07 February 2013

Flaviana kutangaza Diesel na Edun



Na Mwandishi wetu

MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya kampuni za nguo ya Diesel na Edun.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Compass Communications Limited, Maria Sarungi amesema Flaviana ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007, anabaki kuwa mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika kushiriki kampeni za nguo hizo.

Kampeni hiyo inayoitwa Diesel+Edun, ilianzishwa Januari mwaka jana ambapo muanzilishi wa kampuni hiyo, Renzo Rosso na waanzalishi wa Kampuni ya Edun, Ali Hewson na Bono walikwenda nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Afrika.

Waanzilishi hao waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalumu, zitakazotokana na pamba za wakulima hao wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja.

Nguo hizo zinatangazwa kama kampeni, ili kunufaisha bara la Afrika.
Pia nguo hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa Machi, mwaka huu katika maduka mbalimbali nchini Marekani na duniani kote.

Pia nguo za Diesel+Edun, zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.


No comments:

Post a Comment