26 February 2013

PAMBO LA BOTI


Wapitanjia wakipita karibu na pambo la boti (juu kushoto) lililowekwa kwenye makutano ya Barabara za Msimbazi na Uhuru, Dar es Salaam jana. Manispaa ya Ilala imebuni mapambo kwenye makutano ya mitaa mbalimbali ili kulipendezesha jiji. (Picha na Charles Lucas)

1 comment:

  1. Ni njia nzuri wameitumia kwa kupendezesha jiji lkn naona wameenda hovyo kama mwananchi wa tanzania inatakiwa wangeweka sanaa mbalinbali za kutengenezwa na wasanii wetu na ziwe za kumbukumbu mbalimbali za kitaifa na hiwe kivutio na kumbukumbu tosha kwa kizazi kilichopo na kijacho mfano ile sanaa ya askari mpaka leo bado ipo na Kizazi kirichopita na kilichopo kinaona historia ya wazee wetu walipotoka na kijacho kitaikuta,kuna mambo mengi ya kihistoria ambayo yangetengenezwa na kuleta mahana kubwa na kumbukumbu kubwa sio ilo dau litapigwa jua na mvua baada ya miaka michache haritafaa tena,hebu waangarie makumbusho ya taifa mambo wanayoyafanya wanaifadhi vitu vya kale na kutengeneza sanaa za kuifadhi kumbukumbu muhimu kwa taifa mambo yaliopita ambayo jamii ya sasa inabaki kusoma ktk vitabu na kufikiria picha kwa hisia tu,mimi naona ilo ndio muhimu kwa taifa,mfano kwa hapo Dar sehemu kama hiyo wangetengeneza sdanamu za watu wakicheza ngoma ya Mdundiko wakubwa kwa wadogo nazani ingevutia watu wengi na kukumbusha wazawa wa mkoa wa Dar wazaramu walivyokua wanahenzi utamaduni wao ambao kwa sasa unaenda kupotea tena hauna miaka 10 haifiki hatutaona tena ngoma ya mdundiko ikipita mtaa kwa mtaa kama miaka ya 80 na zaidi,wadau naomba hili wazo wapelekewe uongozi wa jiji na meha wao,na watengenezaji wa kumbukumbu kama hizo tunawafahamu zaidi namba hii 0713610394

    ReplyDelete