02 April 2013

Kikwete awataka Waislamu, Wakristo wabadilike

Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete amesema, kama viongozi na waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu hawatakubali kubadili muelekeo wao, nchi itaelekea kubaya na kupoteza sifa ya kuwa kisiwa chama amani.

Alisema nyaraka na kauli kali kali zinazotolewa na viongozi wa
dini za Kikristo na Kiislamu, zinamshawishi kuamini mambo
makuu mawili.

“Tanzania ni nchi nzuri lakini tutaivuruga, sifa tuliyonayo ya kisiwa cha amani itapotea na kuingia katika orodha ya nchi zenye migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe,” alisema.

Alisema kwanza kila upande unatuhumu, kushutumu na kulaumu upande mwingine kwa kufanya vitendo viovu dhidi ya dini yake ambapo mihadhara ya kudhalilisha dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu, kuchoma moto nyumba za ibada, mzozo wa nani
mwenye haki ya kuchinja na kuuawa kwa viongozi wa dini
ni baadhi ya mambo yanayotolewa mifano.

Pili kila upande unailamu Serikali kwa kupendelea upande mwingine Wakristo wakidai mihadhara ya kudhalilisha Ukristo inaendeshwa na Serikali haichukui hatua.

Alisema Wakristo wanadai kuteswa na viongozi wao kuuawa na Waislamu, lakini Serikali haichukui hatua, imeshindwa kuwalinda raia wake na kupendelea Waislamu. 

Aliongeza kuwa, Waislamu nao wanadai kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo bila Serikali kuchukui hatua.

Wanadai kunyanyaswa katika nchi yao,  kukamatwa hovyo, kutopewa fursa sawa na kwamba Serikali inawapendelea
Wakristo na nchi ikuendeshwa kwa mfumo wa Kikristo.

“Mimi binafsi wananishutumu na kudai napendelea kushiriki zaidi kwenye shughuli za Wakristo kuliko za Waislamu kama harambee za kujenga makanisa na shule za makanisa. 

“Naambiwa mimi ni mwepesi wa kushiriki maziko ya Maaskofu kuliko Mashekhe wanapofariki...ipo Misikiti mitatu Dar es Salaam wamenisomea itikafu nife. 

“Katika itikafu hiyo, wamewajumuisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,” alisema.

Alisema yeye na Serikali anayoiongoza hawapendelei upande wowote na hatwafurahishwi na kitendo cha mtu kudhalilisha dini
ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri wa dini ya Kiislamu na wahubiri wa dini ya Kikristo wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa nyakati mbalimbali.

Vyombo vya usalama vinatambua wajibu wake kama haifanyiki ni ulegevu wa mtu katika kutimiza wajibu wao hivyo si sera wala maelekezo yake au ya Serikali. 

Rais Kikwete alisema Serikali yetu haijashindwa kulinda usalama wa raia wake au viongozi wa dini na nyumba za ibada na kama ingeshindwa, Taifa lingeshuhudia ongezeko la mauaji ya raia, viongozi wa dini na matukio ya kuchomwa nyumba za ibada.

“Nawasihi sana ndugu zangu Wakristo na Waislamu, tusiyachakulie matukio ya kuuawa kwa Mchungaji Mathayo Kachila kule Buseresere, Geita, na Padri Evaristus Mushi kule Zanzibar, au kumwagiwa tindikali Shekhe Fadhili Soroga ambaye ni Naibu Mufti wa Zanizbar, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda na kuchomwa moto kwa Makanisa Zanzibar na Mbagala, Dar es Salaam kuwa ni kielelezo na ushahidi wa Serikali kushindwa kutimiza wajibu wake.

Alisema kila tukio lina mazingira yake na hakuna ushahidi wa vyombo vya Serikali kuzembea au matukio hayo kuunganika ambapo hadi sasa, hakuna ushahidi wa kuwepo kikundi cha Waislamu wanaopanga kuua viongozi wa Kikristo na
kuchoma moto makanisa yaliyopo nchini.

“Watanzania wenzangu nawaomba mtanabahi na mjue kuwa, wapo watu wanaocheza mchezo mchafu wa kuwagonganisha na kutaka kuwagombanisha Wakristo na Waislamu kwa sababu wanazozijua wao kwa faida yao,” alisema Rais Kikwete.

