24 May 2013

Obama kuja na watu 700

Na Rehema Maigala


 RAIS wa Marekani, Bw. Barack Obama, atakuwa na ujumbe wa watu 700 katika ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema kutokana na ziara ya kiongozi huyo, alitoa wito kwa wafanyabiashara wenye hoteli, migahawa, magari ya kukodisha waziboreshe biashara zao ili Wizara hiyo iingie mkataba nao.
Aliongeza kuwa, akiwa nchini, Bw. Obama atafanya mkutano na viongozi wa nchi zinazoendelea kwa kuzungumzia umuhimu wa sayansi na teknolojia katika nchi zao.
“Ugeni huo ni mkubwa, ujio wa kiongozi huyu utaisaidia nchi kupata pesa
za Miradi ya Changamoto za Milenia (MCC), ambazo zitatumika katika maji, elimu na barabara.
“Pia Rais Obama atazungumzia jinsi nchi za Afrika zitakavyopata umeme wa kutosha tofauti na sasa...kimsingi tumejiandaa katika mapokezi yake hata kwenye mavazi,” alisema Bw. Membe.
Hata hivyo, Bw. Membe alisema tayari baadhi ya ujumbe ambao ataongozana nao umeanza kuwasili nchini kwa matayarisho.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. John Haule, alisema Umoja wa Nchi za Afrika (AU), kesho unafikisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema maadhimisho hayo yatafanyika Makao Makuu ya umoja huo Addis Ababa, nchini Ethiopia ambapo nchini Tanzania, yatafanyika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo nchini atakuwa Bw. Membe ambaye atakuwa na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.
Bw.Haulea lisemaumoja huoulianza mwak a1963 a mbapohadi sasamafa nik iowaliyoya patani onge zekolawa nachamakuto ka32hadi54,kupat ikanakw auhuruwa nchi ya S udanKusin i,vio ngozi wanawak ebaraniAf rikanawananchiku waheshi muviong ozi wanchi zao .
A lisemambali ya mafanikio waliyopa tapiakunachangamotozilizopoka tika nchi wanachama kamatis hiolaugaidi, uh aramiana hali te tekati ka baadhiyanchi kam aSomalia na Mali.

14 comments:

 1. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema"uunaweza kupewa chembe za chupa ukambiwa ni almasi halafu ukaenda unashangilia kama zuzu........." tunaangalia mantiki iliyopo ya ujio wa watu 700 wote wakiandamana na Rais Obama,Tunashangilia na kuandaa mapokezi eti tutafaidika,tumesahau yakwamba tumezidiwa utashi ya kwamba tujiandae kwa vita ya utashi kuliko kuandaa mahoteli na usafiri!,..tuamke Watanzania!

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ni kweli unachosema lakini ni kawaida kwa Watu kulaumu alipoangukia badala alipojikwa.Ndugu yangu unapashwa kujua kuwa Soko la Uchumi wa dunia liko wako ndipo ungenena hayo unayoyasema na kama hujui ingekuwa vizuri uulize uambiwe, huwezi kuamuka wakati njia kuu ya wewe na mimi kuamuka imeshikiliwa na mataifa ya Mangaribi au hujui hilo.............''

   Delete
 2. Nakuunga mkono, maana wakati umefika Watanzania tufunguke akili zetu na tuangalie mbali, maana Watanzania tumezoeya kupokea vya bure na hatuangalie baadae tunaangalia karibu sana tena tukijua leo tuna lala njaa basi ukiona wakukupa msaada unasahau kuwa msaada utakaopewa leo kesho je atakuja utaenda tena kwa mwingine na mwisho wake unakuta hata pa kuishi huna maana ulisha binafsisha hata familia yako kwa kukosa kuangalia mbali. WATANZANIA TUTAZAME MBALI SANA, maana tunasema Tanzania ni nchi ya haki na amani lakini si kweli na tuendapo ndiyo mbaya zaidi,

