06 February 2013

Serikali yajipanga kukomesha ujangili nchini


Na Godfrey Ismaely, Manyara

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amesema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuona matukio ya
ujangili nchini yanaongezeka siku hadi siku, muda wowote
ataagiza majeshi yote kushirikiana ili kudhibiti matukio hayo.


Hatua hiyo inatokana na Serikali ya Tanzania kusaidi dikezo maalumu na Serikali ya Marekani ambalo kushirikiana katika
kudhibiti matukio ya ujangili nchini.

Balozi Kagasheki aliyasema hayo jana mkoani Manyara katika
hafla maalumu ya uzinduzi wa Kituo cha Mapokezi kwa watalii ambacho kipo chini ya Jumuiya ya Usimamizi wa Hifadhi ya Wanyapori Burunge (WMA), Wilaya ya Babati, mkaoni Manyara, kilichojengwa na Marekani kupitia Shirika lake la  USAID.

Jana (juzi) mimi na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Bw. David Hayes, tulisaini dokezo hili kwa lengo la kukomesha matukio ya ujangili nchini,” alisema na kuongeza kuwa, matukio
ya ujangili yanaichafua nchi pia ni mateso kwa wanyama.

Alisema mapambano dhidi ya majangili yanawezekana ambapo Serikali imeanza kujipanga ambapo Rais Kikwete, wakati wowote atatoa uamuzi kamka Amiri Jeshi Mkuu wa nini kifanyike kudhibiti hali hiyo nchini.

Alisema suala la kucheleweshwa fedha zinazotokana na makusanyo ya WMA ambayo ni asilimia 50 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi, litafanyiwa kazi na wakati wowote mambo yatakuwa mazuri.

Kwa upande wake, Bw. Hayes ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi huo, alisema lengo la nchi yake kutoa ufadhiri
kwa jumuiya za WMA nchini, mbali ya kulenga kukomesha
ujangili pia jamii zitanufaika kupitia mapato mbalimbali.

“Kufanikiwa kwa WMA ni fursa moja wapo ya kukomesha kabisa matukio ya ujangili yanayotokea Tanzania, vitendo hivi vinachangia kuhatarisha usalama wa binadamu, wanyamapori na hata kutatiza shughuli za utalii,” alisema Bw. Hayes.

Balozi wa Marekani nchini, Bw. Alfonso Lenhardt's, alisema utaratibu wa wanajamii kuanzisha WMA nchini umeweza kuwa
na mafanikio makubwa, kuboresha miradi ya shule, zahanati na
kusomesha watoto kutokana na mapato yanayopatikana kutoka
kwa wawekezaji walioingia nao mikataba.

“Tangu mwaka 2006, WMA tisa zimeweza kuingia mikataba na wawekezaji binafsi katika sekta ya utalii ambapo zimefanikiwa kupokea zaidi ya dola za Marekani milioni tano kutokana na
shughuli za uwindaji na upigaji picha.

“Hatua hii imewezesha zaidi ya wanajamii 400,000 kunufaika kwa namna moja ama nyingine pamoja na kupata ajira hivyo Marekani itaendelea kuzijengea uwezo jumuiya hizi mara kwa mara ziweze kufikia malengo ya uhifadhi na maendeleo kwa wananchi,” alisema.

No comments:

Post a Comment