Kuanguka ghorofa

Rais Kikwete alisema, tukio la kuporomoka kwa ghorofa 16, katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kuua watu 34 na wengine 17 kujeruhiwa, limemuhuzunisha na kuziagiza malmaka husika, kuwachukulia hatua wote waliosbabaisha maafa hayo.

Alisema wahusika hao washtakiwe mahakamani na kufutiwa leseni za kufanya shughuli za ujenzi, taaluma zao na kuzitaka mamlaka zinazohusika na usimamizi wa majengo kutimiza wajibu wake.

Rais Kikwete aliyasema hayo katika hotuba yake ya kila mwisho mwa mwezi na kuongeza kuwa, kama mamlaka hizo zingetimiza wajibu wake ipasavyo, tukio hilo lingeepukika.

“Halmashauri za miji na Wilaya zina wajibu maalumu katika ujenzi kwenye maeneo yao, yaliyotokea Dar es Salaam yawe fundisho kwa wote...naamini Bodi ya Usajili wa Wakandarasi na Bodi ya Usajili wa Wahandisi, itakamilisha mapema uchunguzi wake ili ukweli uweze kujulikana,” alisema Rais Kikwete.

Aliongeza kuwa, Bodi ya Usajili wa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi na Baraza la Taifa la Ujenzi, nao washirikishwe kwa ukamilifu ili ukweli upatikane na hatua stahiki zichukuliwe. 

Uhusiano wa Wakristo na Waislamu

Rais Kikwete alisema, imefikia mahali ambapo kama viongozi na waumini wa dini hizo hawatakubali kubadili muelekeo wa sasa, nchi inaelekea kubaya na kupoteza sifa ya kuwa kisiwa chama amani.

“Tanzania ni nchi nzuri lakini tutaivuruga, sifa tuliyonayo ya kisiwa cha amani itapotea na kuingia katika orodha ya nchi zenye migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe,” alisema.

Alisema nyaraka na kauli kali kali zinazotolewa na viongozi wa
dini za Kikristo na Kiislamu, zinamshawishi kuamini kuwa, kauli zina mambo makuu mawili.

Kwanza kila upande unatuhumu, kushutumu na kulaumu upande mwingine kwa kufanya vitendo viovu dhidi ya dini yake ambapo mihadhara ya kudhalilisha dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu, kuchoma moto nyumba za ibada, mzozo wa nani
mwenye haki ya kuchinja na kuuawa kwa viongozi wa dini
ni baadhi ya mambo yanayotolewa mifano.

Pili kila upande unailamu Serikali kwa kupendelea upande mwingine Wakristo wakidai mihadhara ya kudhalilisha Ukristo inaendeshwa na Serikali haichukui hatua.

Alisema pia Wakristo wanadai kuteswa na viongozi wao kuuawa na Waislamu, lakini Serikali haichukui hatua, imeshindwa kuwalinda raia wake na kupendelea Waislamu. 

Aliongeza kuwa, Waislamu nao wanadai kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo bila Serikali kuchukui hatua.

Wanadai kunyanyaswa katika nchi yao,  kukamatwa hovyo, kutopewa fursa sawa na kwamba Serikali inawapendelea
Wakristo na nchi ikuendeshwa kwa mfumo wa Kikristo.

“Mimi binafsi wananishutumu na kudai napendelea kushiriki zaidi kwenye shughuli za Wakristo kuliko za Waislamu kama harambee za kujenga makanisa na shule za makanisa. 

“Naambiwa mimi ni mwepesi wa kushiriki maziko ya Maaskofu kuliko Mashekhe wanapofariki...ipo Misikiti mitatu Dar es Salaam wamenisomea itikafu nife. 

“Katika itikafu hiyo, wamewajumuisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,” alisema.

Alisema yeye na Serikali anayoiongoza hawapendelei upande wowote na hatwafurahishwi na kitendo cha mtu kudhalilisha dini
ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri wa dini ya Kiislamu na wahubiri wa dini ya Kikristo wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa nyakati mbalimbali.

Vyombo vya usalama vinatambua wajibu wake kama haifanyiki ni ulegevu wa mtu katika kutimiza wajibu wao hivyo si sera wala maelekezo yake au ya Serikali. 

Rais Kikwete alisema Serikali yetu haijashindwa kulinda usalama wa raia wake au viongozi wa dini na nyumba za ibada na kama ingeshindwa, Taifa lingeshuhudia ongezeko la mauaji ya raia, viongozi wa dini na matukio ya kuchomwa nyumba za ibada.

