02 April 2013

Milioni 30 kutumika kuje nga mazalia ya samaki


Na Mwajuma Juma,
Zanzibar

JUMLA ya shilingi milioni 30 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kutengeneza Matumbawe (mazalia ya samaki ya kienyeji) katika ghuba ya chwaka huko kijiji cha Marumbi wilaya ya kati Unguja.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bw. Mussa Aboud Jumbe amesema kuwa wameamua kutengeneza Matumbawe hayo na kuyatupa katika bahari hiyo kutokana na kuwepo kwa uharibifu mkubwa unaosababishwa na uvuvi haramu ambao umesababisha kupungua kwa samaki katika vijiji hivyo.

Hata hivyo alisema kuwa mpango huo utawezesha kupunguza mgogoro uliopo baina ya vijiji viwili hiyvo kati ya Chwaka na Marumbi katika suala zima la
upatikanaji wa samaki,kutokana na kuwa kutakuwa na samaki wa kutosha ndani ya eneo hilo.

“Eneo la marumbi ni sehemu moja wapo lililoharibiwa na wavuvi wanaotumia uvuvi haramu ,hali iliosababisha ukame wa upatikanaji samaki katika kijiji hicho na hata vijiji jirani, hivyo hatua hii itaweza kusaidia kuondosha
upungufu huo”, alisema.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuwa kutoka na  athari kubwa iliojitokeza wameamua kuendesha mrdi huo kwa majaribio ambao unalengo la kuengeza nyumba za samaki pamoja na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa samaki katika eneo
hilo.

Alisema kuwa mbali na malengo hayo pia faida yake kubwa ni kuweza kudhibiti uvuvi haramu katika maeneo hayo.Sambamba na hilo amesema kuwa kuna haja ya Serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza fedha zaidi ili kuweza kuwanusuru wavuvi wa Zanzibar.

Kwa upande wao wenyeviti wa kamati za uvuvi kutoka vijiji vya uroa,pongwe na Chwaka walisema kuwa wakati zoezi hilo likiendelea tayari mafanikio
yameanza kujitokeza baada ya kuona samaki wageni wakiingia katika matumbawe
hayo.




No comments:

Post a Comment