Na Florah Temba, Same
WANACHAMA w a Vikundi vya Kuweka na Kukopa (VICOBA) wamekabidhiwa simu za
mkononi bure,ili waweze kuweka fedha zao kwa njia ya kisasa na kuachana na
mtindo wa utunzaji fedha kwa njia ya masanduku.
Hatua hiyo ya
kuwakabidhi simu hizo ilizinduliwa Dar es Salaam jana na Makamu wa kwanza wa
Rais wa Vicoba Taifa Scholastica Kevela.
Akizindua
kampeni hiyo kwa wana Vicoba, Bi. Kevela alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza
taarifa za upotevu wa fedha na kuwarahisishia uwekaji wa fedha katika mazingira
mazuri.
“Hata kama simu
ya mkononi itaibiwa lakini fedha zilizokuwepo hazitaweza
kuchukuliwa labda
muhusika awe anafahamu namba ya siri na hivyo leo nitakabidhi kwa vikundi vya
Midizini A, Midizini B na Minazi Mirefu na juhudi hizi zitaendelea,” alisema.
Alisema vikundi vingi bado
vinaendelea kuweka fedha kwenye vibubu na kwamba hali hiyo ni hatari kwani
inatoa mwanya kwa vibaka na vishawishi kwa wale wanaotunza vibubu hivyo.
“Sasa hivi tunahamasisha electronic
vicoba (utunzaji fedha kwa njia ya mtandao) mnaweka fedha zenu kwa njia ya
M-Pesa, kwa sababu wanachama wengi wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa
fedha kutokana na utunzaji wa kwenye vibubu," alisema Kevela.
Makamu huyo wa Rais wa Vicoba,
alisema pia baadhi ya watu wamekuwa matapeli kwa kuchangisha fedha watu na
kutokomea nazo hivyo akawataka wanachama wa vicobakutunza fedha zao wenyewe.
Pia aliwataka wanachama wa vikundi
hivyo kuacha majungu na kufanya kazi kwa bidii ili kujikomboa kiuchumi.
Naye
Mratibu wa Ujasiriamali VicobaTaifa, Flora Masalu, alitoa wito kwa wanachama wa
vikundi hivyo kutokurupuka kwenda kuchukua mikopo bila kuwa na biashara ya
kufanya.
No comments:
Post a Comment