16 May 2013

Kukua kwa teknolojia duniani kunasababisha kuenea uhalifu

Na Rehema Maigala


KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdul Wakili amesema kukua kwa teknolojia duniani kunasababisha kuenea kwa wingi uhalifu.
Hayo alisema jana wakati akifunga mkutano wa 18 wa Maofisa wa Jeshi la Polisi Katika Nchi za Kanda ya Kusini mwa Afrika (SARPCCO) ambao ulikuwa na lengo la kujadili jinsi ya kukabiliana ya uhalifu.
Alisema wakuu hao kutoka nchi 14 wamekutana kwa ajili ya
kukaa pamoja na kuweka mikakati ya ushirikiano ili kupambana ugaidi ulioenea katika nchi za Afrika.
"Hivi sasa uhalifu umevuka mipaka kwa sababu ya kukua kwa teknolojia hivyo inatakiwa kukaa pamoja na kujadili suala hili ili liweze kupungua,"alisema Wakili.
Aliongeza kusema kuwa nchi moja ikikaa peke yake ili iweze kutatua tatizo la ugaidi haiwezi kufanikiwa inatakiwa kukaa pamoja na nchi zingine ili kupanga nini cha kufanya.
Alisema kuwa kukaa kwa nchi zaidi ya tatu kutasaidia kuleta mafanikio makubwa kwani nchi nyingine inakuwa na uwezo mdogo na nyingine inakuwa na uwezo mkubwa wa kujua nini cha kufanya ili kumaliza tatizo la uhalifu.
Vilevile alisema hivi sasa wahalifu wengi hutumia teknolojia ya kisasa ili kufanikiwa na mambo yao wanayoyafanya.
Naye Mwenyekiti wa SARPCCO, Saidi Mwema ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania mkutano huo umesaidia kujua njia mbalimbali za kuweza kuwafichua wahalifu wanaozitesa nchi za Afrika.
Alisema kuwa, sasa hivi wanataka kufichua vyanzo vinne ambavyo ndivyo vya uhalifu ni wachocheaji, wawezeshaji na wanaojilipua wenyewe kwa ajili ya uhalifu.
Mwema alisema kuwa k a t i k a mk u t a n o h u o watapeana taarifa na kubadilishana taarifa hasa katika makosa ya uharamia baharini na kuzagaa kwa silaha katika nchi za Afrika.

No comments:

Post a Comment