  ReplyDelete
 3. Tunapenda Kumshukuru Mungu ambaye anatupa viongozi waadilifu wa kuongoza watu wake.Aidha napenda kutoa shukrani zangu kwa serikali ya Marekani chini ya Uongozi wa raisi Baraka Obama kwa kuchagua kwanza kuja Tanzania kabla hata ya kwenda nchini kwake Kenya

  Hii ni kuonyesha ni jinsi gani Marekani ilivyo na imani na Tanzania na watu wake kwani tukirudi nyuma tunakutana na maraisi kama Clinton na raisi Bushi wote waliona ni heshima kudhuru Tanzania wakiwa madarakani

  Serikali ya marekani imetawaliwa na watu weupe kwa karne kadhaa tangu miaka ya 1700 hadi Mungu alipoona sasa yatosha mtu mweusi naye atawale taifa hili kubwa

  Tunachotakiwa sisi watanzania kuchuma toka kwenye taifa hili ni maendeleo walionayo. Lakini ni lazima tuwe na akili kwani sisi ni wachanga sana na wao wameendelea sana hata kufikisha tecnologia yao kwenye sayari nyingine kama mwezi na Mars

  Tanzania tuna kila kitu ambacho marekani inahitaji, tukianza na gesi asilia tuna nyingi sana ambayo kama viongozi wetu hatutatumia hekima na busara katika kuingia nao mikataba tutaishia kuwa maskini kwani tusisahau kuwa bado siasa yao ni ubepari na tumkumbuke mwalimu alisema nini kuhusu ubepari

  Eneo jingine ni madini , marekani inahitaji sana madini yetu hasa dhahabu na Tanzanite, ukija hapa kuna kiwanda cha kukata Tanzanite madini pekee yanayopatikana ulimwenguni wamarekani wana fedha zao wanapenda vitu vizurikama hayo madini yanayopatikana Tanzania Tanzanite kazi ni kwetu viongozi tusinunuliwe tufanye kwa maslahi ya Taifa zaidi

  Tunaweza kunufaika sana na secta ya Umeme lakini tusisahau hata Richmond ni kampuni ya kimarekani pia ni jinsi gani watanzania wanaingia mkataba na ujumbe atakaokuja nao Raisi Obama kwa maslahi ya Taifa zaidi

  Tukija kwenye secta ya barabara hapa kuna barabara nyingi na nzuri mno hata zinapita chini ya bahari tukiwatumia vizuri kwa maslahi ya Taifa tutafurahi, kuna flyover nyingi mno, madaraja yanayo pita juu ya bahari ni mengi mno tuwakaribishe kwa kukumbuka usemi wa mwalimu

  Yapo mengi ambayo tunaweza kuyapata kutoka kwao hasa chini ya Riasi mweusi Baraka Obama ambaye naye angependa kuishi Tanzania baada ya kustaafu kwake kwani hata jina lake linafanana na la watu wa Kilimanjaro , yaani Barakaeli

  Tusisahau secta ya Kilimo wenzetu wana mashine na mitambo mingi kwa ajili ya kuzalisha chakula lakini tusisahau sheria zao za trace passing maana yake ukishaingia naye mkataba usipoangalia utakuwa mtumwa wake kwani hata kwenye shamba huruhusiwi kukatiza ukikatiza ni kupigwa risasi

  yale tunayoona watanzania tunataka kupata kwako tuwe waangalifu na mikataba hata ikiwezekana kuandika mikataba kwa lugha ya kwetu /kiswahili ili tusome kila neno kwa ufasaha

  Tuitumia hiyo baraka kwa manufaa ya watanzania wa leo na vizazi vijavyo

  Karibu Raisi Obama Tanzania Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nakushukuru kwa kuainisha maeneo muhimu ambayo twaweza kufaidika kwa ujio wa rais Obama.....Je, je jeeee viongozi wetu wameelewa wamesikia ulichosema...Karibu Obama