“Nawasihi sana ndugu zangu Wakristo na Waislamu, tusiyachakulie matukio ya kuuawa kwa Mchungaji Mathayo Kachila kule Buseresere, Geita, na Padri Evaristus Mushi kule Zanzibar, au kumwagiwa tindikali Shekhe Fadhili Soroga ambaye ni Naibu Mufti wa Zanizbar, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda na kuchomwa moto kwa Makanisa Zanzibar na Mbagala, Dar es Salaam kuwa ni kielelezo na ushahidi wa Serikali kushindwa kutimiza wajibu wake.

Alisema kila tukio lina mazingira yake na hakuna ushahidi wa vyombo vya Serikali kuzembea au matukio hayo kuunganika ambapo hadi sasa, hakuna ushahidi wa kuwepo kikundi cha Waislamu wanaopanga kuua viongozi wa Kikristo na
kuchoma moto makanisa yaliyopo nchini.

“Watanzania wenzangu nawaomba mtanabahi na mjue kuwa, wapo watu wanaocheza mchezo mchafu wa kuwagonganisha na kutaka kuwagombanisha Wakristo na Waislamu kwa sababu wanazozijua wao kwa faida yao,” alisema Rais Kikwete.

7 comments:

 1. Mheshimiwa Rais wetu, tafadhali usitumie usemi eti "wakristo, waislamu wabadilike". Tafadhali sisi wakristo sio watoto wadogo wa kudanganywa kama wehu. Kauli sahihi ingekuwa " ndugu zangu waislamu tubadilike"
  Tumeishafanya utafiti toka awamu ya pili ya utawala, anaposhika madaraka Rais muislamu basi mambo yote huwa shida. Kumbuka enzi ya utawala wa Mwinyi, mambo yalikuwaje. Alipokuja Mkapa alijitahidi na kufanakiwa kuuondoa udini uliokuwa unaota mizizi kabisa.
  Sasa umekuja ndugu yetu, mambo ya udini yamerudi kwa kasi ya ajabu
  Ebu fikiria tu endapo Wakristo wangejifanya kulipiza kisasi angalau kwa kuchoma moto msikiti hata ule ulioezekwa kwa nyasi mambo yangekuwaje?
  Washauri waumini wenzako wawe wastaarabu, waache mambo ya kitoto.

  ReplyDelete
 2. Watu kama nyie kina Jackline James ndo tatizo. Unataka kutuambia wakristo wao hawafanyi kosa? Aliyekojolea msahafu ni mwislamu? Hata kama ni mtoto si amefuata mafundisho anayopata kanisani? Mbona watoto wakristo walikuwepo tu toka enzi na kamwe hawakufikiria kutenda kitendo kile? Walikuwa wanapata mafunzo mazuri kanisani. Sasa makanisa yamekuwa biashara, hata wasio waadilifu wanakuwa na kanisa! Lazima Raisi awaonye pande zote kwa wooote wapo miongoni mwao watu waovu. Hii akili ya kufukiri ni upande wa pili tu ndo wanakosea eti upande wako uko sawa ndio tatizo lenu nyie wakristo hafifu!. Umezungumza kuhusu mkapa umesahau ndiye wakati wake waislamu waliuawa kule Pemba na wengine ni wakimbizi hadi leo? Huu mtazamo wenu wa kudharau maraisi waislamu nao ni tatizo. Nchi hii kama alivyosema Kikwete itaharabika kama watu kama nyie hamtaacha mitizamo yenu potofu. Wote wakemewe, waislamu na wakristo kwani miongoni mwao kuna watu wasioitakia nchi hii mema.

