27 May 2013

CHADEMA wapata pigo Sengerema


 Na Mwandi shi We tu, Sengerema

 ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( BAVI CHA) , mk o a n i Mwanza, Bw. Slavatory Magafu, amekihama chama hicho na kujiunga Chama cha NCCR-Mageuzi.
Bw. Magafu alijiunga na chama hicho juzi wakati wa kampeni za kumnadi mgombea udiwani katika Kata ya Nyampulukano, wilayani Sengerema, Bw. Dotto Nungwa.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya NCCR-Mageuzi,Bw. Magafu alisema ame b a i n i CHADEMA hakiwezi kuifikisha nchi katika mikono salama.“Mwaka 2010 niliwania ubunge wa jimbo hili kwa tiketi ya CHADEMA, hivi sasa nimejiunga rasmi NCCR-Mageuzi chama ambacho hakina udini, ukabila wala ukanda,” alisema.
Kwa upande wake, Bw. Nungwa aliahidi kuwasaidia wananchikwa kumaliza kero zao na kuhakikisha wanashiriki mikutano yakata na vijiji pamoja na kusomewa
mapato na matumizi.
“ N i t a h a k i k i s h a namfuatilia mbunge wa jimbo hili ili fedha za Mfuko wa Jimbo zinufaishe wananchi wa Kata ya Nyampurukano na kuwasaidia wananchi waliodhulumiwa viwanja vyao ili warudishiwe,” alisema.
Viongozi wengine ambao hivi karibuni wamejiunga na NCCR-Mageuzi ni Bw. Eddo Makata aliyekuwa Katibu wa CHADEMA, Mkoa wa Mbeya na Bw. Deogratius Kisandu aliyekuwa Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Tanga.
Kampeni hizo za udiwani zinaoongozwa na Katibu wa Habari na Uenezi Taifa, Kitengo cha Vijana wa NCCR-Mageuzi, Bw. Kisandu pamoja na Kamishna wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Bw. Ramadhan Amran
Na Said Hauni, Lindi
ASKARI wawili wa Jeshi la Polisi akiwemo mmoja wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, wamelazwa katika Hospitali ya Nyangao, baada ya pikipiki waliyokuwa wakiitumia kugongana na gari ndogo.
Ajali hiyo ilitokea wakati askari hao wakimkimbiza mwendesha pikipiki aliyekuwa amekiuka Sheria za Usalama Barabarani. Kamanda wa Polisi mkoani humo, George Mwakajinga, alisema ajali hiyo imetokea wilayani humo Mei 20 mwaka huu.
Aliwataja askari hao kuwa ni F 6986 PC Living aliyevunjika miguu yote miwili na mkono wa kushoto na G 2116 PC Edwin, ambaye amepata maumivu ya ndani kwa ndani.
“Hawa askari walikuwa kazini wakiwa wamepakiana kwenye pikipiki aina ya Suzuki namba PT 2951, iliyokuwa ikiendeshwa na PC Living, waligongana na gari ndogo aina ya Land Cruiser namba T 398 AME iliyokuwa ikiendeshwa na Bw. Juma Mandundu.
“Ajali hii ilikuwa mbaya na dereva wa gari amejisalimisha mwenyewe Kituo cha Polisi Wilaya ya Nachingwea na atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika,” alisema.
Mashuhuda wa ajali hiyo, wameliambia gazeti hili kuwa, askari hao walikuwa wakiikimbiza pikipiki nyingine ambayo dereva wake alikaidi amri ya kumtaka asimame na kuelekea upande wa Barabara ya Masasi.
Walisema kitendo hicho kiliwafanya askari hao wachukue pikipiki yao na kuanza kumfukuza na walipofika katikati waligongana uso kwa uso na gari ndogo ambalo hawakuliona kutokana na vumbi.

No comments:

Post a Comment