02 April 2013

JK atembelea wajeruhi wa kifusi


Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, jana aliwatembelea majeruhi ambao waliangukiwa na kifusi cha ghorofa 16 ambalo liliporomoka
asubuhi ya Machi 26 mwaka huu, katiika Mtaa wa Indira
Ghandi, Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu 22.

Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambapo Rais Kikwete akiwa na mkewe mama Salma,
walitumia fursa hiyo kuwapa pole kwa majeraha waliyopata.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Bi. Hawa Ghasia.

Akiwa hospitalini hapo, Rais Kikwete ambaye pia aliongozana
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Bi. Hawa Ghasia, walimtembelea Mohamed
Ally Dhamji, Baqir Virani, Selemani Saidi na Yusuf Abdallah waliolazwa Taasisi ya Mifupa (MOI).

Majeruhi hao kwa mujibu wa daktari anayewatibu, alisema wanaendelea vizuri na kuongeza kuwa, kati ya marejuhi sita waliokuwa wamelazwa, wanne ndio waliobaki hospitali.

“Poleni sana kwa maumivu mliyoyapata, nawatakia mpate nafuu
ya haraka,” alisema Rais Kikwete akiwaeleza majeruhi hao.

No comments:

Post a Comment