07 February 2013

BFT kuongeza mabondia timu za Taifa



Na Mwali Ibrahim

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), linatarajia kuongeza mabondia zaidi katika timu za Taifa za wakubwa na vijana hivi karibuni.

Mabondia watakaoingizwa katika timu hizo ni wale walioonesha mkubwa katika michuano ya Klabu Bongwa yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 20, JKT Makao Makuu ilinyakua ubingwa huo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema wameona kuna umuhimu wa kuongeza mabondia katika timu hizo, kwa kuwa wengi walionesha uwezo wa kuzichezea timu za Taifa.

"Hatuwezi kuwaacha mabondia hao hivi hivi, kwa kuwa wana umuhimu mkubwa katika timu za Taifa, hivyo kuwaacha  ni kutowatendea haki," alisema.

Aliongeza kwa sasa Kamati ya Utendaji, ipo katika mchakato wa kupendekeza majina ya mabondia hao, majina yao yatapelekwa BFT.

Mashaga alisema, baada ya kuwachukua wataanza kuwapa mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali ya kiamataifa, watakayoshiriki.

Alisema ana imani kwa kuwaongeza mabondia hao, Tanzania itakuwa na timu nzuri na watakaoweza kutoa upinzani katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment