04 January 2013
Zitto atoa msimamo urais 2015
Na Reuben Kagaruki
WAKATI mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Edwin Mtei, akimtaka Naibu Katibu Mkuu
wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe, kumwachia Katibu Mkuu wake, Dkt. Willibrod Slaa, fursa ya kuwania urais mwaka 2015 kwa madai ndiye chaguo la watu kwa sasa, mwanasiasa huyo kijana (Zitto), amejitokeza na kuzungumza yaliyo moyoni mwake.
Kupitia mtandao wake wa kijamii, Bw. Zitto alisema, “Ninaulizwa sana kuhusu suala la urais 2015 baada ya kauli za wanachama waandamizi kunukuliwa wakizungumzia jambo hili”.
Alisema wote wanaotaka kusikia kauli kutoka kwake, moja ya maazimio yake mwaka 2013 ni kutoongelea kabisa suala la urais
wa 2015 na hatasema kitu kuhusu suala hilo hadi Katiba Mpya
itakapopatikana na chama chake kuweka utaratibu wa machakato wake,” alisema Bw. Kabwe kupitia mtandao huo.
Bw. Kabwe aliyasema hayo ikiwa ni siku chache tangu Bw. Mtei atangaze kuunga mkono kauli ya Bw. Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa), kuwa Dkt. awanie tena urais katika uchaguzi Mkuu ujao na yeye kujiondoa kwenye orodha ya viongozi wa chama chake ambao watawania nafasi hiyo.
Gazeti moja linalotoka kila siku (sio Majira), lilimnukuu Bw. Mtei akisema “Zitto ana haki ya kuonesha demokrasia ndani ya chama kwa kutangaza kuwania urais mwaka 2015 na ndiyo maana halisi ya chama chetu, kuonesha hisia si dhambi, kila mtu ana hisia zake”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
zitto karibu ccm
ReplyDeleteWABUNGE WAGOMBEE VIPINDI VIWILI TU IWE KATIKA KATIBA TUPATE MAWAZO MAPYA
Deletehamna kitu siasa za bongo. Ni ubinafsi tu. Wtz tupige kazi. Waza kwa kina chukua hatua mtz.
ReplyDeletezito we muha tuachie wenyewe kaskazini na chama chetu na uraisi baki hapo tulipokuweka uctake kutuvuluga kama msukuma shibuda tutamalizana na wewe
ReplyDeleteWeka sera na point tanzania haina ukabila nenda Kenya
Deletemawazo makavu
ReplyDeleteZitotoo, wewe kwanza siyo Mkaskazini na pili siyo mkristo sasa unang'ang'ania ni kwenye CHADEMA yetu? au unasubiri hadi tukufukuzeee?
ReplyDeleteSishangai hii ndio tabia yetu watz,bongolala baada ya kutoa maoni ya kujenga sisi tunatoa maoni kama mipasho ya akina Hadija kopa/mze yusufu.Hapa kweli tunahitaji msaada wa wamarekani kama kawaida!
Deletekweli hao wote sio chadema mmepandikizwa ionekane kuna mgogoro ndani ya chama hamtaisambaratisha chadema kama mlivyoifanya nccr na cuf mbinu zenu chafu wengi wamezibaini.
Deleteoraaa acheni swaga za ukabila nojipya tema point kwa faida yetu watz
Deletenyie wote mliotoa mwawazo haapo juu ni wanafiki na wazambiki wakubwa NYIE SIYO CHADEMA NYAUUUUU
ReplyDeletekwani we hujui historia ya chama? au we ndo sio CHADEMA? Acha UKASUKU WW.
DeleteHakuna mchadema hata mmoja hapo juu badala yake mnataka kuleta uchonganishi wa kitoto, zito ana akili nyingi zaidi ya hizo mnazotumia kumchonganisha.
ReplyDeleteHakuna kinachoongelewa ambacho hakipo
DeleteKUNA SHERIA ZILIZOANDIKWA NA ZILE AMBAZO HAZIJAANDIKWA. ZILE AMBAZO HAZIJAANDIKWA NDIYO ZINA NGUVU ZAIDI. MOJAWAPO ISIYOANDIKWA NI KUWA KAMA HUJATOKA MIKOA HIYO USISUMBUKE KUGOMBEA. JARIBU!
ReplyDeleteMh. Kaka yangu zitto umeongea maneno ya busara sana, na mimi shakiru wa mtwara, nakuomba usimamie msimamo huo huo, mpaka katiba mpya ipatikane.
ReplyDeleteKila mwanachama wa chadema anayo haki ya msingi kuwania urais kwanini anazuhiwa huyo zitto wamwache agombee na wajitokeze hata zaidim ya wa2 si harimashauri kuu hipo,itapiga kura kuonyesha demokrasia kumchagua wanaye mtaka atakaepata kura nyingi ndio mshindi hebu wanachadema tuwe na demokrasia wajitokeze wapambane tumpate m1 ambaye atatukomboa wanachadema na nchi yetu kwa ujumra.
ReplyDeleteMtaambulia kuwa wasindikizaji kila mwaka. Wasio wajua ndio wanaendelea kuwashabikia, UKABILA na UBINAFSI vimezidi.
