02 April 2013

Padri asoma waraka wa onyo kwa serikali


Na Steven Augustino, Tunduru

JUKWAAA la Wakristo nchini (TCF), limesema kama Serikali itashindwa kuchukua hatua za kuwalinda wananchi wake, kanisa litachukua hatua ya kuwaeleza waumini wake kwa uwazi kuwa Serikali iliyopo madarakani inaibeba dini moja.


Katibu wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Padri Dominiki Mkapa, aliyasema hayo wakati akiwasomea waumini wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba mjini huo, waraka uliotolewa hivi karibuni
na TCF kwa Serikali ambao umesambazwa katika makanisa.

Alisema tamko hilo limeyataka makanisa kutafakari upya
uhusiano wake na Serikali ambayo waraka huo ulidai imeshindwa kuchukua hatua dhidi ya watu wanaotumia kivuli cha dini kufanya vitendo vya mauaji kwa viongozi wa dini nyingine, kuvuluga amani na utulivu wa nchi.

Awali Askofu wa Jimbo Kuu la Tunduru na Masasi, Mhashamu Castory Msemwa, aliwataka wazazi kuwasaidia wachungaji katika malezi ya watoto wao ili kuhakikisha wanalinda maadili.

Askofu Msemwa ambaye alikuwa akitoa mahubiri kwenye ibada
ya Pasaka juzi, alisema watoto wasipolelewa na kupewa elimu ya kutosho katika maadili na misingi mikuu ya imani ya dini, kuna hatari ya kuingia kwenye makundi yasiyofaa.

Aliwataka waumini kusimamia imani yao kikamilifu, kutowaogopa wauaji wanaotishia imani za wengine na kudai wanachoweza kukitoa ni uhai lakini roho roho itabaki hai.

1 comment:

  1. Duh huyu padri bandia, haya siyo mafunzo ya bwana yesu, tukifuata mafunzo ya maisha ya mwana yesu huwezi kua na padri wa aina hii, imani itawale mioyo yetu, tuwe na mioyo ya msamaha, tupende binaadamu hata kama ni adui yako

    ReplyDelete