02 April 2013

Watoto 197 wazaliwa mkesha wa Pasaka Dar



Na Waandishi Wetu

WATOTO 197 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Pasaka, kwenye Hospitali ya Amana, Wilaya ya Ilala, Mnanyamala, Wilaya
ya Kinondoni pamoja na Temeke zote za Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Amana, Bi.
Agnes Temu, watoto 72 walizaliwa hospitalini hapo kati ya hao, wanaume 44, wanawake 28.

Alisema watoto saba wamezaliwa kwa upasuaji ambapo wazazi wawili wamejifungua watoto mapacha na wanendelea vizuri.

“Jana (juzi), tulipokea wajawazito 90 kutoka Wilaya za Ilala, Temeke na Kinondoni, ambao walikuja kujifungua,” alisema.

Naye Ofisa Muuguzi Kiongozi wa zamu katika Hospitali ya Mwananyamala, Bi. Erica Masawe, alisema watoto 56 walizaliwa hospitalini hapo katika mkesha wa Pasaka.

Alisema kati ya watoto hao, wanaume 26, wanawake 30 ambapo wazazi 15 walijifungua kwa upasuaji na hakuna mapacha.

“Watoto wote na wazazi wao wanaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa, waliobaki wanasubiri ruhusa,” alisema.

Katika Hospitali ya Temeke, Muuguzi wa zamu hospitalini hapo, Bw.Amos Kaberege, alisema watoto 64 walizaliwa kati yao 33 wanawake, wanaume 31.

Alisema wazazi wote wamejifungua salama bila kufanyiwa upasuaji na hali zoa zinaendelea vizuri pamoja na watoto wao.

Kwa upande wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Muuguzi wa zamu ambaye hakutaka kutaja jina lake akidai yeye si msemaji, alisema watoto watoto watano walizaliwa hospitalini hapo kati ya
hao wanaume watatu, wanawake wawili.

Imeandaliwa na Heri Shaaban, Jesca Kileo na Gladness Theonest.

No comments:

Post a Comment