*ASEMA MAKAMPUNI 45 YAJITOKEZA KUTAKA KUWEKEZA
*KUZINDUA UJENZI KIWANDA CHA SARUJI, AJIRA NJE NJE
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
SERIKALI
imesema kuwa, makampuni 45 tayari zimejitokeza na kuomba kuwekeza mkoani
Mtwara, baada ya ugunduzi wa gesi asilia kwenye Bahari Kuu Kusini mwa Tanzania.
Makampuni
hayo ni pamoja na Dangote Industries ya Alhaj Dangote ya nchini Nigeria inayotaka
kuzalisha saruji tani milioni tatu kwa mwaka na kitaajiri wafanyakazi 1,000
ndani ya kiwanda na nje 9,000 ambao ni wakala, wasafirishaji, wajenzi, wauzaji
rejareja.
Waziri
Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, aliyasema hayo mjini humo jana
kwenye Ibada ya kuwekwa
Wakfu Askofu Lucas Mbedule wa Dayosisi mpya ya Kusini Mashariki ya Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
“Kesho
(leo), nitaweka jiwe la msingi la Kiwanda cha Saruji cha Dangote...viwanda
vingine vinavyotarajiwa kujengwa hapa Mtwara ni kile cha mbolea, bidhaa za
plastiki na kusindika gesi asilia kwenye mitungi,” alisema Bw. Pinda.
Alisema
hivi sasa kuna viwanda vinne vya saruji nchini vyenye uwezo wa kuzalisha tani
3,000 kwa mwaka, ila vinazalisha tani milioni 1.2.
Aliongeza
kuwa, Bandari ya Mtwara nayo
itapanuliwa pamoja na kujengwa reli ya kuunganisha mkoa huo na machimbo ya
chuma yaliyopo kwenye mikoa jirani.
Bw. Pinda
alisema ofisi yake ndiyo inayoratibu Kituo cha
Uwekezaji
nchini (TIC), ambapo viwanda vitakavyoanzishwa mkoani humo kutokana na ugunduzi
wa gesi asilia vitakuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo
na Taifa kwa ujumla.
Alisema viwanda vyote ambavyo
vitajengwa mkoani humo vitakuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi kwa wana Mtwara
hususan kwenye suala la ajira na kukuza kipato chao.
“Kuhusu tatizo la maji hapa Mtwara,
nimemuagiza Waziri wa Maji alete wataalamu waje kuangalia uwezekano wa kupata
maji kutoka Mto Ruvuma unaotenganisha Tanzania na Msumbiji,” alisema.
Aliwataka viongozi wa dini watafute
mbinu za kuhakikisha Taifa linaongozwa kwa amani ili kuleta maendeleo ya
kiuchumi.
Aliahidi kushughulikia maombi ya
KKKT kupata ardhi eka 30 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Elimu, wilayani
Masasi.
Bw.
Pinda aliwasili mkoani humo juzi akitokea mkoani Dodoma kwa ajili ya kushiriki
ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu Mbedule na uzinduzi wa miradi ya viwanda
vitakavyotumia gesi
No comments:
Post a Comment