20 February 2013

Kanisa lapigwa moto tena Z'bar *Walianza kulipiga mawe, wahusika wasakwa *Utaratibu wa kuyalinda na polisi waandaliwa


Na Mwajuma Juma, Zanzibar

WATU wasiofahamika, wamelishambulia kwa mawe na kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililopo eneo la Kiyanga kwa Sheha, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.


Tukio hilo limetokea juzi saa 9:30 usiku siku mbili tangu kuuawa kwa Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili Zanzibar, aliyepigwa risasi tatu kichwani na watu wasiofahamika.

Padri Mushi aliuawa wakati akishuka katika gari lake ili kwenda kuongoza ibada kwenye Kanisa la Betras ambapo wauaji hao,
walikuwa kwenye pikipiki aina ya Vespa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, ACP Augostine Olomi, alisema moto huo ulizuka kanisani hapo baada ya kikundi
cha watu watatu kuonekana wakipita karibu na kanisa hilo.

“Baada ya muda, mlinzi wa kanisa hili alisikia kishindo cha mawe juu ya paa hivyo alilazimika kukimbia na kwenda kujificha huku akiangalia kwa mbele kinachoendelea,” alisema Kamanda Olomi.

Aliongeza kuwa, wakati mlinzi huyo akiwa amejibanza mafichoni, aliona moto ukiwaka ndani ya kanisa ndipo alipopiga simu kwa kiongozi wa kanisa hilo ambaye naye aliwajulisha polisi.

Alisema baada ya polisi kufika eneo la tukio, walisaidiana na wananchi kuuzima moto huo ambao tayari ulishateketeza
thamani za kanisa na vitu vingine vilivyokuwa ndani.

Kamanda Olomi alisema, moto huo ungeweza kusababisha
athali kubwa kama usingedhibitiwa mapema ambapo dali zake
ambazo ni Gibsam, zimesaidia kuunusuru moto huo usifike
kwenye paa kuliteketeza kabisa.

“Wakati uongozi wa kanisa ukifanya tathmini ya hasara waliyoipata kutokana na moto huu, Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka wahusika wa tukio hili kwa kushirikiana na raia...hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa na uchunguzi unaendelea,” alisema.

Hata hivyo, Kamanda Olomi alisema jeshi hilo kwa kushirikiana na Vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, wataanza utaratibu wa kuyalinda makanisa yote ili kuzuia matukio ya aina hiyo.

Mlinzi wa kanisa hilo Bw. Mussa Jackson, alisema awali alikimbilia vichakani ili kunusuru maisha yake na baadaye alikwenda kuomba hifadhi nyumba jirani iliyopo katibu na kanisa hilo.

“Wakati nikiwa lindoni, ghafla niliwaona watu watatu wanakuja ambao sikuwafahamu...nilipojaribu kuwafatilia wakaanza kurusha mawe hivyo nikaamua kukimbia,” alisema Bw. Jackson.

Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo, Penuel Wisdom alisema alipokea simu kutoka kwa Bw. Jackson ya kuchomwa kwa kanisa hilo ambapo thamani zilizoungua ni pamoja na viti, meza.

“Hii ni hujuma ya pili kufanywa katika kanisa letu ambapo mwaka 2011, kanisa hili lilivunjwa na watu wasiopungua 50, hasara iliyopatikana ilikuwa sh. milioni 20.

Alisema tukio la sasa ni pigo kwa kanisa hilo ambapo zaidi ya waumini 100 wa kanisa hilo, watakosa mahali pa kuabudia.

Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar, PCI Yussuf Ilembo, alisema tayari wameanza uchunguzi wa tukio hilo ambapo hadi sasa, hakuna mtu aliyekamatwa.

7 comments:

 1. WAISLAM WANGEWEZA KUVUMILIA KAMA WANGEFANYIWA HAYA WANAYOYAFANYA? TUNAWAJUA NCHI INGEKUWA IMESHAWAKA MOTO.LAKINI SIKU MOJA MUNGU ATAWALIPA
  TU.MUNGU HUTETEA WANAO ONEWA.SIKU ZOTE ANAPOTAWALA RAIS MWISLAM,WAMEKUWA WAKIFANYA VURUGU ZA JINSI HII.

  ReplyDelete
 2. IKO KAULI KUWA USIPOPIGANA VITA VYA JIHADI SI RAHISI KUINGIA MBINGUNI KIRAHISI KUINGIA MBINGUNI SI LELEMAMA

  ReplyDelete
 3. February 21,2013 at 11:14pm
  NINAVYO ELEWA UKUBWA WA UNGUJA,SI KWELI KUWA WAHARIFU WALIOUNGUZA KANISA HAWAJAPATIKANA.MIMI SINA IMANI NA JESHI LA POLISI,YAWEZEKANA NAO PIA WANAHUSIKA NA HAYO MATUKIO.

  ReplyDelete
 4. TATIZO LA NCHI HII WANAPENDA KUTATUA MAMBO WAKATI WA DAKIKA ZA MWISHO NAAMINI IPO SIKU SERIKALI NA MAKAFIRI WA NCHI HII WATASEMA WENYEWE CHUKUENI HII HAPA ILE HAKI MLIOKUWA MNAITAKA BILA HATA YA KUSEMA MAANA MUDA WA KUPIGA KELELE NA KULALAMIKA UTAKUWA UMEKWISHA.

  ReplyDelete
 5. kweli sisi ni mabongo lala yaani afadhalli tunge warudisha wazungu waendelee kututawala coz wnyw hatuwezi ni ma bumbumbu kwa ujumla.

  ReplyDelete
 6. Mlikabidhiwa nchi ikiwa na amani na uchumi mzuri. Uchumi wetu hoi,amani imo mashakani. Mungu atunusuru kwani haya yanayofanyika ni matokeo ya kuficha maradhi tunasubiri kilio kituumbuwe?

  ReplyDelete
 7. Nchi isipotawaliwa kwa kufuata misingi ya haki na sheria matokeo yake ndiyo hayo. Tunakwenda wapi mbona tumepoteza mwelekeo?????? Turudi jamani watoto na wajukuu zetu watapiga bakora hata makaburi yetu watakapokuwa wanahangaika kusaka amani.

  ReplyDelete