28 February 2013

Uandikaji wosia mapema itasaidia kupunguza migogoro ya mirathi



Na Rose Itono

MITAZAMO hasi ya kudai mtu akiandika wosia ni kujitabiria kifo ni kichocheo kikubwa cha migogoro ya mirathi miongoni mwa jamii.


Baadhi ya watu wamejijengea hofu kuandika wosia wakati wakiwa hai kutokana na kuhisi ni njia ya kujitabiria kifo.

Migogoro ya mara kwa mara imekuwa ikijitokeza ndani ya jamii kutokana na kutokuwepo kwa utamaduni wa kuandika wosia tukiwa hai hasa pale linapotokea tatizo la kifo.

Nionavyo tabia ya kuandika wosia ukiwa hai na kwa kufuata taratibu zote zinazohitajika kutasaidia kwa kiasi kikubwa kumalizika kwa migogoro inayojitokeza mara kwa mara hasa kwa upande wa mirathi.

Nionavyo hali hii huwatesa zaidi wanawake hasa wanapofiwa na waume zao na kubaki wakihangaika na hatimaye kubaki masikini kwa mali zao kuchukuliwa na ndugu wa mume kinyume cha taratibu za kisheria.

Naamini tabia ya kuacha wosia ndiyo suluhisho kubwa katika jamii hii katika kupunguza migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mnara kwa mara pale inapotokea tatizo la kufiwa.

Nionavyo kuna haja ya wanajamii kuondokana na mitazamo hasi ya kudai kuwa mtu akiandika wosia ni sawa na kujitabiria kifo badala yake kila mtu ajijengee mazingira na utaratibu wa kuandika wosia ili kupunguza migogoro.

Nionavyo serikali ina kila sababu ya kuingilia suala hili kwa kutoa elimu kwa jamii kuanzia ngazi ya mtaa ili kuweza kumaliza matatizo yanayojitokeza mara kwa mara.

Nikiangalia ni wazi asilimia kubwa haina uelewa wa kutosha juu ya namna ya uandikaji wa wosia na kufanya jamii kushindwa kuona umuhimu wake.

Nionavyo serikali ikitoa elimu juu ya umuhimu wa kuandika wosia kabla ya kifo migogoro ya mara kwa mara hususan katika suala la mirathi itamalizika.

Sambamba na hilo elimu ya namna ya uandikaji wa wosia pia ni muhimu ili kuweza kufuata taratibu zote zinazokubalika.

Nionavyo suala la elimu kwa wazazi juu ya haki ya mtoto kupata mali za wazazi wao pale wanapofiwa bado ni tatizo ambalo huleta migogoro miongoni mwa jamii.

Elimu kwa wazazi juu ya haki za watoto katika maeneo mbalimbali kwani wazazi wengi hawafamau haki za watoto.

Wazazi wengi hawajui juu ya haki za watoto na pia hawatambui nafasi zao katika malezi hali ambayo imekuwa ikiwafanya kushindwa kuwatimizia watoto wao haki zao za kimsingi ikiwepo kupata elimu.

pamoja na haki ya mtoto katika kupata elimu pia watoto wana haki ya kurithi mali za wazazi wao pale wanapofariki.


No comments:

Post a Comment