02 April 2013

Wananchi wamtimua mwe nyekiti wao wa kijiji


Na Thomas Kiani 
Singida

WANANCHI 3,700 WA Kijiji cha Mpugizi Kata ya Mwaru Wilayani Ikungi mkoani Singida kwa pamoja wamemtimua Mwenyekiti wa Kijiji na Mtendaji wake na kugoma kuendelea kutoa michango ya ujenzi wa Zahanati na choo cha shule ya msingi wakidai
viongozi hao kula fedha za michango vyanzo vya mapato. 

Wakizungumza na Gazeti hili juzi kijijini
hapo katika Mkutano wa ndani wa kijiji hicho wajumbe wa Serikali ya kijiji hicho walisema walifikia uamuzi huo wa kumuondoa Mwenyekiti Sendama Banku baada ya kuona kazi zote za ujenzi zimesimam, hazifanyiki na fedha zake hazipo hata,
hivyo wamedai Mtendaji wao wa kijiji hapatikani tangu mwezi Disemba mwaka jana.

Wajumbe hao walienda mbali zaidi wakidai Banku aliendesha kijiji katika misingi ya kikabila licha ya ubadhirifu wa fedha za kijiji wakiwa na Mtendaji wa wake Haji.

Walisema kuwa viongozi hao walikuwa hawasomi mapato
na matumizi ya kijiji, hivyo hakuna mabadiliko ya maendeleo katika kijiji tangu viongozi hao wawepo madarakani.

Wameendelea kusema katika Mkutano mkuu wa kijiji  mwaka uliopita Novemba 2, 2012 wananchi kwa pamoja waliamua kumuondoa kabisa Sendama Banku kwenye madaraka ya uongozi kama Mwenyekiti na nafasi yake kuchukuliwa na Jaffari Mpinga hata,na kumuweka mtendaji Kingu njia panda. 

Wajumbe hao waliendelea kusema kwa miaka mingi tangu kijiji hicho kianzishwe hakuna huduma za afya hadi Mwaru umbali wa kilomita 11 hivyo ni vigumu kwa akina mama wajawazito, watoto na wazee kupata huduma za afya ipasavyo.

Mkazi wa Kijiji hicho Hamisi Ng’eni alisema tangu wachimbe msingi wa Zahanati mwaka uliopita mpaka sasa hakuna kinachoenelea michanga na kokoto zimeanza kuibiwa na choo cha shule hakijafunikwa na wanafunzi wanapata taabu.

Serikali ilitoa ramani ya ujenzi wa zahanati na kijiji ikailipia wananchi na wakafyatua matofali  na kuchimba msingi,lakini kazi zote zimesimama kwa sababu hakuna fedha,"alisema.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mwaru Edward Mtau amethibitisha kuwepo kwa malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Mpugizi kwamba hawawataki viongozi wa kijiji chao wakidaiwa kukwamisha maendeleo yao yakiwapo ulaji wa fedha za michango ya zahanati na choo cha shule pamoja na fedha za kijiji kutoka vyanzo vyake vya mapato na zaidi
wananchi hao hawana huduma za afya.

Diwani wa Kata ya Mwaru Bw. Hassani
Kamugisha amewataka viongozi wa sasa na wananchi wa kijiji hicho cha Mpugizi kuendelea kujiwekea mikakati ya maendeleo kwa manufaa yao na kusimamia vizuri changamoto zinazojitokeza ili kufikia malengo yao waliojiwekea.

 

No comments:

Post a Comment