03 January 2013
Wizara yasitisha ombi la uuzaji meno ya tembo
Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Maliasili na Utalii, imesitisha maombi ya kibali
cha kuuza meno ya tembo ili ipate muda wa kutekeleza masharti yaliyotolewa na Shirika la Kimataifa linalojihusisha na ulinzi wa wanyama walio katika hatari ya kutoweka duniani (CITES), yanayotakiwa kutimizwa ili kuruhusu uuzwaji wake.
Taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari Dar es Salaam jana
na Msemaji wa Wizara hiyo, Bw. George Matiko, alisema awali Wizara ilipeleka maombi CITES ya kutaka kuuza tani 101 za
meno ya tembo.
Alisema ili kufanikisha hilo, CITES iliomba tembo wa Tanzania washushwe kutoka Daraja la Kwanza la pili ili uuzajwaji wa meno hayo uweze kufanyika kwa taratibu za shirika hilo.
Aliongeza kuwa, vigezo vilivyotolewa na shirika hilo vinahitaji muda wa kutosha kuvitekeleza ambavyo baadhi yake ni kudhibiti ujangili wa tembo nchini na meno yake ambayo yanapitishwa
kutoka nchi jirani, kufanya sensa upya ili kupata takwimu mpya
za idadi ya tembo walioko nchini.
Bw. Matiko alisema ili kutekeleza vigezo hivyo, Wizara imeamua kusitisha ombi lake la kuuza meno ya tembo ambalo lingejadiliwa kwenye mkutano wa 16 wa CITES uliopangwa kufanyika Bangkok nchini Thailand, Machi 2013.
“Ombi la kuuza meno ya tembo litapelekwa tena katika Mkutano 17 wa CITES ambao utafuata baada ya ule wa Bangkok, Tanzania bado ina nia ya kuuza shehena ya meno ya tembo ili kujipatia fedha za kuendeleza uhifadhi,” alisema Bw. Matiko.
Aliongeza kuwa, meno yatakayouzwa ni yale yaliyotokana na tembo waliozeeka, kufa vifo vya asili na waliouawa baada ya kutishia maisha ya binadamu na mali zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment