18 May 2013

Mchungaji, wanakwaya wapigana kanisani

Na Moses Augustine, Sengerema


 KATIKA hali isiyo ya kawaida, ugomvi mkubwa umetokea kwenye Kanisa la AICT, kati ya baadhi ya wanakwaya wa kanisa hilo linalofahamika kwa jina la “Bupandwa” na mchungaji wao Petro Masule.
Tukio hilo la aina yake, limetokea kwenye Kijiji Bupandwa,Kata ya Bupandwa, Wilaya ya Sengerema, mkoani  Mwanza.
 Wanakwaya hao walisimamishwa kutoa huduma Kanisani kwa njia ya uimbaji kwa kosa la utovu wa nidhamu ambapo ugomvi huo, ulitokea Mei 12 mwaka huu, baada ya ibada.
Inadaiwakuwa , Mchungaji Masule hakutumia lugha nzuri baadayakuwaitawanakwaya hao “watenda dhambi ambao hawapaswi kuingia katika hekalu la Bwana”.
Kauli hiyo inadaiwa kuwakera wanakwaya hao ambao kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo, walisema Mchungaji Masule aliyasema hayo katika mahubiri ya ibada ya kwanza.
Mchungaji huyo alidai kuwa, kutokana na makosa waliyotenda wanakwaya hao, wanapaswa kutubu ili waweze kuingia kanisani.
Baada ya ibada hiyo kumalizika, baadhi ya wanakwaya waliokuwa wamesimamishwa ambao walihudhuria misa hiyo, waliamua kuungana na kumfuata Mchungaji huyo akiwa na wazee wa kanisa wakihesabu sadaka.
Wanakwayahao walimuomba Mchungaji huyo awape vyombo vya kuimbia ambavyo walidai kuvinunua kwa fedha zao ili wakaazishe kanisa lao wakidai kukerwa na mahubiri yake.
Kutokana na matakwa ya wanakwaya hao, ilitokea vurugu kubwa ndani ya kanisa hilo kati yao na Mchungaji Masule, ambapo katika ugomvu huo, inadaiwa muumini mmoja aliumia sehemu mbalimbali za mwili wake.
Gazeti hili lilipomtafuta Mchungaji Masule, alikiri kuzipiga na wanakwaya ndani ya kanisa hilo ambao walikiuka maadili na matakwa ya kanisa kwa kutokufuata sheria na kanuni.
Kwa upande wake, Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Vincent Ngidingi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kulaani kitendo kilichotokea kanisani hapo na kuwaasa waumini kufuata sheria za kanisa.

9 comments:

  1. sasa wandamu tumefika pabaya hadi shetani ameumia mbavu kwa kicheko. hii yote ni kutona na kuwa nje ya uwepo wa Mungu hivyo hakuna hofgu ya Mungu tena. Mchungaji na wanakwaya hao wote wanatakiwa kujutia tendo hilo na wajidhili mbele za mungu na kutubu na kumrudia Mungu upya.

    ReplyDelete
  2. Yessssss!!!!! kutoka bungeni hadi church, sasatujiulize ndiyo kujitambua au nini!!!!

    ReplyDelete
  3. dah hii sasa kali au mchungaji ali apply af akatoswa?na hii ina7bshwa na uanzishaji wa makanisa kiholele km walokole wazipga cc wapagani twafanyajeeeeeeee?

    ReplyDelete
  4. Kuimba sikuzote ni kazi ya Shetani alielaniwa na Mungu ,Hii kukaa makanisani kike kwa kiume nusu uchi kifua wazi matiti nje cio ibada jamani. any way kama hoa walikosa kwa bwana mbona pesa hawakurudishiwa wenyewe ,wamejifungia ndani kuhesabu jioni kwenye..... .

    ReplyDelete
  5. yangu macho, kwaya vigelegele kwa wingi lakini mhhh....... mnamambo/ hivi ukinunua vyombo kanisani vya muziki vinakuwa ni vyako sk zote au huwa ni mali ya kanisa kwa sababu mlitoa sadaka zenu kwa kununua vyombo hivyo ili kumtukuza MUNGU??Je mbona hamkudai na sadaka zenu za kila Jumapili mlizokuwa mkitoa sk zote???mnadai vyombo mlivyovitoa kwa SADAKA KWA MUNGU AU MLIVITOA KWA MCHUNGAJI??NAULIZA MLIVYOTOA VYOMBO HIVYO MLIVITOA KWA AJILI YA MUNGU AUIKWA AJILI YA KUMWAZIMISHA MCHUNGAJI WENU????AU MLIMKOPESHA MCHUNGAJI WENU???
    Na wewe mchungaji kwanini kuwafuuza moja kwa moja kanisani badala yA KUWAENGUA KWENYE UIMBAJI NA WAKABAKI WAUMINI WAKAWAIDA TU???KWANI WOTE WANAOSALI HAPO KANISANI KWAKO UNAUHAKIKA HAWANA dhambi au makosa yoyote???maana asiye na dhambi ni MUNGUpeke yake je kwa mwanadamu inawezekana hilo kutokuwa na dhambi???kilichotakiwa ni kuwaengua kwenye uimbaji tu na siyo kuwafukuza kanisani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hao ndio wanaojiita waenda minguni,biblia imetuonya kutubu,kunyenye kea,kutojivuna.vilevile kutojiinua juu ya wapakwa mafuta WA bwana!je!biblia tunazibeba mfano tu? Hatujifunza juu ya DAUDI na mfalme sauli?
      Halafuwewe ununuaye vyombo na kuzidai hunakumbukumbu ya annania na safira mkewe mbona umeitafuta laana kabla ya muda wake? Ok hayo ni maamuzi yako ila kumbuka kuna na wengine pia fedha zao zimo kwenye vyombo hiyo.
      Acheni kumhuzunisha ROHO Mtakatifu

      Delete
  6. Baada ya kukujibu sasa ninataka nikupe siri moja kubwa iliyijificha ktk nyumba nyingi za ibada duniani wengi huja kama wacha mungu tena waimbaji wazuri sana wenye vocal but in the real sence ni tipical devil woshiper and agents.
    Watu hawa ni wepesi sana Mujitolea ktk kila kitu kinacho hitaji mchango makanisani mradi tu they can winn some weak Christian soul to satan so kama wakigundulika ndo haoooo wanzishaji WA vurugu makanisani maana wamemiss target.glry glory be to our almighty GOD
    AMEN.

    ReplyDelete
  7. hii si sawa kwa wa2 wa dini namna hii

    ReplyDelete
  8. Naona hata tusisumbue kichwa maana maandiko yako bayana na yanasema wanaomwabudu Mungu kwa roho na kweli tutawatambua kwa matendo,hao tuwaweke kundi lipi maana tusihukumu hukumu ni kazi ya Mungu ila tuwaonapo kama matendo yao hayaendi sawa na unabii tujitenge nao

    ReplyDelete