Mohamed (25), amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela
au faini ya sh. milioni tatu baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka
matatu.
Mashtaka hayo ni kutoa taarifa za
uongo katika mitandao ya simu za mkononi na kutuma ujumbe wa maudhi kwa Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema.
Mshtakiwa huyo alisomewa hukumu hiyo
jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na Hakimu Hellen
Liwa ambapo upande wa mashtaka uliwakilishwa na wakili Bw. Ladslaus Komanya.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Liwa
alisema hayo ni makosa mapya yaliyo katika Sheria Mpya ya Mawasiliano na
Mitandao.
“Kwa kitendo ulichokifanya kuwatumia
ujumbe viongozi wa juu wa
serikali unahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au
kutoa faini ya sh. milioni tatu iwe fundisho kwa wengine, kama hujaridhika na
adhabu unaweza kukata rufaa,” alisema.
Katika maelezo ya awali, ilidaiwa
Mei 20 mwaka huu katika Makao Makuu ya jeshi hilo, zilipelekwa taarifa za
kiintelejentsia kwa maofisa wa ngazi za juu kuwa kuna mtu ambaye namba yake ya
simu imesajiliwa kwa mitandao tofauti.
Namba hizo ni 0687 521947 na 0687
521948 za Airtel na 0759 799956 ya Vodacom zilizokuwa zikitumika kutoa ujumbe
kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na IGP.
Baada ya upelelezi kufanyika,
ilibainika namba hizo zilisajiliwa kwa majina tofauti ambayo ni Fadhili Issah,
Fadhili Issa na Godfrey Joseph ambazo alikuwa akizitumia mshtakiwa.
Baada ya mshtakiwa kukamatwa Mei 25
mwaka huu na kuhojiwa polisi, alikiri kutumia namba hizo na kuzisajili kwa
majina tofauti kwa lengo la kufanya uhalifu na kuficha utambulisho wake.
Mei
27 mwaka huu, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka
yanayomkabili na kukiri kutenda makosa hayo
No comments:
Post a Comment