   Delete
 4. Kuja na ujumbe wa watu 700 ni tishio. Kunavitu vipo tayari kwenye mikatba ya sri inakuja kusainiwa. Delegetion ni kubwa mno hata mjinga atashtuka. Kila Raisi wa marekani anakuja Tanzania kwa speed kubwa kwenye awamu ya mwisho wa utawala wao.Bush alikuja kutoa misaada ya ukimwi ambapo hakutoa chote alichoahidi. Badala yake, Alikwenda na kutumia muda mwingi munduli, unajua almasi kule na Lowasa. Alikwenda namtumbo, kwenye Uranium. Sitashangaa kama vita hii ya Mtwara ni mmojawao ya vipengele vya gesi na mikataba ya marekani. wamtwara watachapwa viboko kupisha Njia mzungu na raisi wa marekani kufosi ubia. Mengi anajiandaa najua anafahamu fika yupo tayari kwa mikataba hiyo bila kuweka wazi kwa manamtwara na maeneo mengi namtumbo pia. Wameshazungumzia umeme, badala ya Watanzania kujulishwa kabla ya ujio huu kwamba uranium, Gesi, mbegu za kilimo zenye sumu na kuzizungumzia kabla hazijapokelewa, Mengi na Raisi wetu wameshazipokea watawapiga na kuwaua wananchi kwa kufosi. Hii si Domokrasia. Na kama Amerika inatangaza Demokrasia pia ni potofu, inajali maslahi ya America kwanza kwa nchi ambazo viongozi wake wamelala na hawana uzalendo kamili, wala hawananguvu ya kusimama kama mwanaume mwenzao kabla ya kujiweka kwenye kona na kusema ndio. Inferiority complex ya Wasomi wengi Waafrika ni mzigo kwa Africa.Kama mikataba i00 itasainiwa ukiongeza na ya wachina zaidi ya mia, waingereza, Warusi, Wanetherland, ufaransa, Njia zote kuu za uchumi nchini zimekwisha. Najua wanakuja na CIA patakuwa shwari. Askari wetu watawanyanyasa watanzania kama vinyama.
  Maendeleo Ya kisayansi na tecknnologia MMmm.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Asante sana watoa maoni kwa kutahadharisha serikali. Lakini jiweke kama wewe ndiye mheshimiwa raisi. Mwenye nguvu anakuja kuchukua chake. Hebu angalia mfano wa pakistan ambayo ina nguvu hata za nyuklya na kisiasa imeendelea zaidi yetu. Kwa vile ina wanasiasa wa mrengo wa kushoto wengi. Wenye hata hulka ya kujilipua na kujiua kwa kutetea kile wanachoona kua ni haki yao. Lakini Wamarekani wanaingia na kutoka kama vile wanaingia choo cha umma! Naona tuwashauri viongozi wetu. Hiyo ni vyema. Lakin tuwe na muelekeo chanya wenye kutunza heshma ya taifa letu pamoja ne utamaduni wake wa amanai na upendo. tatizo ni kwamba kila kiongozi wa Kiafrika, awe wa sasa ama atakeyekuje, hata kama ni mwanamapinduzi kiasi gani breki ya kwanza Uingereza ama marekani. Labda tuwe na watu kama akina Mgabe, ambao pia wanapigwa vikali na wanachi wao, ingawa wameuiliwa kwenda Ulaya na marekani. Labda tupate viongozi amabo watasema Marekani hatuendi ndipo uzalendo utakapooneka. ingwa uzalendo huo utafuatiwa na adhabu kali ya kutengwa kama ilivyo Irani. Je waheshimiwa mko tayari kukinywea kikombe cha Irani, Korea Kaskazini na Zimbwambe. Mimi niko tayari kabisaaa!Uzalendo sio kusema maneno matamu bali ni kua tayari kukabiliana na athari za maneno yako

