WADAU
wa kilimo nchini wameitaka Serikali kuuangalia upya mfumo w a k u w a k o p e s
h a wakulima pembejeo za kilimo.
Pia
wameitaka kuangalia mfumo wa kuwakopesha wakulima kwa kupitia taasisi za
kifedha ili ulete manufaa kwa wakulima wadogo nchini.
Hayo
yalibainishwa juzi mjini Dodoma na wadau hao katika semina kwa wakuu wa mikoa
na wilaya nchini iliyolenga kuutambulisha mfumo mpya wa kuwakopesha wakulima
ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa kupitia benki na kuongeza kuwa mfumo huo
unaweza kumfanya mkulima mdogo ambaye ndiye mlengwa akashindwa kukopeshwa
kutokana na urasimu uliopo katika taasisi hizo za kifedha.
Pia
walisema kuwa wakulima wakubwa ndio mara zote wamekuwa wakitumia taasisi hizo
kukopa fedha kwa ajili ya kilimo chao hivyo wasije wakajinufaisha wao binafsi
kupitia mfumo
huo na kuwasahau wakulima wadogo.
Akizunguma katika mkutano huo, Mkuu wa
Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza aliwataka wadau hao kutotanguliza kushindwa
kwasababu kila jambo lina changamoto zake na badala yake waende kusimamia mfumo
huo kwa umakini ili uweze kuleta tija kwakuwa wananchotaka wakulima ni
kuoneshwa njia ya jinsi ya kutumia mfumo huo ili waweze kujiongezea kipato.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto
Mbwilo alieleza kuwa mfumo huo unahitaji usimamizi wa karibu kutoka kwa wadau
wote wa kilimo ili uweze kufanikiwa kama ulivyokusudiwa.
"Hakuna kitu kinachofanikiwa bila
ya kuwa na usimamizi wa karibu na ndiyo maana hata mfumo wa vocha za pembejeo
kwenye baadhi ya maeneo ulishindwa kufanikiwa kutokana na kutokuwa na usimamizi
makini," alisema Mbwilo.
Awali Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Christopher Chizza alisema wameamua kuutambulisha mfumo huo kwa wadau
ili kupata maoni yao kuhusiana na mfumo huo kabla ya kuanza kuutumia kwa
wakulima nchini.
Alibainisha kuwa mfumo wa vocha za
pembejeo ulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo udanganyifu kwa watu waliopewa
dhamana ya kugawa vocha hizo ndio hivyo kuwataka wadau hao kuukubali mfumo huo.
Hata hivyo
alibainisha kuwa mfumo huo utakwenda sambamba na vocha za pembejeo hasa kwenye
maeneo ambayo yalionesha mafanikio makubwa ya kilimo kwa kutumia mfumo huo.
No comments:
Post a Comment