05 April 2013

Mbatia ahofia vita ya udini nchini *Shekhe ataka Wakristo, Waislamu kujadili mgogoro wa kuchinja


Darlin Said na Kassim Mahege

MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), Bw.
James Mbatia, amesema Tanzania ipo hatarini kuingia kwenye
vita ya kidini kama hatua za haraka kudhibiti mifarakano ya
kiimani, inayotokea hazijachukuliwa.

Bw. Mbatia aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati mgogoro unaoendelea nchini kati ya Waislamu na Wakristo juu ya nani mwenye haki ya kuchinja.

Alisema kutokana na mifarakano inayoendelea, TCD inatarajia kukutana na viongozi wa dini zote, Serikali ili kukaa pamoja kuzungumzia suala la amani ya nchi.

“Viongozi hao watakutana kuanzia Aprili 23 hadi 24 ambapo kikao hicho pia kitahusisha watu mashuhuri nchini,” alisema Bw. Mbatia na kuongeza kuwa, kwa hali ilivyo sasa nchi inaweza kupoteza sifa ya kuwa kisiwa cha amani.

“Miaka yote tumeishi kwa amani na utulivu, mataifa ya nje yanaifahamu Tanzania kama kisiwa cha amani na kupata sifa
nyingi za kuwaunganisha Waafrika,” alisema.

Aliwaomba Watanzania kutochezea amani iliyopo badala yake kila mmoja atumie muda wake kuzungumza maendeleo na kuepuka mifarakano isiyo na tija inayoweza kuwagawa wananchi.

Bw. Mbatia alisema mifarakano hiyo haina tija kwa Taifa, tusikubali 
kuona mama yetu Tanzania aliyezaa watoto milioni 46 tukimpoteza biola sababu za msingi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, amewataka viongozi dini hizo kukaa pamoja ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Alhad Salum, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na gazeti hili na kusisitiza kuwa, amani ni jambo
la msingi hivyo kila Mtanzania anapaswa kulinda kwa gharama
yoyote ili kuchochea maendeleo ya sekta mbalimbali.

Aliwaomba viongozi wa dini ya Kikristo, kuacha kusambaza
waraka unahamasisha waumini wao kudai haki ya kuchinja
badala yake wasubiri kikao cha pamoja ili kupata ufumbuzi.

“Waraka wa Wakristo kudai haki ya kuchinja umeenezwa nchi
nzima hivyo nawaomba viongozi wenzangu wawe na subira ili tuweze kukutana na kumaliza mgogoro uliopo,” alisema.

Aliongeza kuwa, katika kipindi hiki Waislamu wanapaswa kuwa watulivu, kuwasikiliza viongozi na kuzingatia wanayoambiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Farijika, Padri Baptiste Mapunda, alisema suala la kuchinja ni haki ya kila mtu kutokana na maandiko matakatifu yanavyosema.

Alisema Serikali inatakiwa kutoa tamko kuhusu suala hilo na kuongeza kuwa, kila mtu ana uhuru wa kuabudu ili kuepusha
kuepusha migogoro isiyo na tija.

5 comments:

  1. Mheshimiwa Lipumba alitoa ushauri kama mtu mwenye mapenzina nchi yake akimtaka Rais akutane na viongoz wa dini ...lakini ikachukuliwa kama siasa ......Rais akahutubia tukategemea atatoa tamko la kuweza kusuluwisha hii migogoro mapema ....lakin vichwa vya habari vya magazeti vimeendelea kutoa taarifa kuhusu hii mada kama vichwa vikubwa vya habari....tuzibe ufa mapema watanzania hatuamini kuwa tunauadui wa kidini kiasi hiki

    ReplyDelete
  2. hapo nyuma wakristo hawakujua kama kuchinja kwa waislam ni ibada ,
    lakini sasa wamefahamu kuwa walikuwa wanaingizwa katika ibada zisizo katika imani yao,ndiyo maana sasa liwe huru kwa watu wa imani zote ili amani iwepo.
    pius

    ReplyDelete
  3. kwani waislamu wakila nyama iliyochinjwa na wakristo wanapata aleji gani si watu kama wao tu shida ni nini. lakini kwa kuwa wao wamesema kuchinja kwao ni ibada wasitulazimishe kwenda sikitini wakati sisi tumekulia kanisani

    ReplyDelete
  4. Lakini tatizo liko wapi kwetu sisi watanzania? Imani zetu za jadi tumeziacha,sasa twagombana na imani za kigeni.Tuachane na hayo,tuijenge nchi yetu.Nyama ni Nyama,aijalishi kachinja nani.Hata hivyo, kitu cha msingi tujiulize kwamba;ukristo wangu (JAPHET NALLY) Unamadhara gani kwake (HAMIS)? Tuachane na hayo TZ.

    ReplyDelete