02 April 2013

Mamba aliyeua watu wawili auawa


Na. Jovither Kaijage,
Ukerewe  

MAMBA mmoja anayesadakiwa kuua watu wawili katika nyakati tofauti katika wilaya ya Ukerewe,Mwanza  ameuawa.

Kwamujibu wa taarifa toka eneo la tukio katika kijiji cha Muluseni kata ya Ngoma zinasema Mamba huyo mwenye uzito wa kilo 300 na urefu wa futi 18 aliuawa juzi baada ya kunashwa na mtego wa ndoano.

Ofisa Mtendaji wa kata ya Ngoma, Hamis Ndaro  akithibitisha kuuawa Mamba huyo alisema zoezi la kuwatafuta na kuwaua Mamba wengine linaendelea baada ya kupata kibali cha idara ya wanya ma poli.

Alisema katika eneo la mwambao wa ziwa Victoria  la vijiji viwili vya Nantare na Muluseni linakadiwa kuwa na Mamba zaidi ya 10 na kuongeza kuwa wanyama hao hatari tayari wameua watu wawili katika eneo hilo.

Aliwataja waliouwa kuwa Veronica Leonard [15] aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Muluseni aliyeuawa siku tatu zilizopita wakati anaosha vyombo eneo la kitongoji cha Ilingo.

Mwanafunzi mwingine Pascal Abudalla (15) wa darasa la sita katika shule ya msingi Nantare  aliuawa na Mamba hapo Novemba 11 mwaka jana saa za jioni wakati akichota maji ya kumwagilia bustani  ya Nyanya.

Afisa wanyapoli wa wilaya ya Ukerewe,Israel  Musangi amethibitisha kutokea vifo vya watu hao na kuongeza kuwa tayari idara yake ikishilikiana na  ofisi ya kata ya Ngoma wameanza shughuli ya kuwasaka na kuwaua mamba hao ili kunusulu maisha  ya watu.

Akifafanua alisema wanalazimika kutumia njia za asili kuwanasa mamba hao kwa sababu sio kazi raisi kubaini maficho yao na kutaka wakazi wa eneo hilo
kuepuka kwenda kando ya ziwa katika eneo hasa kuoga na shuguri nyigine ili kuepuka madhala ya wanyama hao. 

No comments:

Post a Comment