05 April 2013

Mchungaji, Diwani wajisalimisha polisi vurugu za Tunduma



Na Rashid Mkwinda, Mbeya

DIWANI wa Kata ya Tunduma Bw. Frank Mwakajoka (CHADEMA), na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), mjini Tunduma, mkoani Mbeya, Gidioni Mwamafupa, wamejisalimisha kwa Jeshi la Polisi mkoani humo
kutokana na vurugu kubwa zilizotokea jana mjini humo.


Vurugu hizo zilichangiwa na mgogoro wa nani mwenye haki ya kuchinja ambapo jeshi hilo lilitoa tamko la kuwasaka viongozi
hao wakihusishwa na vurugu hizo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Diwani Athumani, alisema
Bw. Mwakajoka na Mchungaji Mwamafupa, wanahojiwa na
polisi kutokana na taarifa za kiintelijensia juu ya kuhusika kwao.

Alisema vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa mali na majeruhi ambapo watu 94, walikamatwa na kufikishwa polisi ambapo baada ya mahojiano, watu 45 walijidhamini kutokana na jeshi hilo kujiridhisha na udhamini wao.

Aliongeza kuwa, watu 45 walifikishwa jana katika mahakama ya Wilaya ya Mbozi kwa tuhuma za kufanya vurugu, uharibifu wa
mali, kuvunja msikiti na kujeruhi ambapo kesi yao itatajwa tena
mahakama hapo Aprili 18 mwaka huu.

CHADEMA yatoa tamko

Muda mchache baada ya kukamatwa Bw. Mwakajoka akihusishwa na vurugu hizo, chama chake kimetoa tamko la kulitaja Jeshi la Polisi kutozihusisha vurugu hizo na mambo ya kisiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa CHADEMA mkoani humo, Bw. Boyd Mwabulambo, alisema kuwa jeshi hilo linataka kutumia fursa hiyo kuvuruga amani ya mji huo.

Alisema jeshi hilo halikupaswa kumshikilia Bw. Mwakajoka  kwani alikuwa miongoni mwa watu waliokuwemo katika Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo ambacho pia
kilimuhusisha Mkuu wa Mkoa, Bw. Abbas Kandoro.

Juzi mji wa Tunduma uliopo mpakani mwa Tanzania na Zambia, ulisimamisha shughuli zake za kiuchumi kwa siku nzima kutokana na kuibuka kwa vurugu za nani mwenye haki ya kuchinja.

Vurugu hizo zilisababisha kundi la watu kuingia barabarani, kuchoma moto matairi na kuzuia barabarani kwa mawe na
miti lakini vurugu hizo ziliweza kudhibitiwa na polisi.

14 comments:

  1. MBONA MBOWE KWENYE HOTUBA YAKE BUNGENI AMETAJA TU GEITA HUKO TUNDUMA AKAACHA AKILAUMU CCM KWA KUCHOCHEA UDINI ,MUANDISHI KIBANDA WALIZUNGUMZIA TU KUZUGA LAKINI WAO AKILINI MWAO NI MWANGOSI ILA MUUZA MAGAZETI MOROGORO MBONA SIKIPAUMBELE CHAO ,KAMANDA WA POLISI LIBERATUS BALOW NI SAWA NA SHETANI ,WAMETAJWA MAPADRI NA MASHEHE LAKINI HATA ANAYETAJA UNGEFANIKIWA KUMTAZAMA USONI NI UNAFIKI MKUBWA HAINGII AKILINI INAFIKIA JENGO DAR ES SALAAM LIMEANGUKA CHADEMA WAMENYAMAZA KIMYA JE WAO NI FREEMASON WAMEFURAHIA DAMU ZA WALIOKUFA??? ILA MUNGU HAMFICHI MNAFIKI SIMBA HATA AVAE NGOZI YA KONDOO YEYE NI SIMBA TU ,NYOKA NI NYOKA TU HATA AWE MPOLE VIPI HAWEZI KUWA MJUSI MUTAFICHA MAKUCHA KWA MAOMBI YA DINI ZOTE MUNGU ATACHAGUA RAIS WA TANZANIA WALA SI MALAYA AU KIBAKA

