ROME, Italia
KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I, jana amesimikwa rasmi kutumikia wadhifa huo na kutumia fursa hiyo kuwataka viongozi mbalimbali, kuwalinda wanyonge na masikini.
Papa Francis I, alitoa wito huo katika misa maalumu iliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma ambapo katika misa hiyo, alivalishwa pete ikiashiria sasa amekuwa Baba Mtakatifu wa 266.
Kwa mujibu wa Kituo cha Utangazaji cha CNN, Papa Francis I, alizunguka katika viwanja hivyo akiwa kwenye gari la wazi na baada ya kuteremka, aliwabariki mahujaji mbalimbali.
Hata hivyo, inakadiriwa zaidi ya watu milioni 1.6 waliudhuria sherehe hiyo huku mamilioni wakiifuatilia kupitia vyombo vya habari wakiwemo viongozi 130 kutoka duniani kote.
Papa huyo alichaguliwa na Mkutano wa Makadinali wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedict XVI aliyetangaza kujiuzulu wadhifa huo Februari 28, mwaka huu.
Papa Benedict XVI alikuwa papa wa kwanza kujiuzulu katika
miaka 600 ya historia ya kanisa hilo akidai umri wake wa miaka
85, asingeweza kutekeleza kikamilifu majukumu yake.
Katika hatua nyingine, Papa Francis I, anaonekana kuwa na mtazamo tofauti na watangulizi wake.
hili gazeti lenu si mfunge? siku sita hakuna kipya, amka ee mbongo!
ReplyDelete