05 February 2013

Mhasibu atoa ushahidi uvamizi KKKT



Na Rehema Mohamed

SHAHIDI wa tatu katika kesi ya kuchoma moto kanisa na uhalibifu wa mali zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 500, jana ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa, aliona kundi kubwa la watu wakivamia Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mbagara.


Alidai Oktoba 12,2012, alifika kanisani hapo asubuhi na baadaye aliondoka kwenda kuosha gari lake lakini Mchungaji wa kanisa
hilo alimpigia simu na kumwambia kuna vurugu kubwa eneo
la Mbagara Polisi.

Sahidi huyo Bw. Joas Joel ambaye ni Mhasimu wa Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS), ya kanisa hilo, aliyasema hayo
wakati akitoa ushahidi wake mahakamani hapo mbele ya
Hakimu Waliyarwande Lema, akiongozwa na wakili wa
serikali Bw. Tumaini Kweka.

Alisema baada ya muda, alirudi kanisani hapo ndipo kundi kubwa
la watu liliwavamia hivyo walilazimika kukimbilia katika nyumba
ya Mwinjilisti iliyopo katibu na kanisa hilo.

Alidai wavamizi hao mbali ya uharibifu walioufanya kanisani hapo, pia walivunja Ofisi ya SACCOS, kuima meza na kumpyuta moja aina ya Dell.

Aliongeza kuwa, Novemba 7,2012 aliitwa Kituo cha Polisi Mbagara na baada ya kufika, alionesha vitu vilivyoibiwa na kuvitambua kuwa ndivyo vilivyokuwa ofisini kwake. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 11 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na ushahidi
upande wa mashtaka.

No comments:

Post a Comment