ReplyDeletekila mtu anahaki ya kugombea uraisi,lakini mi naona hapa,taratibu zinapaswa kufuatwa ikiwemo kuchaguliwa na wanachama husika kupitia mikutano huru ya chama.suala la kujitangaza ugombea ni uhuni,na uzandiki chamani,hivyo kwa mtu kama zito anatakiwa atumie busara zaidi,kwani hata huko ccm kwenyewe wanautaratibu wa kutafuta wagombea wa uraisi kulingana na nyakati.
ReplyDeleteCHADEMA ndio chama mbadala ambacho kinaweza kututoa watanzania katika umasikini wetu kulingana na rasilimali tulizonazo! CCM wamegundua hilo ndio maana wamenunua gazeti la majira, mtanzania, na jambo leo ili kudhoofisha jitihadi za kuchukua dola 2015, lakini mmechelewa kwakuwa CHADEMA imejipanga vyema
ReplyDeletepositive attitude to everything is better than negative attitude to nothing
ReplyDeletewatanzania tunapaswa kupima,kudadavua swala zima la siasa zetu nikiwa na maana hii kukwepa kauli za uchochezi,ubaguzi,na kuwepo kwa kauli zisizo na msingi. tuwaze MAENDELEO KWANZA."we are still poor'
ReplyDeleteSijaona siasa za maana hata kidogo. Naona kuna kelele tu. Bado ipo kazi kuwajua 'wanasiasa na wanaharakati'.Uongozi si kitu cha ku-assess kelele za watu. Wengi hao ni 'wanaharakati'.Tufanye utafiti ili tujue hizo tafauti.Watu wanadhani unaweza kurupuka ukajiita "eti... mimi mwanasiasa..."Ni kinaweza ku-qualify?Kelele tu bila hoja za msingi?Eti hakuna maendeleo, nani mjinga leo hii utamweleza hayo na akaona kweli hakuna maendeleo.Siasa isionekane ni sehemu ya kuwatumia watu kama wale wa bodaboda na wamachinga ili upate ki-jimshahara cha miaka mitano. Kuna kazi nyingi za maana za kufanya.
ReplyDeleteNyero,
ReplyDeleteLeo hii naamini sana Watanzania wanauelewa mkubwa sana wa kujua nani angalau ana-utashi wa siasa.Sio sehemu ya kupata maisha. Utafiti unaonyeha hivyo.Wakati mwingine ni aibu kwa Mbunge kuonekana huna 'focus na determination'.Huna mawazo yanayooshewa wewe ni research oriented au una-kurupuka na malalamiko ya kijiweni.Wengi wana list ya matatizo na hawana solutions.Uongozi unataka ujue utatatuaje tatizo na kuwashawishi watu kuwa njia ya kweli ni A,B...Kwanini hatufunzi kutoka kwa watu wengine nje ya mipaka ambako tunaona kweli siasa zao zina akili.Unaweza onekana huna akili ukiwa utapinga tu bila hoja tafiti.Kwa mfano swala la Mtwara, lilichochewa na wahuni wachache wanaojiita eti wana-siasa.Hawezi kutoa hoja ambazo zitatoa solution. Hakuna hata kidogo.Watanzania wamejifunza kwa lile tukio na Mtwara.Wengi wanajiita wana-siasa, hapana hao ni 'wanaharakati'.
acheni ukabila wapuuzi nyie hivi mnataka kuturudisha wapi tena, ninyi wachaga hatuwapendi na ubaguzi wenu huo na CHADEMA. hIVI MNAJUA WAOLIOIPA CHADEMA JINA NCHI HII. NI WAKINA NANI KAMA SIO MAREHEMU CHACHA WANGWE NA ZITO. WEWE MBOYE UNAKURUPUKA CHADEMA KAMA NI SACCOS YAKO WAAMBIE WATU WAJUE NA SIO KUMINYA DEMOKRASIA. NI NANI KAKWAMBIA WAGOMBEA HUTANGAZWA MAJUKWAANI. ACHA KABISA
ReplyDeleteNAUNGA MKONO MAWAZOO YA MWENYEKITI WA CHADEMA KUMWACHIA DR. SLAA KUWA MGOMBEAWA URAISI MWAKA 2015, KWA MARA YA PILI.
ReplyDeleteDR. SLAA PAMOJA NA MAPUNGUFU YAKE KWENYE NDOA YAKE MAANA LAIZAM TUWEKE WAZI KUMWACHA MKE MWENYE WATOTO NAYE NA KUMCHUKUWA ALIYEKUWA MKE WA MTU HAKUFANYA VYEMA LAKINI TUNAMWONA ANAFAA KUTOKANA NA UWEZO WAKE MKUBWA ALIO NAO KATIKA SIASA. DR. SLAA ALIMPA JK WAKATI MGUMU NA NGOJA APEWE TENA NAFASI WAKATI KATIBA MPYA ITAKUWA IMETOKA TANZANIA NA ILE TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI ITAKUWA HURU NA MATOKEO YA UPIGAJI WA KURA NAYO YATAKUW HURU.
MUNGU IBARIKI CHADEMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
chadema mnajizalilisha kwa nini mnapenda ukabila na ndo maana mnamkataa zitto kwa sababu sio wa kaskazini mnatuchosha
ReplyDeletekuzugumzia ukabila ni upuuzi mkubwa katika nchi kama tz. kweli kumbe watu wengi ni maskini hata wa kufikiri jambo dogo kama la mustakaali wa taifa letu. nawaombea wapambanaji wote kuendelea na mapambano bila kuchoka. ccm kwaheri, yaonesha wafuasi wa ccm wanakkosa cha kuchangia.
ReplyDelete