05 February 2013

Sumaye ataka shule za vipaji zisaidiwe



Na Queen Lema, Arusha

WAZIRI Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, amezitaka taasisi
na mashirika mbalimbali, kujenga tabia ya kusaidia, kuziendeleza shule za vipaji maalumu ambazo nyingi zimesahaulika.


Bw. Sumaye aliyasema hayo jana mkoani Arusha katika mahafali
ya 20 ya kidato cha sita, Shule ya Sekondari Ilboru na kusisitiza kuwa, taasisi na mashirika binafsi yana uwezo wa kuendeleza
shule hizo na kuzifanya ziwe na ubora mkubwa.

Alisema shule hizo zinakabiliwa na changamoto nyingi ingawa wadau kama hao wana nafasi ya kuzisaidia ili ziweze kuinua
viwango vya kitaaluma nchini.

“Kama wadau hawa watawekeza zaidi katika elimu na kutatua changamoto zilizopo, wasomi ndani ya Taifa hili wangekuwa
wengi...umefika wakati wadau waone umuhimu huu,” alisema.

Wakati huo huo, Mkuu wa shule hiyo, Bw. Julius Shula, alisema wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya uchakavu wa miundombinu ambapo zaidi ya sh. bilioni moja inahitajika ili
kurekebisha iliyopo ambayo imechoka sana.

Alisema kama watafanikiwa kupata fedha hizo, wataweza kuirekebisha shule hiyo ili iweze kuonekana katika viwango
bora zaidi na kuongeza ufanisi wa elimu nchini.



No comments:

Post a Comment