  ReplyDelete
 3. MMMMMMMMMMMMH KAZI IPO

  ReplyDelete
 4. Mheshimwa Rais amenena maneno ya hekima sana.Mimi ni mkristo na ninashirikiana vizuri zaidi na waislamu mahali nilipo.Wakristo wenzangu wamejaa ubaguzi wa " Mimi nimeokoka zaidi ya yako, mimi ninanena kwa lugha ni bora, sijui kanisa lako halina wokove, mara hauna Roho mtakatifu nk" Kama ni hivyo kwa wakristo wenzao je itakuwaje kwa wenzetu wa dini ya kiislamu si ndio wanawadharau kabisa na kuwatukana? Uozo aliousemea Mheshiwa Rais umeota mizizi pande zote.Kama Ukristo ni mmoja imekuwaje siku hizi makanisa yanaibuka kama uyoga na kuwaghiribu watu kuwaibia hata mali zao kwa kisingizio cha kuwapatia baraka za kutajirika na kuwaondolea matatizo wangali wanaendelea kuwa na matatizo.Sisi Wakristo tuonyeshe mfano mwema hata kwa kauli zetu, tunajitia tunasamehe waliochoma makanisa huku tunanung'unika na kulaumu serikali, huo ukristo gani?nakumbuka Mtumishi Christopher alitufundisha semina moja namna ya kusamehe na kusahau.Hilo muhimu siyo kujitia mafuta usoni huku moyoni umejitia matope.Natamani sana sisi wakristo tuonyeshe mfano mwema wa kupendana na kuheshimiana katika uchaji wa roho na utakatifu wa Kimungu siyo maigizo tunayofanya sasa makanisani mwetu.Sasa hivi wakristo wa sharika za kilutheri jiji Dar wameanza kuiga mambo ya makanisa yanayojiita ya kiroho ili eti wasipoteze waumini wao.Je, mtaiga mangapi?Badala ya kuwafundisha watu wamjue Mungu walijue neno lake ili wasimame imara katika imani zao tumeanza kupandikiza roho ya kuiga kuabudu na kusifu kwa unafiki mkubwa. Kumbuka Mungu Hadhihakiki hata kidogo.Mheshimiwa Rais Mungu akubariki kwa uongozi wako na jinsi ulivyo na upendo na huruma kwa watu wote unaowaongoza pasipo ubaguzi.

  ReplyDelete
 5. Napenda kumshukuru mheshimiwa Raisi kwa matamshi yake kwa dini zote mbili.

  Kusema kweli vurugu za imani zikisha anza hakuna atakaye sema ameshinda kwani kitakachotokea ni mauaji na machafuko tu

  Tujifunze kwa wenzetu wa Israeli na Palestina ni mzozo wa kidini waislamu na wakristo kila mmoja anasema ana haki lakini tunaweza kuona adhari zake ni nini , mauaji . uharibifu wa mali nk

  Tanzania imekuwa kisiwa cha amani kwa muda mrefu na amani hiyo imetafutwa kwa shida na waasisi wa Taifa letu akiwemo marehemu Julius Kambarage Nyerere na Raisi wa Zanzibar Amani Karume

  Tusisahau kwamba mmoja alikuwa mkristo na mwingine alikuwa mwislamu, waliweka pembeni itikadi zao za udini na kuunganisha nchi , shule zikajengwa wanafunzi wakasomeshwa bila kufuata misingi ya dini, serekali ikasimamia elimu mwanafunzi wa Mtwara wakapangwa kusoma boding Mwanza wa Kigoma wakasoma Dar au Zanzibar au Pemba au Tangaili hali kuwachanganya na kuleta taifa lenye uelewano mzuri na amani tele

  Walipomaliza shule waislamu na wakristo walioanza uchumba shuleni wakaoana, lugha na tabia zikawa moja za utaifa la watanzania udini ukawekwa pembeni waslamu wakawa wakristo, wakristo wakawa waislamu

  Hali imeanza kubadilika tangu waasisi hao walipoondoka bajeti ya elimu ikafinywa hakuna tena waranti za kusafiria shule za kata zikaanzishwa za wakristo pekee na waislamu pekee, vyuo vikuu navyo vikaanza kwa mwelekeo huo huo, chuo kikuu cha waislamu wapi sijui mfumo ukaanza kuwa tofauti,

  Utawala wa mheshimiwa Raisi Mwinyi ukaliona hilo Mzee Mwinyi akatoa ruksa anayetaka kula nguruwe sawa na anayetaka kula chura sawa . mgawanyiko ukaanza kutokea waislamu nao wakaona kama wanaonewa wakristo nao wakaona kama wananyanganywa haki yao

  Mambo yameendelea sasa mauaji yanaanza upendo uliokuwepo wakati wa enzi ya Nyerere unatoweka watu sasa wanaanza kuogopa hata kusema dini zao wanaweka ulinzi makanisani kama ilivyokuwa kwenye kanisa la Mt Joseph Dar kama yalivyo mataifa yenye migogoro mikubwa ya kidini kati ya waislamu na wakristo mfano huko Naigeria, Sudani nk