   Delete
  2. Atakayefanya fujo apigwe vizuri. Maanake siku zote tulikua na rasmali, tumekaa juu yake hatukuzifanyia kazi yoyote. Hiyo gesi, dhahabu, yureniam na mengineyo yavijapatikana kufutia ujio wa Obama. Tusijaribu kujitia wajanja kwa vitu tusivyovigundua sisi ila vimegunduliwa na hao hao mabeberu. Hata wachina wana heavy investment kutoka Marekani kiasi kwamba Marekani ikiondoa vitegauchumi vyake uchumi wa china utayumba sana. Ni kweli tunapaswa kua jasiri kulinda rasmali za nchi kwa silaha yoyote ile, hata rungu, mishale na majambia. Lakini tunataka mwenye hekima atangaze mbinu mpya sio kurudia yaleyale yaliyomshinda Nyerere.Nyerere alizilinda mpaka leo hatuwezi kutengeneza hata baiskeli ya mbao tukavinjari nayo barabarani. Kua na adui mwenye nguvu zaidi yetu na mjanja zaidi yetu kusitufanye Watanzania kujengeana chuki na lawama zisizo na sababu tukaja kuuana bure!Hata kama mikataba ikiandikwa kwa kiswahili bado tutapunjwa tu kwani wao ndio waliandika kamusi za kiswahaili ama kufadhili unandishi wake.

   Delete
 5. Wewe Mr/miss AnonymousMay 25, 2013 at 10:24 PM.Uzalendo"achana na hizo propaganda zako ambazo unahubiri hapa.toka miaka 50 ya uhuru wa Tanzania,hatujaweza kujikomboa hata kiuchumi.Hatujui hata kubunia mashine ya kutengeneza wembe,sasa technologia ya kuchimba hayo mafuta na gasi n.k. ni zao,Hatuwezi kuendelea kukalia utajiri tukijifanya wazalendo, huku hatuna hata dawa ktk mahospitali yetu,madesk ya kukalia watoto wetu shuleni n.k!n.k.
  Kumbuka uchumi ulimwenguni sasa hivi umeungana kiasi kwamba inchi haiwezi kujitenga peke yake na uzalendo wake,hata iwe tajiri kiasi gani.Cha maana hapa ni kuwa makini na mikataba itakayosainiwa na hao viongozi wetu,je ina faida na Watanzania wote?

  ReplyDelete
 6. Boniface FaustineMay 30, 2013 at 1:50 PM

  ujio wa watu 700 mh kwangu ni tishio, Hivi gharama za kuwapokea zinatoka wapi? ndugu zangu watanzania si kila unayemsikia analia chumbani basi atakua amepigwa, wangine wanalia bse wamefurahi nk...hatujui yatakayokuja mbele nyuma ya watu 700?kumbuka mwenye harufu atafuatwa na inzi lkn nini kazi ya inzi?kama si kukuonyesha unaharufu mbaya? tusipojua kutumia tulivyonavyo basi wapo wajanja watatusaidia kutumia,Tanzania hii si nchi yenye kulia umasikini eeh MUNGU tusaidie tupate viongozi bora..NDUGU ZANGU MBONA TUNAKUWA WATUMWA KTK NCHI YETU WENYEWE? DAH INAUMA SANA

  ReplyDelete
 7. Hebu tueleze jinsi wewe na hao viongozi bora mtakavyotumia hizo raslimali ili tukuone mtu wa maana. Hebu eleza soko lako la nje na ndani liko wapi?

  ReplyDelete
 8. yote nisawa tu maana mwenye nguvu mpe

  ReplyDelete
 9. Duniani hapa kuna watu wajinga sana. Mtu anasema anaomba Mungu Obama akistaafu aje aishi Tanzania. Huu ndiyo umaskini wa fikra ambao tunaambiwa ni mbaya kuliko wa kipato.

  Mtu hakai akifikiri jinsi ya kukuza biasara kwa kutumia opportunities zilizopo kama AGOA n.k. Mawazo yote yameganda kwenye aid tu,

  ReplyDelete
 10. Huna jipya. Umeshajifunza vizuri nadharia za South-South cooperation, Demand for New Economic Order, Non-alignment Movements, Science of Poverty etc.? Tunachohitaji kwa ukweli ni resistance na wala sio victory. Wakija Wamarekani waelezwe hatutaki hili na lile. Litakua jambo jema. Tumia lugha inayofaa kwa vile matamanio yako yote ni ya kweli lakin hayatekelezeki. Inawezekana hapo uliko ukawa umevaa suruali ya kichina ama ya mtumba. You are not freeman!

  ReplyDelete