MBUNGE wa Fuoni kwa tiketi ya
CCM, Bw.Said Mussa Zuberi, ameshangazwa na wabunge kupitisha bajeti za wizara
mbalimbali, lakini fedha hizo hazipelekwi kama zinavyoidhinishwa.
Alitoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya
bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Alisema
inashangaza wabunge kupitisha bajeti, lakini
fedha zinazotolewa ni kidogo na
vilevile hazipelekwi zote kwenye wizara husika.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za
Makao Makuu ya CCM,jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Bw. Nape Nnauye, alisema mkutano wa Kamati Kuu ya
CCM uliofanyika hivi karibuni, umeitaka Serikali kuhakikisha mizizi inang’olewa
ili kukomesha matukio ya aina hiyo.
Nape alisema kuwa CCM i m e r i d h
i s h w a n a h a t u a zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi wakati wa tukio
hilo. Alisema Kamati Kuu, ililaani matukio hayo kutokana na kuwa yanavuruga
amani, upendo na umoja wa Watanzania.
“Kamati Kuu imeishauri Serikali
kuongeza kasi kuwasaka na kung’oa mzizi huo ili kukomesha vitendo vya namna
hiyo,” alisema, Bw. Nape
Hata hivyo, Bw. Nape alisema Mei 18
na 19 mwaka huu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, atakutana na wabunge wa
chama chake pamoja na sekretarieti ya chama ili kupata maoni ya wabunge pamoja
na kushauriana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Akijibu maswali ya waandishi wa
habari, Bw. Nape alisema kuwa miongoni mwa ajenda zitakazozungumzwa ni pamoja
na utekelezaji wa ilani ya chama na mwenendo wa maendeleo pamoja na kuweka
mikakati thabiti ya maendeleo.
“Kikao kitakuwa kati ya mwe n y e k
i t i , wa b u n g e n a sekretarieti ambayo ndiyo wamiliki wa ilani
inayotekelezwa,” alisema.
Alisema
kuwa baada ya kikao hicho na wabunge hao, Kamati Kuu ya CCM itakutana tena Mei
20 na 21 ili kujadili mambo yatakayoongelewa katika kikao cha wabunge.
No comments:
Post a Comment