    ReplyDelete
  2. Kwanza nilipe pongezi jeshi la polisi mkoa wa mbeya kwa jitiada wanazozifanyika katika kuhakikisha wanaleta amani na utulivu wa nchi kimsingi wana mbeya tunapaswa kujua athali za migogoro hivyo tusipende kuwa watu wa mfano katika kuanzisha mogogoro ebu tujitaidi kutatua tofauti zetu kaia hali ya amani ningependa kuwashauri wana mbeya kama tutaendelea hivyo basi haya yunayoyaona katika nchi za wenzetu nasi tutakuwa mkoa wa kwanza kupata athali nalieleza hili kwa ujasili na uchungu mkubwa kwan nipo sehemu abayo nimekuwa nikishuhudia watu walivopoteza maisha familia na ali kwa sababu ya kuruhusu migogoro na hii hali tunayokwenda nayo ni vichocheo vya kuaka kuvuruga amani ya nchi hasa kwa watu wenye uchu wa madaraka jamani naitizama hiyo kichani kibichi na hali ya hewa mzuri mwisho wa siku itakuwa ni jangwa na tutalia mfano chokochoko za mafuta mipaka vingozi wetu wa mbeya wanapaswa walifanyie kazi kwa umakini sn nawaomba nimeguswa sn
    toka sudan

    ReplyDelete
  3. hivi ni vurugu za chama ama za kidini na kama ni za kidini CHADEMA inahusikaje na kama diwani kakamatwa yeye alikuwa anahamasisha kwa bendera ya chama au ? huyo kiongozi pia na raia mnaposema chama mnakosea kumbuka hata mwalimu akiwa chumbani na mke wake anabaki kuwa ni mawlimu na hata bahati mbaya akakorofishana na mkewe hawawezi kutumia jina la lake bali la cheo chake hivyo sioni tatizo juu ya hilo hilo ni suala la kidini chama kisiwekwe msipige kampeni kutumia mbinu chafu CCM!

    ReplyDelete
  4. Kushindwa kwa serikali kuweka sheria bayana Matokeo yake ni haya .hakuna nchi yeyote duniani inayosema mwislamu tu ndiye achinje, isipokuwa nchi zenye kurndeshwa na sheria za kiislamu tu. Tanzania haipo kwenye kifungu hicho,
    Hata nchi zilizoendrlra kuna macula pekee kola mtu anayajua yanayoiza chakula kinachoitwa kosha kwa wayshudi na maduka ya nyama yanayoiza nyama iliuochinjwa na waislamu kusudi waislmu wasiwe na wasi na nyama wanauonunua.
    Wanasheria wa Tanzania Badala ya kuweka na kufafanua sheria hii wake kimya na Iko tayari kuleta machaguko ya nchi wakiwatuhumu wakristo na CHADEMA.
    Hivi Wanasheria SETI wote ni waislamu?
    Mbona wakened kimya? Ni utovu wa Chana cha C C M na Wanasheria espionage kwenye uislamu na siasa chafu na raisi asiye na ngvu na dhaifu.
    Hatupo Uarabuni kwenye unyapala wa Namna hii.
    Na nyinyi polisi mnaokiuka sheria ya nchi hii mkijua nchi yetu haina dini hiyo sliyewaajili sijui Ni nani. Jenafuata sharia law?

    Hilo Ni chanzo cha matatizo yote haya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kajifunze kuandika kwanza. Huoni haya kuandika machokorooo

      Delete
    2. Yaani akili yako kama kichaa vile. Nadhani wewe ni miongoni mwa wasiopenda amani ya nchi hii.chama chako kinakudanganya. Usidhani nchi hii tutawapatia wenye uchu na madaraka kama chadema. Maana ni wanafiki wa waziwazi.Halafu, upende usipende, waislamu wataendelea kuchinja. Acha fikra potofu za Padri Slaa,hapendi amani huyo!

      Delete
    3. Kwani uongo! Chama kinachotaka nchi isitawalike. Wao watatawala vipi baada ya kuharibu watanzania hasa vijana kwa kuwapandikizia fikra za chuki na kuogopa maisha. Wao wasubiri uchaguzi ili ccm ing'oke kihalai sio kutaka watu wauane ili tu wafanikiwe kisiasa.

      Si kuna uchaguzi? wakataeni mafisadi wakati wa uchaguzi. Alafu chague hao watawa wenu. Future will tell

      Delete
  5. SIKU ZOTE USIPENDE KUPINGA KILA KITU WANACHOFIKILIA WENZAKO HAYO NI MAWAZO YAKE UWE MZALENDO USITUMIWE BILA KUJIJUA

    ReplyDelete
  6. polisi lazima wafanyekazi yao hawako kwenye udini wala uchama.kamata wote mnaoona wanaweza kuwasaidia ktk kazi yenu

