02 April 2013

Watu wawili wanaosadikiwa majambazi wauawa Lushotoa a

Na Yusuph Mussa, Lushoto

WATU wawili wanaosadikiwa ni majambazi wameuawa na wananchi wenye hasira kali baada
ya kuwatuhumu kufanya vitendo vya ujambazi na uporaji wa mali za wananchi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana (Mach.30) Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Tanga Bw. Constantine Masawe alisema tukio hilo limetokea juzi saa 12 asubuhi kwenye
kijiji cha Ubiri kata ya Ubiri wilayani Lushoto.

Bw. Masawe aliwataja marehemu hao kuwa ni Bw. Simon Mswaki (32) mkazi wa Kitongoji
cha Vuli, Kijiji cha Ubiri wilayani Lushoto na Bw. Godfrey Changoma (35) mkazi wa
Kijiji cha Mshangai, Kata ya Mazinde wilayani Korogwe.

"Watu hao inaaminika ni majambazi, na walikutwa na vitu vya wizi kama deki na vitu
vya kuvunjia nyumba. Wananchi waliamua kuchukua sheria mikononi na kuwaua papo
 hapo kwa kuwakatakata miili yao" alisema Bw. Masawe.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi mmoja wa mashuhuda Bw.
Henry Lazaro alisema watu hao wamekuwa wakiiba mali za watu kama vile mbuzi na
wakati mwingine kuvamia majumbani na kuwajeruhi watu kisha kuchukua luninga na vitu
vingine.

"Hawa watu waliouawa hivi karibuni wamemjeruhi kwa kumkata vidole Mwenyekiti wa CCM
Kata ya Ubiri Bw. Rajab Shehoza, ambapo ilibidi apelekwe KCMC Moshi, lakini wanapita
wakiiba mifugo na vitu vingine.

"Kwenye hilo tukio la kuuawa walikuwa watatu, lakini mmoja akakimbia na kumjeruhi
mtu mmoja, wenzake miili yao imekatwa vipande vipande hadi walipotaja mtandao wao wa
ujambazi, ndipo walipopasuliwa vichwa vipande vinne kwa shoka" alisema Bw. Lazaro.

Bw. Lazaro amewashauri polisi kama wanataka kufanikiwa kuwakamata majambazi
wasitumie ubabe kwa wananchi, na wanatakiwa kuwauliza kwa upole, kwani hasira za
wananchi wa maeneo hayo zimekuja
 baada ya ndugu zao kutiwa kashikashi wakati walikuwa hawahusiki na ujambazi.

No comments:

Post a Comment