  Kweli hatutafika kama hatutabadilika kama hatutakumbuka kuwa sisi tangu awali ni kisima cha Amani na mataifa mengi yamepata amani kupitia kwetu kama Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Boswana, South Africa kwa Mzee Mandela Sudani Uganda nk
  Ole wetu kwani tutaanza kuwa kama huko Naigeria na Sudani

  Watanzania tusiipoteze amani yetu kwa ajili ya ubinafsi wetu, dini ni kibao tu cha kuwaelekeza waumini wake kwenda mbinguni , kibao hicho hakiondoki mahali hapo ila mwanadamu ndiye anefikia mwisho na kufa , dini haitamfikisha mtu mbinguni , ukitaka kwenda mbinguni tafuta njia ya kweli siyo dini ni Imani na uamini kweli kweli.

  Mheshimiwa Raisi Kikwete yeye ni baba wa wakristo na waislamu serikali haina dini na kama Raisi kigezo kikubwa hastahilli kubagua, ndio maana anakwenda kuzika kwa wakristo wakati yeye ni mwislamu , Raisi Mkapa pia na Nyerere walihudhuria sherehe na misiba mingi ya waislamu ni mababa hao mnataka baba abague watoto wake. Ndiyo maana tunamuenzi kuwa baba wa Taifa siyo wa wakristo bali na waislamu na wasio na dini pia

  Tujifunze hata kwa mataifa ya magharibi serikali zao hazichanganyi dini na siasa, angalia Marekani hata sikukuu ya pasaka hawaisherekei ni serikali, raisi anawatambua hata wale wanaofikiriwa wanafanya maovu kama wenye ndoa za jinsia moja ni baba kwanini asiwatambue ni sawa na wewe kuwa na mtoto asiyesikia ni mtoto wako tu

  Ndugu zangu waslamu na wakristo tupendane, hakuna amri kuu kuliko hii kumpenda Bwana Mungu wako kama nafsi yako na kumpenda ndugu yako kama nafsi yako
  Wakristo na waislamu tumekuwa ndugu wa damu kwa siku nyingi mimi ninayesema hapa watoto wa ndugu yangu karibu wote wameoa waislamu je nianz kuwachukia hao HAPANA

  Na tukirudi kwenye upendo tuliokuwa nao wa kuoana hakuna mkristo au mwislamu atakaye msema mwenzake vibaya.TUBADILIKE

  Mungu Ibariki Tanzania

  ReplyDelete
 6. Siku zote unachokipanda ndio utakachovuna.
  Kwa miaka mingi sasa tokea kuanzishwa siasa ya Vyama vingi Serikali ya CCM imekuwa ikipandikiza siasa za UDINI, UJIMBO, UKABILA na mengi mengineyo ili iweze kupata ushindi wa rahisi kwa kipindi fulani kumbe wamesahau kuwa fitna na sumu ile zitakuwepo kwenye damu za watu na kuja kuathiri.

  Kikwete na Chama chako cha CCM vuneni mlichokipanda na nyie ndio mtobeba jukumu wa hilo maana ndio mlioleta siasa za UDINI ili mtawale

  ReplyDelete
 7. Nafikiri tutumie muda tuliopewa Mwenyezi Mungu pamoja na akili tulizojaaliwa na hata tukaweza kusoma na kuandika,kutumia njia za kisasa za mawasiliano kujadili suluhu ya tatizo na sio kuendeleza mzozo wa mimi mkristo naonewa,mimi muislam naonewa.Jamii tufike mahali utamaduni wetu ulindwe na tujifunze kwa wenzetu kama Nigeria yalikotokea kama haya.Hayakuanza ghafla hapana,waliendekeza madogomadogo kama haya hadi wakafika walipofika.
  Wanadini,tujiulize,TUMEISHIJE MIAKA YOTE HII KWA UMOJA,AMANI NA UPENDO? MISAHAFU NA BIBLIA HAVIKUWAPO? MIFUGO ALICHINJA NANI?
  Tukiyapatia majibu sahihi maswali haya ni hakika tutarudi mahali tulipokuwa,tukitengana katika haya,ni dhahiri tutatengana na katika mengine yoote.
  HEBU NATUMHESHIMU MUNGU

  ReplyDelete