07 February 2013

Twanga yamwandalia 'pati' LuizaNa Mwandishi Wetu

BENDI ya muziki wa dansi nchini, African Stars 'Twanga Pepeta' imepanga kumwandalia kiongozi wake, Luiza Mbuta, sherehe ya kuzaliwa kwake (birthday party), itakayofanyika Jumamosi katika Ukumbi wa Mango, Kinondoni.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Meneje wa bendi hiyo, Hassan Rehani, Luiza anafanyiwa sherehe hiyo ikiwa ni ya mara ya pili mfululizo na na Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) ambayo mwaka jana pia ilimwandalia.

"Ikumbukwe ASET, imeamua kumfanyia, Luiza sherehe hiyo kwa mara yapili mfululizo kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa katika bendi ya Twanga Pepeta kwa kwa muda mrefu bila kuhama.

"Na pia anaandaliwa pati hiyo kwa kufanya kazi kwa kujituma bila ya kuchoka, tangu alipoanza kazi rasmi ndani ya bendi mpaka leo," alisema Rehani.

Alisema sherehe hiyo ya kiongozi huyo, itanogeshwa na Twanga kama kawaida kwani wameandaa uhondo wa kutosha kwa mashabiki wao ambao nao wanakaribishwa kumpa hongera ya kuzaliwa Luiza.

Alisema kama kawaida bendi hiyo, imeandaa keki kwa ajili ya kumlisha Luiza, kama ilivyofanyika mwaka jana amabapo utaratibu maalumu umeandaliwa kwa marafiki na wadau wa bendi hiyo.


No comments:

Post a Comment