26 March 2013

Viongozi wa dini waombea mradi wa maji


Na Steven William, Muheza

VIONGOZI wa dini ya Kikristo na Kiislamu, katika Kijiji cha Lusanga, Wilaya Muheza, mkoani Tanga, wameshiriki katika
ibada ya kuombea mradi wa kisima kirefu cha maji ili ujenzi
wake uweze kukamilika haraka na kuwasaidia wananchi.


Kisima hicho kinajengwa katika eneo la Kitisa Estate ambapo maombi hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki yakiongozwa
na Shekhe Mkuu wa Msikiti wa kijiji hicho, Abdi Hamisi
Mdoe na Mchungaji wa Kanisa la Angilikana, Haidano Kamote.

Maombi hayo pia yalimshirikisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Bi.
Subira Mgalu, Mhandisi wa Maji wilayani humo, Patric Hansi
na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.

Bi. Mgalu aliwashukuru viongozi wa dini kwa kukiombea kisima hicho ili ujenzi wake ukamilike mapema na kupunguza tatizo la
maji ambalo linakwamisha maendeleo ya wananchi.

Alisema mradi huo hadi kukamilika kwake utaghalim sh. milioni 800, ambapo awamu ya kwanza fedha zilizotumika sh. milioni 229 hivyo wanasubiri fedha za ujenzi wa awamu ya pili.

“Nawaomba viongozi wa dini muwaombee viongozi wa nchi ili wapate nguvu za kuwatumikia wananchi na kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya maji,” alisema.

Aliongeza kuwa, mradi huo utawanufaisha wananchi wa Vijiji vya Mamboleo, Kitisa, Lusanga na Muheza Mjini ambapo kwa sasa Mfuko wa Jimbo uliopo chini ya mbunge wa jimbo hilo, Herbert Mntangi, umetoa fedha za kutandaza mabomba.

2 comments:

  1. kweli muheza ndipo kuna ushirikiano wa kidini muda mrefu sana, tangu karne ya 18 kwani ukristo ulianza hapo zamani sana kabla ya maeneo mengine (magila)na wasomi wa kwanza kabisa walitokea hapo na walikuwa ndio watawala (administrators)wa mwanzo katika serikali za kikoloni(wajerumani na waingereza)na wazungu waliwapenda kwa utendaji mzuri(good performances)na kidini wanashikamana sana hata koo zao ni pande wakristo na upande waisilam, ila taratibu zao hazinakuza uhusiano mf. baba mzazi akiwa mkristo alifariki baba zao wadogo hata kama ni waisilam wanawalea wale kama baba mlezi na kuwakuza huku wakiwa na imani zao tofauti, watsoma, wataolewa na kuoa kwa uangalizi mkubwa wa mlezi wao, wanaheshimiana sana wanatunzana sana, wanaupeo wa kiakili sana, ila shida kubwa inayosumbua ni imani ya kishirikina imerudisha sana maendeleo yao nyuma ikiwa, ingekuwa ni eneo lenye maendeleo makubwa sana barani afrika na si tanzania tuu, natumaini watajitahidi kurudisha hadhi yao ya zamani kama ilivyokuwa katika utawala wa ukoloni.

    ReplyDelete
  2. MBONA HUKO BAGAMOYO WALIKATAA KUSHIRIKI UZINDUZI WA KISIMA WAKITATA MAJI KUTOKA DAWASCO MUNGU ANGEFANYA MUUJIZA AHAMISHIE KISIMA HICHO LUSANGA ILA WAFADHILI WANAKATISHWA TAMAA INAPOFIKIA MADIWANI NA WABUNGE KUKOSA UADILIFU LIKO DARAJA AMBALO LILIZINDULIWA NA KUONYESHA KUGHARIMU MAMILIONI YA FEDHA WAKATI SI KWELI INGEKUWA VEMA AGREY MWANDRY WANGEZALIWA WENGI AZUKE AKATATHIMINI DARAJA LA MUHEZA KUELEKEA MASUGHURU IWAPO VALUE FOR MONEY NI SAWA

    ReplyDelete