03 January 2013
SUMATRA yawafariji wagonjwa kwa zawadi
Na Stella Aron
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imetoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye
thamani ya sh. milioni 2.2 kwa wagonjwa waliolazwa katika
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Hospitali ya Mwanayamala ili kuwafariji katika kipindi hiki cha sikukuu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo juzi, Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Bw. Ahmad Kilima, alisema
lengo la SUMATRA ni kuwafariji wagonjwa.
“Tumetumia fursa hii ya sikukuu kutoa zawadi kwa wagonjwa, msaada wa vifaa na dawa kwa akina mama waliopo katika wodi
za wazazi ili kuwafariji,” alisema Bw. Kilima.
Alisema mamlaka hiyo imelazimika kutembela MOI ambako kuna majeruhi waliopata ajali zilizotokana na vyombo vya moto ambao
ni wadau wao wakubwa.
“Majeruhi wa ajali kwa namna moja ni wadau wetu ndio maana tumewatembelea na kuwafariji, vifaa tulivyokabidhi ni dawa aina
ya Fefol kwa ajili ya kuwaongezea damu akina mama 100 ambao
ni wajawazito 100, pamba pamoja na kanga,” alisema.
Vitu vingine ni vipande wa sabuni aina ya detal kwa ajili ya watoto na ile ya maji, nepi, mafuta ya kupaka watoto wadogo, juisi, nguo
za watoto wachanga, sabuni za kufulia, karatasi laini na vitu
vingine mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment