamia haki hakuwataka hawa ni akina Mh Lucas Silelii, lakini watuhumiwa wote hakuwasema, katibu huwezi kuongoza chama hivyo huyu mzee alikuwa ajiwezi mpaka tukafikia kuiita ccm ya swahili,hakuna kitu chochote makamba ataongea uelewe anaongea nini, mzaa, utani, matusi na kiburi basi lakini yeye akashindwa kujua kwamba ccm ni katibu mkuu, ukimuuliza asilimia ngapi ameimarisha chama kwa kwenda mikoani ajui na hajawahi kwenda ndiyo maana uchaguzi ulikuwa mgumu sana kwa ccm, kwani chadema waliimarisha chama kupitia operation sangara.Kikwete tunamtaka Mangula Philip arudi ccm kama katibu mkuu, alifanya kazi nzuri sana, kwani hata chiligati siyo mzuri.

    ReplyDelete
  20. duniani si kwamba kila mtu atakupenda, lakini kama kila mtu anakuchukia, basi una tatizo.

    ReplyDelete
  21. Makamba aende, ameleta udini, hana busara , mropokaji, hekima zero. JK ajifunze na aache kukumbatia mafisadi, asipoangalia CCM itamfia mikononi.
    Elizabeth -Bukoba

    ReplyDelete
  22. hana busara mzee huyu,angalia alivyotetea mafisadi na kumngoa spika sitta

    ReplyDelete
  23. Mtashangaa na roho zenu atakapowepa nafasi nyeti yenye ulaji na shukrani.Mnawajua waswahili mnawasikia? mmenyamazishwa na uteuzi wa mawaziri subirini post nyingine. Rais ana madaraka ya kuteua watendaji wengi tu katika nafasi nyeti serikalini bila kupitia bunge. Bodi na kurugenzi nyingi zinalipa mishahara mikubwa tu kuliko nafasi zenye majina. Je unafahamu mshahara wa kiongozi yeyote kwenye EAC? au Board Member wa bandari? au balozi wetu Italy na Brazil? mtaendelea kushangaa. Unafiki wa waswahili umefunika roho zao ukianacho sio kilichoko rohoni mwao. Ukitaka kujua kwa undani fuatilia shughuli zao za kifamilia.

    ReplyDelete
  24. CHAMA KINAHITAJI KIJANA ILI AWEZEKWENDA NA MABADILIKO YA KISIASA SASA HIVI WAPIGA KURA ZAIDI YA 70% NI VIJANA NA CCM IMEWASAHAU KABISA CHAIRMAN HEBU TUPIA HAPO KWENYE UKATIBU MKUU WA CCM MH.DK NCHIMBI HATA MIMI NITARUDI CCM, NA NINAKUHAKIKISHIA NDIYO MTU PEKEE ANAYEWEZA KWENDA NA KASI HII YA VIJANA

    ReplyDelete
  25. Wewe unayesema waswahili wewe ni mdini, na uasumbuliwa na tatizo la udini, limekuganda hilo, mlitaka nafasi zetu 100% mupewe nyie na watu wengine hata kama wana uwezo na wamesoma na watendaji wazuri wasipate nafasi kama enzi zile za Mtakatifu alivyoweka wakatoliki kila sehemu. Sasa waswahili tuko macho au mmesahau kuwa hata hizo 1/3 ya nafasi tunazopata na zinawauma tulizipigania kwa nguvu zote? Mmesahau harakati na maandamano yetu na virungu na mabuti ya polisi tuliyokuwa tunapigwa tukidai haki zetu?

    Sasa tumepata hiyo 1/3 au one third mnaanza kutufuata fuata kama vile tumepewa 1/2 au nusu au 50%. Subirini tuanze kuadai mgawo wa 50/50 ndio mtatujua waswahili ni kina nani. Tumewanyamazia, tumewachekea, tumewapokea kwenye miji yetu, na bado mnatutukana, mmesahau kuwa usafi na ustaarabu mmeutoa kwetu. Hapa sio mahala pake lakini ngojeni tuanze kudai kuanzia kwenye baraza la mawaziri sawa kwa sawa, kama wabara/wakristo 10 basi na waswahili/pwani waislamu wawe 10. Na nafasi nyingine za ukurugenzi na ukuu wa wilaya tutaanza kudai mgao wa sawa sawa, maana wote ni binadamu tulio sawa na kila mtu anastahili heshima.

    Tatizo mnadhani ustahamilivu na ukarimu wetu ni weakness yetu lakini tukilianzishaga wote mnajichimbia ndani!

    ReplyDelete