    ReplyDelete
  7. kwa kuwasaidieni kanunueni kitabu kiitwacho "when victims become killers" usishabikie ccm kwenye uozo wala chadema kwenye uozo. tunachokishuhudia leo ni matokeo ya ombwe la uongozi wenye maono nchini. na kama ninyi ndio aina ya wananchi wa tanzania, nachelea kusema kesho mtakuwa ndo watu wa kwanza kubeba mawe. tuna matatizo makubwa na ya msingi nchini, mtu anayeyasema matatizo ili yatatuliwe ndiye anayefaa na si anayepulizia manukato kwenye uozo. watanzania zindukeni, huu si wakati wa kupewa kofia na elfu 50. fikrieni nchi ya wanenu.fikrini kwa vichwa vyenu msiwategemee kina nape, mtatiro, ruhuza na lisu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yes! hapa umesema. Wanasiasa wajanja sana. Mbona M4C haitangazi kiama Moshi,Boma, Same,Mnayara lakini ni Arusha, Lindi, Mtwara, Mwanza, Mbeya na kwingineko tu? Hata Dar hapaingiliki vizuri. Hapo utashika pabaya. Akina nanihii wana shughuli zao zitavurugika. Nataka zile ndizi zisuzike kwa vile wale wazee ni wanachama wa ccm. Msitutupie mabezo yenu sisi tulio vijijini. Tuna mziko wa kutosha kubeba. Sio zambi kufaa sare ya chama flani. Eti kwa vile sisi masikini tuzuiwe hata kuvaa sare ya ccm?

      Delete
  8. Ndugu zangu kama mtu akikosea kwanini asoshauliwe? Mnataka kusema kuwa ccm imefanya mazuri tu? Au Chadema wamefanya vizuri kila sehemu na tusposahau CUF? Nina imani pamoja nawachangiaji wengine tuwe na mawazo chanya katika kulikomboa taifa letu kwenye umasikini. Kipindi chanyuma kafu walikuwa wadini, leo ni chadema, je kesho? Ni mhimu tubadilike. Siku hizi hata benki unaulizwa wewe ni Omari au John ndipo upewe mkopo. Kaanzisha nani? Tujisahihishe pale tunapokosea na tusiwe radical hata kwenye mambo yasio na msingi.

    ReplyDelete
  9. Bado tuko mbali kifikra. Elimu yetu Tanzania imedorola sana. Nasoma hizi feed back, Tanzania kwa miaka hii kumi imeshuka kihadhi. Tumelea watu wanaojikurupusha huku na kule bila kuwa na majifuno, elimu safi ya kufikiri na kujikwamua. Tumeingia kwenye soko la ulimwengu bila kujikomboa kiakili, kiutendaji, tunataka kuchota pesa, kuwa na gari, nyumba nzuri bila kujua kwamba hata tukiwa na vitu hivyo bila elimu na utaalamu kikazi, kifikra ni bure. Tutaendesha pikipiki mikokoteni ya Wachina tukiwaachia mwanya kusomba madini, gesi, pembe za ndovu, na kuchukua kila ajira ya Tanzania tukibakia kukodoa macho na kupiga simu za makopo toka china.Nyenzo zote kuu za uchumi ambazo wewe mtanzania inabidi uzishike na kwa sababu huna elimu ifaayo, na utaendeshwa kinyapala mpaka ufe. Serikali yetu inashindwa kumkomboa kijana wa kiafrika kielimu, kifikra, na kimajivuno. Badala yake inawagubika kwa kuwapa vijisenti, vingua, vibarabara ambavyo hata ukiweza kusafirisha mazao bado serikali hiyohiyo inakuibia kimachomacho. Wote mliotoa kauli zisizo na msingi hapo juu tafadhali nendeni shule mkajisomeshe mjikomboe kifikra, kiutendaji na mjue haki zenu. Bado wengi melala. Na taifa lenye uwingi wa watu waliolala halitajitegemea kamwe.Na wasomi wanaopelekwa nje kwaupendeleo ambao hawana maslahi ya nchi usomi wao ni heaw.Ukiangalia nchi zote Duniani zilizoendelea wasomi ni ukombozi na watetezi wa haki kwa walikotokea. Kama unanunuliwa na pesa wewe si msomi. unaelimu hewa.

    ReplyDelete
  10. Ukiwa na akili timamu kama Mtanzania hutatetea chama chogote kinachopotosha Watanzania. Lakini sitasita kusema Chama chetu Tawala ni kianzio cha matatizo mengi nchini.Kwa wale wanaotetea bila kujali maslahi ta Watanzania wote, Usalama wa watanzania wote, uhuru wa kufikiri, kutenda, kuadudu nakujiexpress bila vitisho, matokeo yake ndo haya yanayoibuka kila siku. Ajenda nyingi za Chadema zinalengo la maendeleo kwa wote. Lakini kuna watu ndani ya Chadema hasa vijana pia hawana maadili. Lakini kwa Ujumla CCM imetupeleka mahali pabaya kihistoria katika nchi hii inatia Aibu, na fedheha kubwa duniani. Wanaofurahia huu uongozi wa CCM ni wale walikwenye mitandao yao, maghaidi, mabeberu walioingia chini kwa nguvu na kasi kubwa kwa kipindi kifupi, na watu wanoataka kuibomoa zaidi nchi hii.

    ReplyDelete