06 February 2013

Mabaharia 6 wahofiwa kufa majiNa John Gagarini, Pwani

MABAHARIA sita wanahofiwa kufa maji baada ya jahazi walilokuwa wakisafiria kwenye Habari ya Hindi kuzama.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei, alisema mabaharia hao walipanda
jahazi la mizigo na walikuwa saba lakini mmoja ameokolewa.

Alisema jahazi hilo linalofahamika kwa jina la Soweto, lilizama katika Visiwa vya Koma, eneo la Mwamba wa Chokaa, wilayani Mkuranga.

“Usajiri wa jahazi hili bado haujafahmika na lilikuwa na shehena
ya mbao na mirunda likitokea Kyasi kwenda Zanzibar,” alisema.

Aliwataja baadhi ya mabaharia wanaohofiwa kufa maji kuwa ni Ally Hasan, Hassan Mamba, Nasoro Isa, Abdala Said na Husein Huku wakati Hasan Rajab, aliokolewa na wanaendelea kutafutwa.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa polisi kawa wataziona maiti zinazoelea majini.

No comments:

Post a Comment